CRDB bank mnaturudisha miaka ya 90

Mkuu hiyo ni for your own security. Na hasa kama una draw zaidi ya million 5. Na mara nyingi hufanya hivyo kama account yako haina mazoea ya kutolewa hela sehemu zaidi ya ulipofungulia.

Ukifanya transactions kama hizo zaidi, basi wanakuwa hawafanyi tena hivyo.

Vumilia mkuu.
Ni usumbufu kwa mteja waangalie means nyingine lakini sio kwa utaratibu huo kwani ni hatarishi pia kwa mteja ikitokea mmoja wa watumishì wa crdb sio muaminifu na kuniungia zengwe nje ya bank.

Kwa utaratibu huo inatia hofu na shaka kwa mteja.
 
Nina account CRDB zaidi ya miaka 15 Mara nilipohama kutoka NBC sijawahi kupata shida yoyote.

Natoa pesa Tawi lolote na ATM yoyote bila shida Mara moja moja sana unaweza kukuta pesa hakuna au mtandao hakuna ktk ATM.

Na CRDB wameboresha sana Huduma zao ukilinganisha na miaka ya nyuma
 
Mkuu njoo equity bank. Ukifungua account wanachukua fingerprint yako. Baada ya hapo unakua huru kuchukua fedha kwenye branch yoyote bila kuwa na haja ya kuwasiliana na tawi lako....maana wakati wa kuchukua wanascan fingerprint na papo hapo system inaconfirm kama ni wewe au laa. Hakuna blaa blaa
 
Na ukilinganisha katika huduma kati ya crdb bank na nmb bank
Kwa kuanzia mwaka 2016 katika huduma yupi anafanya vizuri katika huduma za kibennki kwa wateja ambao sio waajiriwa wa serikali
 
Back
Top Bottom