Dah mkuu Ngongo hili suala la katibu mkuu wa EAC kutokea Burundi na figisu alizofanyiwa inaonekana ni jambo nyeti sana na halikuvuma kabisa kwenye media.
Kama una nyama vizuri ni bora tuanzishe uzi mzuri kabisa hapa tulijadili kwa mapana yake, maana ile clip iliyorushwa na TBC ikimuonesha Magufuli na Kenyatta wakihojiwa ni kama Kenyatta alikua anajichekesha kinafiki nafiki fulani hivi mpaka mie nikastuka.
Seems kuna ishu kubwa sana inaendelea aiseee
Dah Thanks sana mkuu, umenifungua sana macho.Mkuu asigwa unajua nafasi ya Secretary General EAC ni nyeti sana.Kipindi cha utawala wa Dr Sezibera raia wa Rwanda ambaye alikuwa Dr binafsi na Aide de camp wa General Kagame kabla na baada ya vita vya uvamizi (RPF) ndio tulishuhudia EAC ikiyumba sana kwakuwa alikuwa akitekeleza ajenda za CoW.Zipo taarifa kwamba kuna baadhi ya funds zilikuwa zikitoka EAC kugharamia na kuratibu mikutano ya CoW mfano EAC defence protocal & Northern Corridor Intergration Projects.
Muda wa Dr Richard Sezibera ulipoanza kukaribia kumalizika zikaanzishwa propaganda aendelee kwakuwa chini ya uongozi wake protocals nyingi zilikuwa signed lakini wakasahau audit reports zilikuwa zikimuumbua sana.Burundi ndio walikuwa na zamu ya kumtoa katibu mkuu wa EAC baada ya nchi zote wanachama Kenya,Uganda,Tanzania na Rwanda kuwahi kushika wadhifa huo mkubwa katika jumuiya.Ilikuwa ni dhahiri Rais wa Burundi asingefka katika mkutano kutokana na hali ya kiusalama nchini mwake,tayari makundi ya kimkakati yalishaundwa na waTutsi wa Burundi wakidai eti nchi yao haina haki ya kushika wadhifa huo kutokana na hali ya usalama kwakuwa Tanzania ilishabaini janja ya CoW Dr Magufuli akatumia wadhifa wake wa Mwenyekiti kufanya kikao cha faragha na viongozi wenzake na kujenga hoja matatizo ya Burundi hayawezi kuzuia au kuinyima nafasi ya uongozi ndani ya jumuiya.Rwanda ilikuwa na wasiwasi iwapo wadhifa huo utaangukia kwa raia wa Burundi kutaipataia nafasi kubwa serekali ya Nkurunzinza katika siasa za EAC.
Baada ya CoW kutamba kwa muda mrefu ni dhahiri hali ya mambo imeanza kubadilika sana huku mikakati yao ikizidi kuharibika kabisa.
Dah Thanks sana mkuu, umenifungua sana macho.
Nachoshindwa kuelewa ni kwa nini Museveni ambaye anaonekana mshirika wa karibu sana wa Tanzania anajiingiza kichwa kichwa kwenye ishu ambazo ziko enginered na Kenya kupitia Rwanda au ndio ile slogan kuwa Museveni ni mzee wa kung'ata na kupuliza??.
CoW mtu yeyote mwenye akili alikua anajua kuwa haiwezi kufika popote, kifupi ilikua imeshabuma kabla haijaanza.
Na sasa Sudani Kusini anavutwa kuingizwa ndani ya EAC ili kuwapa nguvu Kenya na Rwanda ila soon naona mchezo utawageukia pia.
Nilicheka sana juzi kati kusikia kuwa Kenya na Ethiopia walikua wamefungiana mipaka "wamenuniana", upande wa Somalia nako mipaka yao ni hatari tupu, palipo na unafuu ni huku kwetu Tanzania sasa nachojiuliza kwa nini hawa jamaa wanatufanyia "unyang'au"??
Mkuu kwanini ni Rwanda tu iwe na ardhi ndogo na sio Burundi na Uganda kwa pamoja? Je wanakabiliana vipi na hali hiyo ya ukosefu wa ardhi, au ndio kuwahamisha raia wao kuja kwetu Tanzania kwa mwamvuli wa wakimbizi?Mkuu asigwa unajua M7 ana ndoto za urais wa EAC kila akipiga hesabu zake Tanzania imekuwa kikwazo kwake haitaki mambo ya haraka haraka hii ndio sababu kuu ya Uganda kupendelea CoW yenye malengo ya kupeleka mambo haraka haraka kabla M7 ajatwaliwa na Mungu hasa tukizingatia umri wake umekwenda kilometa nyingi sana.
