A
Anonymous
Guest
Kuna malalamiko kuhusu matukio ya upotevu wa fedha kwenye akaunti za baadhi ya wateja wa CRDB katika Manispaa ya Morogoro. Miongoni mwa walioathirika ni baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) pamoja na wateja wengine, ambao wamejikuta fedha zikitolewa kwenye akaunti zao bila wao kufanya miamala hiyo au kutoa idhini yoyote.
Kwa mujibu wa wahusika, wamekuwa wakifuatilia suala hili kupitia uongozi wa benki na matawi husika, ikiwemo tawi la Mandela, lakini hadi sasa bado hawajapata ufumbuzi wa kuridhisha kuhusu fedha zilizopotea na mazingira yaliyosababisha miamala hiyo.
Kutokana na uzito wa suala hili, tunaomba JamiiForums na wadau wengine wenye uwezo wa kufuatilia masuala ya maslahi ya umma kulifuatilia kwa karibu ili ukweli ubainike na hatua stahiki zichukuliwe.
Aidha, uchunguzi wa kina unaweza kusaidia kulinda maslahi ya wateja, kurejesha imani ya wananchi katika huduma za kifedha, na kuisaidia benki kuimarisha mifumo yake ya usalama ili kuzuia matukio kama haya yasijirudie siku zijazo.
Fedha za wananchi ni mali muhimu zinazopaswa kulindwa kwa umakini mkubwa, hivyo ni muhimu malalamiko ya aina hii yashughulikiwe kwa haraka, uwazi na weledi.