IFUNYA
JF-Expert Member
- Nov 18, 2011
- 363
- 132
:ballchain:
Uongozi wa benki jaribu kurekebisha kero hizi. Mnatuhabisha na kutukela sisi wateja wenu.
Nawasilisha hii ni kero iliyokomaa pale CRDB Mlimani City, Kumbe hata uwahi kiasi gani huwezi kupata namba za kwanza kwanza ili kukaa kwenye foleni ya kupata huduma ya kibenki.Kisa ni washikaji wale wawili askari na binti mmoja walioko pale mlangoni kwenye mizani ya kutolea namba!! Huwa wanatoa namba za mbali kama 60,70 nk na zile za karibu 1,2,3,nk wanakuwa nazo kuwauzia wateja wale wenye haraka zao na wasiotaka kupanga foleni li wapatei huduma za haraka. Mchezo huo mchafu hufanywa kwa tactics za hali ya juu hata wakati mwingine kuwahusisha wateja.Bei ya tikiti ya namba hufika hadi 5,000/=, mara nyingi book mbili, tatu na nne.Uongozi wa Benki wanajua maana husema "mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake"!!Ndg zangu wateja wengine kero hii mmeiona? Mwasemaje??
Uongozi wa benki jaribu kurekebisha kero hizi. Mnatuhabisha na kutukela sisi wateja wenu.