COVID -19 itatubadilisha sana Waafrika

COVID -19 itatubadilisha sana Waafrika

officialBossmtoto

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2019
Posts
370
Reaction score
1,227
Habari ya humu wanajamvi. Kwanza kama kuna muhanga yeyote wa hili gonjwa ama anamgonjwa ama amepoteza ndugu yake kwa huu ugonjwa naomba niseme pole zangu za dhati.

Pili niseme kuupata sio tiketi ya kufa, ila umakini unahitajika ili kupata nafuu na hatimae kua na afya tele tena.

Dhumuni la uzi huu ni kuchakata namna huu ugonjwa utakavotubadili kama ukipita (wako wanaoamini kwamba huu ndo ule mda unaotajwa kwenye vitabu vya imani kwamba ni nyakati za mwisho)

Swala kubwa ni swala la kuagana katika safari ya mwisho (mazishi). Ukitazama wenzetu wengi wa mataifa ya ulaya, asia na marekani wamekua wakiaga mwili kitofauti na hata mazishi yao hua ya tofauti. Mara chache sana utakuta mkusanyiko wa watu. Kawaida huzungukwa na familia ya karibu na ndugu wachache
IMG_1737.JPG

Licha ya kwamba mazishi yao pia hugharimu sana fedha nyingi hasa ukizingatia mara nyingi eneo la kuzika lazima ulilipie ila ingekua ghali zaidi kama wangefanya kama hapa kwetu

Nirudi nyumbani Africa ambapo kwenye msiba wa mtu utaona watu ambao hata hujui wanahusikaje hapo. Mjukuu wa mwalimu aliemfundisha shule ya msingi na yeye atakuepo msibani, shangazi wa rafiki wa nesi aliemshikia mkoba mke wake wakati anaenda kujifungua naye atakuepo.
Yaani msiba unakua kama mkutano wa kampeni
IMG_1738.JPG

Unakuta marehem alifariki kwa kukosa matibabu ambayo yangegharimu laki nne tuu, ila msiba wake budget inawekwa milioni sita. Ukizingatia aliefariki ndo kichwa cha familia hivo familia ndo inaingia kwenye umaskini hivo ila hilo hawalioni

Kama tutapita Corona naona watu wachache sana kwenye mazishi

Ila kama wote tutakwenda kwa hili tatizo la kushindwa kupumua basi tena tutakutana kwenye hukumu panapo majaaliwa
 
Hiyo picha ya kiafrica imenichekesha aisee mtu mpka atoke kuleee kwenye lundo la watu na ua lake
 
Usiombe aitwe mchungaj wa kilolokole kutoa neno msiban , ni nouma kuanzia saa 5 anatoa neno mpak sa tisa , mpak unawaza npo msiban au kwenye mahubiri ... Misiba kwa Africa ni kero kubwa , people waste lot of time , wazee ndo mda wao wa kucheza karata,, vijana kuchekeshana , wamama kila mmoja aonekane sku hyo ni mstaarabu , mido mana naendaga tyme ya mazishi tuu , mishale ya sa nane ama sa tisa
 
Ni hivi, watu wetu hawana shughuli za kufanya hivyo matukio kama haya yanapata kipaumbele kwenye ratiba zao. Pia, kuwepo na ratiba za vyakula na vinywaji ni incentive kwa sehemu ya jamii zetu masikini kuhudhuria kwa wingi. Aidha, mila zetu zinamtizama mtu asiyehudhuria msiba kama adui bila kuzingatia factors nyingine. Hivyo mwanangu uhudhurie misiba hakuna namna.
 
hata uishi miaka100 lazima utakufa TU..ila tahadhari ni muhimu.

Je uko tayari kufa? Ingekua kifo sio siri? Na ingekua ukijitetea mbele ya israel unaachwa nikuhakikishie watu wengi sana leo hii wangekua hai. Wengi sana

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hiyo picha ya kiafrica imenichekesha aisee mtu mpka atoke kuleee kwenye lundo la watu na ua lake

Unamuuliza baba yule nani
Anakuambia unamkumbuka shangazi yako yule wa Tanga? Sasa huyu ni house girl wa shemeji yake aliemuoa shangazi.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Usiombe aitwe mchungaj wa kilolokole kutoa neno msiban , ni nouma kuanzia saa 5 anatoa neno mpak sa tisa , mpak unawaza npo msiban au kwenye mahubiri ... Misiba kwa Africa ni kero kubwa , people waste lot of time , wazee ndo mda wao wa kucheza karata,, vijana kuchekeshana , wamama kila mmoja aonekane sku hyo ni mstaarabu , mido mana naendaga tyme ya mazishi tuu , mishale ya sa nane ama sa tisa

