Crdb bank Mlimani City rushwa nje nje! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Crdb bank Mlimani City rushwa nje nje!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ABEDNEGO, Jan 16, 2012.

 1. ABEDNEGO

  ABEDNEGO Senior Member

  #1
  Jan 16, 2012
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 109
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nawasilisha hii ni kero iliyokomaa pale CRDB Mlimani City, Kumbe hata uwahi kiasi gani huwezi kupata namba za kwanza kwanza ili kukaa kwenye foleni ya kupata huduma ya kibenki.Kisa ni washikaji wale wawili askari na binti mmoja walioko pale mlangoni kwenye mizani ya kutolea namba!! Huwa wanatoa namba za mbali kama 60,70 nk na zile za karibu 1,2,3,nk wanakuwa nazo kuwauzia wateja wale wenye haraka zao na wasiotaka kupanga foleni li wapatei huduma za haraka. Mchezo huo mchafu hufanywa kwa tactics za hali ya juu hata wakati mwingine kuwahusisha wateja.Bei ya tikiti ya namba hufika hadi 5,000/=, mara nyingi book mbili, tatu na nne.Uongozi wa Benki wanajua maana husema "mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake"!!Ndg zangu wateja wengine kero hii mmeiona? Mwasemaje??
  Mengi mengi yameongelewa hapa kuhusiana na thread hii ya kujenga na ya kupotosha kuhusiana na na utoaji rushwa na upokeaji katika kupata huduma za kibenki pale tawi la CRDB Mlimani City. Ukweli ni huu kwamba mimi binafsi nimehakikisha jambo hili zaidi ya mara mbili na kutoa taarifa za mdomo kwa counter,mara ya kwanza ali ni ignore mara ya pili yule dada aliniambia ataustua uongozi urekebisha hali hiyo.Tatizo ni kwamba hiyo electronic gadget kwa ajili ya kutoa na kupanga haifanyi kazi mara nyingi na hata ikifanya basi kuna kila uwezekano wa kuvuruga taratibu zake.Utakuta wateja wamejikalia tuu kusubiria huduma huku wengine wakiingia na kupanga foleni na kupata huduma chap chap.Swala la rushwa Mlimani City Branch linajulikana kwa wateja wengi ambao hupata huduma za kibenki mahali pale.Jana baada ya post hii kusomwa askari wa pale mlangoni aliniambia mambo si shwari nipange foleni ya kawaida bila rushwa,Kwa hiyo JF imesomeka na wala si majungu kama wengine walivyodai ni habari ya kweli iliyofanyiwa utafiti wa kina na kuripotiwa.Shime watanzania tupige vita rushwa kwani ni adui namba moja wa maendeleo[​IMG] anayeturudisha nyuma.Ushindani wa mabenki hauzuii kuipiga tafu benki yetu isonge mbele.Nime experience tatizo la CRDB mbali na kutokuwa na customer care,Wamelewa wingi wa watejakiasi kwamba hawathamini kabisa.Na wasijue wingi huo wa wateja ndo unawapandisha chat na kuwaongezea tija. Siku nyingine nilienda tawi la Vijana pale Lumumba.Mhudumu anaongea na mteja rafiki yake dirishani kwa muda wa nusu saa huku wateja wengine wakipiga kelele mbona hawapatiwi huduma.Ilibidi nimwone Meneja akamweendea na kumwambia atoe huduma. Nawasilisha na kuwashukuru wote mliochangia na uongozi wa CRDB Mlimani City kwa kuchukua hatua.Mode funga mjadala!!
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jan 16, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kama jambo hili lina ushahidi nenda moja kwa moja kwa Branch Manager umweleze...naamini atasaidia kama hayumo kwenye mgao!
   
 3. Panga La Shaba

  Panga La Shaba JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2012
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 209
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu ABEDNEGO Bank ziko nyingi using'ang'anie CRDB tu kama uridhiki na huduma zake........
   
