Taarifa zipi mkuu sidaiwi mkopo wowote na sikusoma kwa mkopo. Na kama ningekuwa nadaiwa ningeona kwenye bank statement?? Nami nimeshangaa huu mwezi japo sinaga kawaida ya kuangalia bank statement ya akaunti yangu, sasa jana nikataka kutoa M kadhaa nichukue kiwanja baada ya kutoa nikaomba risiti walai nilitaka kuzimia maana sio makato yale.
Na jumatatu nawaendea ofisini siwezi kuibiwa kiurahisi hivyo yaani. Na kama shida kuziona hela kwenye akaunti bora nihame bank au nihamishe namna ya kuhifadhi fedha zangu kwa kufungua NMB saving akaunti.
Nimecho kwa wizi huo na huenda nilikuwa naibiwa toka siku nyingi ila sikuwa na mazoea kuangalia au kuomba bank statement. Kuanzia sasa fedha zangu kwenye simu nitahamishia au kufungua akaunti bank nyingine.