CRDB kukata watu mikopo bila kutowapa hela ya mkopo ni unyanyasaji na wizi

Ndokeji

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
698
475
Kuna Mtumishi wa umma aliomba mkopo bank ya CRDB amejikuta anaingia kwenye ATM, na kukuta amekatwa hela ya mkopo huku hela hiyo aliyoomba hajapewa, amewafuata CRDB wamemwambia watamuwekea tu, akawauliza ni lini wakamjibu mda wowote, sasa hiki kitendo ni wizi na uonevu mtu anaishije unamkata mkopo huku hujamuwekea kiasi alichoomba? Hebu CRDB tupeni ufafanuzi wa hili jambo.
 
Unataka jibu gani zaidi ya hilo ulilopewa na CRDB pale ulipouliza hapo awali baada ya kukuta umekatwa huo mkopo na umeambiwa utawekewe wewe tulia tu
 
Hapo kuna sehemu mawasiliano ya watendaji wa crdb yamepishana, hilo ni tatizo ila kwa kua umewambia watasgughulikia soon.
Japo inaboa ila watashughulikia usiwe na wasiwasi kabisa, hizo ni mistake mkuu kumbuka zile kazi zinafanywa na binadamu wa kawaida kama mimi nawewe
 
Kuna Mtumishi wa umma aliomba mkopo bank ya CRDB amejikuta anaingia kwenye ATM, na kukuta amekatwa hela ya mkopo huku hela hiyo aliyoomba hajapewa, amewafuata CRDB wamemwambia watamuwekea tu, akawauliza ni lini wakamjibu mda wowote, sasa hiki kitendo ni wizi na uonevu mtu anaishije unamkata mkopo huku hujamuwekea kiasi alichoomba? Hebu CRDB tupeni ufafanuzi wa hili jambo.
Utawekewa tu mkuu
Usiwe na shaka kama umejibiwa na wahusika hapa hatutakuwa na jibu sahihi zaidi ya hilo
 
kisingizio ni kuwa walisitisha kufuatia yale majina ya watu wenye vyeti feki yaliyotolewa hivi karibuni. Nimepitia mikataba yao ni KAMA WAMEVUNJA TERMS AND CONDITIONS

KISHERIA wanaweza kishitakiwa na kulipa. haiwezekani mtumishi akatwe na zmigo hajawekewa kama walijua wanasitisha ilibidi wakawitdraw makato kwa afisa utumishi.

NAWASHAURI WALIOKUTWA NA SAKATA HILI WASHUGHULIKIE MAPEMA ILI WASIJE KUKATWA TENA KWENYE MISHAHARA IJAYO

hatua za kuchukua ni kuhakikisha loan officer wanaenda kuondoa makato kwa afisa utumishi(ikiwa tu tarehe ya ku release mikopo haijulikani. manake mtumishi anaweza kuzungushwa mpaka mwezi wa sita ukakatika hivihivi)
 
kisheria haikubaliki inabidi upewe mzigo.MOJA YA MAJIBU WANAYO TOA LOAN OFFICERS NI KUWA HICHO KIASI KILICHOKATWA KWA MWEZI HUU KITARUDISHWA KWENYE ACCOUNT YA MTEJA
Utawekewa tu mkuu
Usiwe na shaka kama umejibiwa na wahusika hapa hatutakuwa na jibu sahihi zaidi ya hilo
 
inabidi hata mie yamenikuta NBC inabidi hizi bank zikemewe ni uonevu
shemeji yangu alitaka ku cancel kufuatia ubabaishaji kama huu kaambiwa aandike barua kwa meneja na kisha atakatwa kitu kama laki moja na vijisenti ili mkataba usitishwe
 
Watwange "demand note" ya siku hata 7 wairudishe au wakupe mzigo kama bado unahitaji. Baada ya hapo fungua madai uwakomoe pia.
 
nipe utaratibu wa hii kitu mkuu hatua kwa hatua.

hawawezi kukiuka masharti afu wajibu hovyohovyo tu majibu yasiyo kuwa na uhakika wa lini wana release mzigo.
 
Andika hiyo barua ukiwataka watekeleze N dani ya muda utakao wapa.Waambie wazi wasipotekeleza kwa wakati hatua zipi utachukua(kufungia shauri).Hii itakupa haki ya kulipwa gharama ya shauri utalofungua. N.a. ili kuwa n.a. uhakika wa ushahidi wape kwa despatch au pata huduma ya wakili
 
Kuna Mtumishi wa umma aliomba mkopo bank ya CRDB amejikuta anaingia kwenye ATM, na kukuta amekatwa hela ya mkopo huku hela hiyo aliyoomba hajapewa, amewafuata CRDB wamemwambia watamuwekea tu, akawauliza ni lini wakamjibu mda wowote, sasa hiki kitendo ni wizi na uonevu mtu anaishije unamkata mkopo huku hujamuwekea kiasi alichoomba? Hebu CRDB tupeni ufafanuzi wa hili jambo.

Aisee!!! Mimi ningelala hapo bank hadi kieleweke.
 
Itakuwa ni bahati mbaya
sio bahati mbaya walisitisha kutoa mikopo siku chache baada ya ile orodha ya majina ya wenye vyeti feki kutolea

sasa kilichotokea ni kuwa makato yalikua tayari yameingizwa kwenye mishahara ya wakopaji

swali linakuja kwanini hawataki kusema lini sasa wataachia hiyo mikopo?
 
Issue ni simple toa notes ya kisheria upate haki yako kama unaona inachelewa.
 
Ndo utaratibu mpya ili kujua kama upo kwenye payrol wanakata kwanz ndpo upewe hela ni Benk zote nchini maagizo toka hazina vumilia utapewa tu hela yako
 
kumbe? baada ya makato sasa huo mchakato unachukua miezi mingapi mpaka mzigo kuingia?
 
Back
Top Bottom