masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 17,906
- 13,211
Kwa zaidi wiki sasa CRDB wamekuwa wakijitangaza kuwa wameanzisha programme ya mikopo hadi millioni 500 na payments ni hadi miaka 20.
Tatizo kubwa la mikopo ya benki zetu ni riba.
Katika kufuatilia nikapiga simu no 0755197700 kama ilivyoonyeshwa gazetini kwenye tangazo.
Siku ya kwanza simu hiyo haikupatikana kabisa!
Nilipopiga simu hiyo leo ikapatikana na baada ya muda mrefu dada mmoja akajibu.
Swali langu lilikuwa simple and straight.
Mikopo yenu ina riba kiasi gani?
Jibu la mkato lilotoka ni hili: Nenda kwenye benki yako na meneja atakujibu>
Nikamuuliza sasa nini maana ya kuweka simu kwenye tangazo? Maana tunataka majibu bila kusumbuka mafoleni!
Jibu: Inategemea mshahara wako!
Nikauliza tena: Mimi si mwajiriwa mi mfanya biashara na nataka mkopo lakini vizuri kujua riba!
Jibu:(baada ya kimya) kwani unataka mkopo kiasi gani?
Nami nikajibu: Milioni mia tano.
Bibie naye akajibu: Nenda kwenye tawi lako watakusaidia.
Nika endelea: Sasa mnaweka simu kwenye tangazo kwa nini wakati hamna majibu simple kama ya riba?
Jibu:..............(akakata simu)
Nikakaa chini na kufikiri, CRDB Benki inayosikiliza !