 4. ULUMI

  ULUMI Member

  #4
  Jan 16, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dosari ya jinsi hii isimfanye mteja kukimbia Benki ili hali inarekebishika.Wahusika watasoma hapa na wachukue hatua mara moja!!!!Tusilee rushwa katika jamii zetu!!
   
 5. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #5
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 935
  Trophy Points: 280
  sasa?
  Kama auto-caller ikishaita namba na kuziona hazina mwenyewe si inawacha kuitisha na kuendelea na namba za mbele. Halafu huyo mjasiriamali analaza ndaza? Anyways, mjini maisha magumu, wakale wapi hao wandugu?
   
 6. s

  sawabho JF-Expert Member

  #6
  Jan 16, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Wasiliana na Vijana wa E. Hosea upewe book 5 yenye namba maalum, maana aina hiyo ya rushwa huwa inashughilikiwa haraka sana.
   
 7. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #7
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Acha fitina na majungu, serious issues unazi-bypass unaleta majungu, zungumzia kwenye hospitali zetu wagonjwa wanavyokosa matibabu au watoto wetu na shule za chini ya miti aghhhhhhhhhhhhhhhhhhh kaa foleni au weka vijisenti vyako mchagoni
   
 8. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #8
  Jan 16, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ndio wewe msomi wa UDSM uliyefukuzwa? au nakufananisha?sasa kwa mawazo kama hayo hapo juu kwa wasomi kama nyie tunawategemea na mnasoma kwa kodi zetu je tutafika?au ndo uwezo wako wa kufikiri kwa jambo kama hilo ndo umefikia hapo?na je ingekuwa wewe ndo meneja wa hiyo CRDB bank ndo majibu hayo ungetoa kwa wateja?
  Kazi tunayo...
   
 9. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #9
  Jan 16, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Hii ni Hatari sasa Rushwa mpaka kwenye kupanga foleni, hiyo Bank haifai kabsaaaaaa. Ushauri nakupa hama hiyo Bank kabla hawajazimaliza pesa zako kwa rushwa. Bank ya Kifisadi hiyo. Mimi nimeshakimbia natumia FNB huduma zao ni bora kuliko hao CRDB
   
 10. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #10
  Jan 16, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Inshu ulishaisema hapa, lazima watafuatiliwa kwa karibu. Na kuna hatari ya watu kupelekwa sehemu isiyokuwa na wateja! kama kweli wanafanya huo mchezo wanakiuka maadili ya kazi zao.
   
 11. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #11
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu vipi na wewe ni mhusika wa mgao huo? Majungu gani aliyoleta hapa? Yeye kakutana na kero hiyo kaileta hapa, basi kama na wewe unazijuwa kero zingine basi na wewe unalo jukumu la kuzipigia kelele.
   
 12. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #12
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  Manager kibongo bongo hana meno ya kung'ata
   
 13. ULUMI

  ULUMI Member

  #13
  Jan 16, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wana JF hayo madogo ndo huzaa makubwa tusi under rate rushwa hata kama ya kalamu ni RUSHWA tuuu ,Mtu huyo ukimkabidhi TANESCO lazima aifisadi kwa nafasi yake kama walivyo wa Richmond.Fichueni Rushwa zote na kwa mapana yote .BRAVO ABEDNEGO!!!!
   
 14. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #14
  Jan 16, 2012
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Wezi sana crdb, pale branch ya mikocheni ndo usiseme...ukienda kutoa hela nyingi lazma upoteze kilo mbili au tatu...nimepigwa mara 3 pale na jamaa zangu wanalalama ikabidi tuchukue internet banking ili tuhamishe wenyewe wezi sana, nimeshaireport kwa masupervisor wao lakini wanabebana...

  Nilikua naitumia sana ile branch kwa sababu haina foleni lakini toka waanze huo mchezo mchafu nimeachana nao. Shame on you.
   