Kenyatta na Kenya wanataka kutawala biashara ya bidhaa za viwandani kwakuwa wana viwanda vingi ukilinganisha na nchi nyingine za EA hawajali nani atakuwa kiongozi mradi mambo yao yanakwenda vizuri
Rwanda inataka ardhi na usalama katika jumuiya.Mambo hayo yanakinzwa na katazo la Tanzania kukatalia ardhi yake huku Rwanda ikilemewa na wingi wa watu na uhaba mkubwa wa ardhi.Kitendo cha Tanzania kupeleka majeshi yake Congo DRC kulikata mirija yake ya wizi wa rasilimali za Congo mambo yote haya yalichangia Kagame kuichukia Tanzania na hasa Kikwete.
Mkuu Uganda sidhani kama ina matatizo ya ardhi, kinachoikabili Uganda ni uchumi mbovu na waasi kaskazini mwa nchi.Mkuu kwanini ni Rwanda tu iwe na ardhi ndogo na sio Burundi na Uganda kwa pamoja? Je wanakabiliana vipi na hali hiyo ya ukosefu wa ardhi, au ndio kuwahamisha raia wao kuja kwetu Tanzania kwa mwamvuli wa wakimbizi?
Mkuu kwanini ni Rwanda tu iwe na ardhi ndogo na sio Burundi na Uganda kwa pamoja? Je wanakabiliana vipi na hali hiyo ya ukosefu wa ardhi, au ndio kuwahamisha raia wao kuja kwetu Tanzania kwa mwamvuli wa wakimbizi?
Upi msimamo wa Tanzania kwenye suala la ardhi yake dhidi ya nchi jirani?Mkuu @Konda wa bodabado nchi zote za EA zina uhaba wa ardhi lakini pia zinazidiana kiwango na nyingine ni ugawaji mbovu.
a) Kenya ina ukubwa wa eneo 581,309 sq km na idadi ya watu 46 million
b) Uganda ina ukubwa wa eneo 241,038 sq km na idadi ya watu 36 million
c) Rwanda ina ukubwa wa eneo 26,338 sq km na idadi ya watu 12 million
d) Burundi ina ukubwa wa eneo 27,816 sq km na idadi ya watu 10 million
Tanzania bado ni kubwa kuliko nchi zote kwa pamoja ukubwa wa eneo 945,087 sq km na idadi ya watu 47 million.Ukitazama ukubwa wa eneo na idadi ya watu Rwanda ndio inaongoza huku ikiwa na mgogoro wa chini kwa chini wa kikabila.Watutsi wengi waliorejea baada ya RPF kushika madaraka waliwapora ardhi wahutu hilo pekee ni tatizo kubwa ambalo jawabu lake pengine lingekuwa Tanzania.Upande wa Kenya lipo tatizo la ugawaji wa ardhi mbovu wanasiasa hasa Kenyetta na matajiri wachahche wanamiliki ardhi kubwa huku idadi kubwa ya raia wakiachwa bila ardhi.Tatizo la ardhi lilikuwa moja ya sababu za muungano wa CoW.
Upi msimamo wa Tanzania kwenye suala la ardhi yake dhidi ya nchi jirani?
Mkuu Ngongo una maanisha kwamba utaratibu wa Tanzania kumiliki ardhi ni rahisi au utaratibu wa EAC ndio wenye utaratibu rahisi sana hadi Tanzania kukataa utaratibu wao?Msimamo wa ardhi uko wazi wana EAC ni wageni wakitaka ardhi wafuate utaratibu wa kuimiliki na si kama wazawa (Tanzania) utaratibu wao wa kumiliki ardhi ni rahisi sana.
Mkuu Ngongo una maanisha kwamba utaratibu wa Tanzania kumiliki ardhi ni rahisi au utaratibu wa EAC ndio wenye utaratibu rahisi sana hadi Tanzania kukataa utaratibu wao?
Wanachekesha kweli hao majirani, yaani watu wameshindwa kuishi kwa umoja kwenye nchi zao, tena zenye idadi ndogo ya makabila tofauti na Tanzania ila hawaoni aibu kutaka kujichanganya kuishi Tanzania kama kwao!Utaratibu wa kumiliki ardhi mtanzania uko wazi na umerahisishwa.Wageni wanautaratibu wao tofauti na wazawa kinachogombaniwa Kenya,Uganda,Rwanda wanataka wananchi wao wakija Tanzania wapewe fursa sawa na waTanzania na si wageni.