CRDB BANK na saa za kazi Kisheria

FREIGHTLINK

Member
Apr 11, 2016
19
7
Habari. Napenda kujua, Sheria ya Kazi inataka mfanyakazi afanye kazi saa ngapi kwa siku?

Wafanyakazi wa CRDB Bank hasa Tawi la Premie huwa manatakiwa saa 1:30 asubuhi wawe wako ofisini. Inawezekana matawi mengine ni hivyo pia. Wafanyaka wa BanknaTawi husika hutoka saa 12 au saa1 usiku. Kwa sasa wanatoka ofisini saa 3 usiku. Cha kushangaza hakuna malipo ambayo wanalipwa kwa kukaa ofisini saa zote hizo.
 
Lakini wao waliandika ktk barua ya ajira iam able to work in challanging environment so why are you complaining mwisho ulisema

Your faithfully

Mtoa uzi
 
'..I can work under challenging environment, odd hours with minimum supervision..'

Vumilia mkuu,ukikaidi, acha kazi uone ilivyo kazi kupata kazi!

Kwa nafasi yako moja, kuna watu around mia na hamsini wanaitolea macho (wengine ni majobless, wengine wanafanya sehemu nyingine wanataka kuhamia hapo, wengine wapo hapo hapo ila nafasi za chini wanataka kupanda kuja ulipo, wengine wapo mikoani wanataka kuhamia mjini na wao, wengine wapo vyuoni wanaota kufanya kazi yako siku moja)!

Hatari sana!
 
Vijana wakitanzania tusipojifunza kufanya kaz kwa bidii na maarifa ajira zetu wakenya watazikomba. Tumshukuru Mungu tumeajiriwa wenzetu maelfu wapo nje bila kazi.
 
Sheria ya kazi inatamka wazi kua kufanya kazi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni masaa 9 kiwango cha juu(max) Tena inatamkwa kua ukifanya kazi kwa masaa 6 mfululizo unatakiwa upewe lisaa limoja upumzike baada ya hayo masaa 6 ya kwanza. Mwajiri anaweza kukubaliana na wewe ukaongeza nusu saa yaani dk 30 tu. Zaidi ya hapo mwajiri anatakiwa akulipe kama muda wa ziada(over time) kwa kila lisaa litakaloongezeka.
Sasa kibongo bongo huwa tunaacha sheria na kufata mazigira ya kazi. Ila siku utakayovunja sheria tambua muajiri atakujulisha sheria na adhabu utaipata. Kama umedhamiria kabisa kukomesha suala la kufanyishwa kazi masaa mengi, ongea na mwajiri wako juu ya hilo ukowa na vieleleO vyako na mwambie una nia ya kumpeleka kwenye baraza la usuluhishi au akupatie stahili zako.
 
Lakini wao waliandika ktk barua ya ajira iam able to work in challanging environment so why are you complaining mwisho ulisema

Your faithfully

Mtoa uzi

Acha kazi

'..I can work under challenging environment, odd hours with minimum supervision..'

Vumilia mkuu,ukikaidi, acha kazi uone ilivyo kazi kupata kazi!

Kwa nafasi yako moja, kuna watu around mia na hamsini wanaitolea macho (wengine ni majobless, wengine wanafanya sehemu nyingine wanataka kuhamia hapo, wengine wapo hapo hapo ila nafasi za chini wanataka kupanda kuja ulipo, wengine wapo mikoani wanataka kuhamia mjini na wao, wengine wapo vyuoni wanaota kufanya kazi yako siku moja)!

Hatari sana!
Umaskini ni mdudu mbaya sana. Hii yote ni sababu ya umaskini.
 
Habari. Napenda kujua, Sheria ya Kazi inataka mfanyakazi afanye kazi saa ngapi kwa siku?

Wafanyakazi wa CRDB Bank hasa Tawi la Premie huwa manatakiwa saa 1:30 asubuhi wawe wako ofisini. Inawezekana matawi mengine ni hivyo pia. Wafanyaka wa BanknaTawi husika hutoka saa 12 au saa1 usiku. Kwa sasa wanatoka ofisini saa 3 usiku. Cha kushangaza hakuna malipo ambayo wanalipwa kwa kukaa ofisini saa zote hizo.
Mhm...wewe haya umeyajuaje? Au una Mke anafanya kazi huko
 
Back
Top Bottom