 15. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #15
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 935
  Trophy Points: 280
  ndo mie mama. Wala hujakosea...
  In fact nina uchungu sana na tatizo la rushwa, ila linahitaji suluhisho la muda mrefu kuliko kuishia kuwakomalia walinzi wa magetini ambao wakati mwingine kupokea kwao rushwa kunachangiwa na ugumu wa maisha. Kama mlinzi analipwa 180k kwa mwezi, labda na viposho vya CRDB ambavyo havizidi 50k, na maisha haya ataishije?
  Wakati mwingine fikiria kuwa huyo ni mumeo, halafu kila asubuhi unataka kodi ya meza... Akikuambia "...kama hutaki piga mbizi" utamlaumu?
  Muwe munafikiria na upande wa pili wakati mwingine.
   
 16. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #16
  Jan 16, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  To shift is not a principle solution. See a branch manager
   
 17. Msolopagazi

  Msolopagazi JF-Expert Member

  #17
  Jan 16, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 659
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Du hii noma bora kuhama bank
   
 18. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #18
  Jan 16, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160

  Kuhama bank siyo solution kwani utakapohamia nako kukijaa wanaanza hizo style matokeo yake utalazimika kuhama tena!! Just face the facts, muone branch manager mweleze, sema tatizo hapa ni kuwa "wahanga wengi wa hili tatizo ni sisi wenye pesa ndogo ndogo ambazo unakuta ukienda kwa manager, utaishia kupata aibu. Lakini pamoja na hayo, ni muhimu tukaanza kufundishana kupeana heshima haijalishi una pesa kiasi gani, au unatoka wapi au unajuana na nani pale bank. Ni jambo dogo tu "Ubinadamu".
  Hao wanaokula rushwa ndogo ndogo, siyo kwamba zinawasaidia sana la hasha! ukifuatilia utakuta wanaishia migombani au kwenye viguest bubu. Ni mara chache utakuta wanafanyia mambo ya maana, believe me.
   
 19. Fighter

  Fighter JF-Expert Member

  #19
  Jan 16, 2012
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 611
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Pale panbore noma! mtu aikatiki, napenda exim ya pale!
   
 20. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #20
  Jan 16, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  You are wrong!. Huwezi kuita haya majungu, watu kama hawa wanatafuta hela hata sehemu zisizostahili ni chanzo cha failure katika taasisi nyingi sana. Watu makini wakiona upuuzi kama huu huwa hawakai kimya, ukikaa kimya unakuwa sehemu ya tatizo. Mi nampongeza mtoa mada kwa hili maana watanzania tumekuwa na tabia za ajabu sana. Hatuangalii tena reputation ya waajiri wetu bali tunaangalia how much can we gather in a short time hata kama kwa kufanya hivyo kutapelekea kuua nguvu za mwajiri na kutupotezea ajira siku za mbele.

  Vita dhidi ya rushwa si kuwa watch dog kama TAKUKURU iliyo strong. Vita dhidi ya rushwa itafanikiwa kwa wote kuikataa kwa vitendo na moja ya njia ya kuikataa ni kumuweka Public yeyote anayeendekeza mchezo huo. Ule usemi wa kumshitaki mtu utamuharibia kazi na kumuonea huruma tuuache, mtu anapaswa kujionea huruma mwenyewe kwa kuepuka vitendo vyovyote vitakavyohatarisha ajira yake.

  Wenzetu wamefanikiwa kuipunguza kwa asilimia kubwa kwa kuwa wananchi hawaoneani aibu, ukimuomba rushwa anakuripoti na akikuripoti unawekewa mitego kama kufungiwa secret CCTV eneo lako la kazi na kukusanya ushahidi wote wa kukutimua kazi. Customer care ni issue ambayo inapewa nafasi kubwa sana katika maisha ya biashara.

  Tuache kutetea upuuzi kama huu maana muda watu wanaotumia bank kwa kutotoa rushwa ungeweka kutumika kuzalisha zaidi na kuwafanya wateja waongeze akiba zao bank na hivyo kuongeza bank's liquidity badala ya watu kutoa pesa zao.
   
Loading...