Mkuu, labda ni maagizo toka juu, au tozo mpya ya Tra..Nianze kwa kuwasalimia wapendwa wangu wa jamii forum kwa kuwapa pole na majukumu ya hapa na pale kwaani bila kuhangaika na kujishughulisha basi unakuwa mzigo kwa taifa na kwa familia yako kama sio kwa jamii.
Wakati naajiriwa nilifanya tafiti naweza kusema mbaya kwa vile niliangalia sababu moja pekee ya kwanini nijiunge na CRDB na sio bank nyingine na ndio bank niliyotumia wakati wote wa masomo yangu.
Niseme tu kwamba CRDB wateja wenu mmewapa mzigo mzito kwaani makato yenu sasa ni maumivu kwa wateja na yanatutesa kupita kiasi na hadi sasa nipo njiani kimawazo katika kuhama bank yenu na nijiunge hata na NMB kwaani wizi tunaofanyiwa yatosha kusema haufai kwa taasisi yoyote ambayo kwao mteja ni mfalme.
Mwezi uliopita bahati nzuri au mbaya kwa yaliyonikuta sikuchukua mshahara wangu nikiwa na maana sikutoa fedha zangu za mshahara lakini jana nikaomba taarifa ya akaunti yangu hakika nimepata hasira mbaya moyoni mwangu na ya kusikitisha sana. Akaunti yangu kwa mwezi 12/2020na 1/2021 nimekatwa sh 52,000 eti fedha za makato ya kuendesha bank, na tarehe 19.01.2021 nimekatwa 15,000 kwa wakati mmoja hakika mnatuibia sana enyi makaburu weusi.
Hivi kwanini mjiangalie nyinyi tu na msituangalie hata sisi akina bora kunakucha and days goes?? Je makato haya yanatija kwa mteja wenu?? Na je kama mteja hana fedha kwenye akaunti mnaendeshaje bank??
Maamzi yangu ni kwamba kama sitawahama on the sport basi fedha zangu nitazitunza kwenye simu na sio bank. Mshahara ukitoka nawaachia 10,000 pekee ya kutunzia akaunti ambayo ipo kisheria kwa hiyo bank yenu ya makaburu weusi maana huenda mnapoziona pesa kwenye akaunti mnawashwa na kuzichukua kwa vile mimi ni maskini na sauti yangu haifiki Ikulu. Ila mteja ni malme itoshe tu kusema hivyo.
Ila mwisho wa yote Mungu hapendezwi na huo wizi maana hakuna chenye mwanzo huwa hakikosi mwisho.
Mkuu nakushauri ucheki taarifa zako upya hakuna makato makubwa hivyo ya kuendesha akaunti,binafsi ni mteja waCRDB miaka 15 Sasa.
Taarifa zipi mkuu sidaiwi mkopo wowote na sikusoma kwa mkopo. Na kama ningekuwa nadaiwa ningeona kwenye bank statement?? Nami nimeshangaa huu mwezi japo sinaga kawaida ya kuangalia bank statement ya akaunti yangu, sasa jana nikataka kutoa M kadhaa nichukue kiwanja baada ya kutoa nikaomba risiti walai nilitaka kuzimia maana sio makato yale.Mkuu nakushauri ucheki taarifa zako upya hakuna makato makubwa hivyo ya kuendesha akaunti,binafsi ni mteja waCRDB miaka 15 Sasa.
Nashukuru kwa ushauri wako mkuu. Jana ilikuwa siku mbaya kwangu maana huenda toka siku nyingi naibiwa ila nilikuwa sijui chochote. Mshahara wenyewe wa ngama huu si tutauana jamaniHuwa unadesturi ya litany’s reconciliation kwa account yako mkuu ili kuweza jua mako ni kiasi gani..
Wana huduma ya email mkuu,binafsi napata statement ya akaunti ya kila mwezi kupitia email,jiunge na hiyo utaona kila kituTaarifa zipi mkuu sidaiwi mkopo wowote na sikusoma kwa mkopo. Na kama ningekuwa nadaiwa ningeona kwenye bank statement?? Nami nimeshangaa huu mwezi japo sinaga kawaida ya kuangalia bank statement ya akaunti yangu, sasa jana nikataka kutoa M kadhaa nichukue kiwanja baada ya kutoa nikaomba risiti walai nilitaka kuzimia maana sio makato yale.
Na jumatatu nawaendea ofisini siwezi kuibiwa kiurahisi hivyo yaani. Na kama shida kuziona hela kwenye akaunti bora nihame bank au nihamishe namna ya kuhifadhi fedha zangu kwa kufungua NMB saving akaunti.
Nimecho kwa wizi huo na huenda nilikuwa naibiwa toka siku nyingi ila sikuwa na mazoea kuangalia au kuomba bank statement. Kuanzia sasa fedha zangu kwenye simu nitahamishia au kufungua akaunti bank nyingine.
Mahesabu yote nayaona kwenye e statement mkuu kila mwezi wanatumaHuwa unadesturi ya litany’s reconciliation kwa account yako mkuu ili kuweza jua mako ni kiasi gani..
Buku Saba Saba za lumumba wangekua wanawawekea kwenye account benkUmeniogopesha sana nilipanga nikivuna huu uwele wangu nifungue account crdb bank ya ushirika na maendeleo vijijini..!!