CRDB Bank mtapoteza wateja kwa ubabaishaji

CRDB Bank mtapoteza wateja kwa ubabaishaji

vevenononombo

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2015
Posts
1,289
Reaction score
421
CRDB bank, inabidi ijitazame upya namna inavyowahudumia wateja wake tofauti na hivyo tutawahama muda si mrefu, kwani kuna mambo mengi hayako sawa kwa sasa nitataja mambo makuu manne yatajayowakimbiza wateja kwenu.

1. Huduma kwa mteja(customer care ) mnatumia muda mrefu sana kumjibu mteja zaidi hata ya dk 15 wakati mteja anakatwa kwa hiyo gharama na mkampuni ya sim au ni deal na makampyni hayo kunyonya wateja.

2. Huduma ya Sim Banking sio imara kwani unaweza tumia lkn fedha usipate muda huu huo.

3. Kuna wafanyakaz wanapitishia mishahara yao ktk bank yenu tena wahasibu wanajitahid kupeleka yote yanayoitajika kwenu kabla ya tarehe 20 lakini mishahara inachelewa kwa zaidi ya siku saba.

4. Atm mashine zenu zimekuwa na tabia ya kuandika kuwa kadu hii haitumiki kwenye mashine hii sijui tatizo ni nini?.

N.B msipojirekebisha mishara yetu tutahamishia bank zingine na niko serious ktk hilo.
 
Jiunge na benki tu kama unafanya bishara inayohitaji kupitishia pesa benk au kama unafanya kazi na wanapitishia mshahara benki azawais godoro lako ukiongeza na M PESA Ni mahala pa usalama zaidi. Godoro halina benki charges, halina foleni, halina system down, huwezi kuibiwa kimtandao n.k
Kama humwamini wife hela zako weka mpesa. kama mnaaminiana weka kwa godoro. hakuna atakae kukuvamia nyumbani kama hutatangaza kwamba unahifazi pesa kwenye godoro
 
Ni kweli hasa tawi la mlimani city wanaboa sana, natafuta bank nzuri nihamie. ATM za crdb cku hizi co reliable tena
 
Mimi mastercard Yao nisha ivunja we toka mwez wa pili mpaka Leo nafatilia card ifanye manunuzi online kila siku wananiambia utatumiwa meseji mpaka Leo kwel..yaan pesa yangu initese kutafuta na wenyewe wanitese for no reason Sipo tayari.
 
Tutalifanyia kazi wadau msiwe na wasi wasi heri chizi ulie mzoea kuliko chizi mgeni
 
Mimi tayari nimeshafungua akaunti Barclays. Japo ni service charge ni gharama, lakini nina uhakika hakuna wakati wowote nitakose pesa kwenye ATM, na kwamba hakuna siku nitakuta foleni benk.
 
Na customer care wao wana mdomo mchafu na hawajui kushughulikia mahitaj ya mteja...pumbavu zao
 
Jiunge na benki tu kama unafanya bishara inayohitaji kupitishia pesa benk au kama unafanya kazi na wanapitishia mshahara benki azawais godoro lako ukiongeza na M PESA Ni mahala pa usalama zaidi. Godoro halina benki charges, halina foleni, halina system down, huwezi kuibiwa kimtandao n.k
Kama humwamini wife hela zako weka mpesa. kama mnaaminiana weka kwa godoro. hakuna atakae kukuvamia nyumbani kama hutatangaza kwamba unahifazi pesa kwenye godoro

Mawazo ya kimaskini haya,tumia benki wewe that's worldwide means ya kusecure pesa yako
 
Sasa ukiweka pesa kwenye godoro na dunia ya sasa ivi tunakwenda kutumia kwa credit card kufanya purchases so utaishije mkubwa?
 
Mnasubiri nn kuhama? Mimi binafsi nina miaka miwili sasa ile akaunti ilopo kwao imekua ya kukusanyia madeni tu mambo mengine nafanyua NMB na hivi wameleta hizo Master cards na wao sitarudi nyuma tena
 
ACB au TPB vip?

ACB wako poa sanaaaa, tena kijitonyama is best,all though wako slow kdgo mule ndani ila customer srvices zao nzuri sana, shda tu kama unahitaji hela weeknd kutoka ATM utazunguka kdgo bt no worries, low bank charges..its good
 
Sasa ukiweka pesa kwenye godoro na dunia ya sasa ivi tunakwenda kutumia kwa credit card kufanya purchases so utaishije mkubwa?

Purchases gani wewe kijana ? Mahitaji yangu napata soko la urafiki pale kila kitu ni cash peke yake. Kariakoo maduka ya nguo na bodhaa za viwandani ni cash peke yake. Isitoshe nilikushauri utumie M PESA pia hii itakusaidia kulipia maji na umeme. Banks are becoming obsolete my dear boy. Believe me. Katika kipindi cha miezi hii sita iliyopita benki wamepungukiwa wateja kwa asilimia 30. Soma majarida. Watu wanarudia utamaduni wa kuhifadhi pesa kwenye magodoro na kwenye MPESA
 
Back
Top Bottom