Na kuna wale wanaokuja special kujionyesha wanamjua mfiwa aunmarehem. Yaani mtu Busy analia kuliko hata ndugu wa karibu. Akitoka hapo anaenda kumuuliza Camera man “Vipi ndugu yangu ulinichukua video wakati nalia? Kama hujanichukua nikae kwa pale ivi nilie unichukue”

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ni hivi, watu wetu hawana shughuli za kufanya hivyo matukio kama haya yanapata kipaumbele kwenye ratiba zao. Pia, kuwepo na ratiba za vyakula na vinywaji ni incentive kwa sehemu ya jamii zetu masikini kuhudhuria kwa wingi. Aidha, mila zetu zinamtizama mtu asiyehudhuria msiba kama adui bila kuzingatia factors nyingine. Hivyo mwanangu uhudhurie misiba hakuna namna.

Vipi swala la kutumia milioni sita kuzika alafu mnaiacha familia maskini kabisa?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Unakuta marehem alifariki kwa kukosa matibabu ambayo yangegharimu laki nne tuu, ila msiba wake budget inawekwa milioni sita. Ukizingatia aliefariki ndo kichwa cha familia hivo familia ndo inaingia kwenye umaskini hivo ila hilo hawalioni
Hata Kama angeipata hiyo laki nne mwisho wa siku angekufa tu. Kufa kunatokana na sababu ya kufa. Na sababu ya kifo inaweza kuwa ugonjwa na sio kushindwa kumudu ghalama za matibabu. Ingekuwa hivyo matajiri wasingekufa.
 
Uuwii, eti nesi aliyemshikia mkoba wakati anajifungua naye atakuwepo, on my way to Machame, mama mdhamini wa ndoa yangu amefariki..🥱🥱
Habari ya humu wanajamvi. Kwanza kama kuna muhanga yeyote wa hili gonjwa ama anamgonjwa ama amepoteza ndugu yake kwa huu ugonjwa naomba niseme pole zangu za dhati.

Pili niseme kuupata sio tiketi ya kufa, ila umakini unahitajika ili kupata nafuu na hatimae kua na afya tele tena.

Dhumuni la uzi huu ni kuchakata namna huu ugonjwa utakavotubadili kama ukipita (wako wanaoamini kwamba huu ndo ule mda unaotajwa kwenye vitabu vya imani kwamba ni nyakati za mwisho)

Swala kubwa ni swala la kuagana katika safari ya mwisho (mazishi). Ukitazama wenzetu wengi wa mataifa ya ulaya, asia na marekani wamekua wakiaga mwili kitofauti na hata mazishi yao hua ya tofauti. Mara chache sana utakuta mkusanyiko wa watu. Kawaida huzungukwa na familia ya karibu na ndugu wachache
View attachment 1435217
Licha ya kwamba mazishi yao pia hugharimu sana fedha nyingi hasa ukizingatia mara nyingi eneo la kuzika lazima ulilipie ila ingekua ghali zaidi kama wangefanya kama hapa kwetu

Nirudi nyumbani Africa ambapo kwenye msiba wa mtu utaona watu ambao hata hujui wanahusikaje hapo. Mjukuu wa mwalimu aliemfundisha shule ya msingi na yeye atakuepo msibani, shangazi wa rafiki wa nesi aliemshikia mkoba mke wake wakati anaenda kujifungua naye atakuepo.
Yaani msiba unakua kama mkutano wa kampeni
View attachment 1435220

Unakuta marehem alifariki kwa kukosa matibabu ambayo yangegharimu laki nne tuu, ila msiba wake budget inawekwa milioni sita. Ukizingatia aliefariki ndo kichwa cha familia hivo familia ndo inaingia kwenye umaskini hivo ila hilo hawalioni

Kama tutapita Corona naona watu wachache sana kwenye mazishi

Ila kama wote tutakwenda kwa hili tatizo la kushindwa kupumua basi tena tutakutana kwenye hukumu panapo majaaliwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sbosti, huku usukumani kwa akina ngosha wanaitisha majina kwenye daftari la nzengo, ole wako kama ni mgeni/kabila lingine uondoke bila kula chakula msibani. Itakuwa gumzo, siku ukifiwa nzengo nzima inagoma kula.

Back
Top Bottom