Course za engineering mbona waombaji wamepungua?.

Wakuu najaribu kujiuliza ni kwa nini course za engineering naona waombaji wachache?.

Has a ukizingatia zile course zilizopo cluster 1,ambazo zinakipaumbele kikubwa cha mkopo mpaka sasa sioni waombaji wakiziomba?.

Mfano Water system and irrigation engineering ipo vyuo viwili tu ambavyo ni Sua na WDMI(chuo cha maji ubungo),na kuna kipaumbele kikubwa cha mkopo saw a na course za afya lakini nikiangalia waombaji online mpaka sasa niwachache kiasi kwamba hata 80 hawafiki.

Ukiangalia pia Petroleum and gas engineering waombaji pia niwachache ingawa inatolewa vyuo vitatu tu,ambavyo ni Udsm,DIT,Udom.

Course zile za cluster 2 ambazo pia zinakipaumbele cha mkopo,zina watu wachache pia.Course kama Mechanical,Civil,Electrical,Mining zina watu wachache pia.

Sasa najiuliza au kwa vile muda wa kuaply bado nimkubwa wataongezeka kadri muda uedavyo.Lakini chakustajabisha siku mbili za mwanzo course kama Water priority namba one chuo cha maji walikuwa watu 67,lakini ukiangalia sasa wapo kama 26,the same na kwa Sua walikuwa zaidi ya watu 71 lakini ukiangalia kwa sasa wapo watu kama 50.

Nikifatilia trend ya mwaka jana muda kama huu course za engineering zilikuwa zina watu wengi wanalio apply tofauti na mwaka huu.

Nimelezea course chache lakini kiujumla engineering hazina watu kabisa ukilinganisha na miaka mitatu iliyopita.Lakini ngoja tuendelee kusubili kadri muda unavyoenda.
Course zipi zimesheheni sana hadi sasa....vp Computer Science, Information technology, information systems, nk kwa baadhi ya vyuo!
 
Mkuu hili linafaida gani au hasara gani kwa taifa?.
Ndo tunakoelekea kuwazika wanasayansi na wataalam mbalimbali rasmi...kwa mfumo huu tegemea kuanzia 2019 kila mtu anasoma arts pekee yake ili atusue pointi 4....unadhani ni wise kiongozi eti sio lazima kila mtu aende chuo kikuu! Nope! Big Nope!
 
Yaa inawezekana vipaumbele vya serikali vimebadilika katika elimu.Sio kupata tena wanasansi wengi Bali wasomi wengi?.
Mimi huwa sielewi pale mnapopima usomi na uwezo wa mtu kwa ufaulu wa darasani ambao unakuwa determined kwa siku moja. Hebu jaribuni kunielewesha labda siku moja nitaelewa. Mitihani ya Kidato cha nne na sita hapa kwetu inapima ni nani aliyekariri maswali mengi na si nani aliyesoma vitabu vingi. Usomi wa kuhangaika na past papers na si vitabu.
 
Duuuu....umemalizia kibingwa eti aliyekariri maswali mengi na si nani aliyesoma vitabu vingi. Usomi wa kuhangaika na past papers na si vitabu! Kweli we mnaa.....daaaa ila big thinker!
 
Nilichosema si majungu, yeyote anayejua vizuri mfumo wetu wa elimu atakubaliana na mimi. Mwanafunzi shuleni hafundishwi kupata maarifa kuhusu anachokisoma ila anaandaliwa ili afaulu mitihani ya kitaifa. Tayari inafahamika NECTA huwa wanachomoa maswali yaliyopita katika mitihani mingine kama yalivyo. Mtu anahangaika na mitihani iliyopita. Hivi idea za vitabu vya review za mitihani unadhani lengo lake ni nini? Hivi unategemea nini kwa mtu anayefanya swali huku akiwa na jibu lake pembeni?
 
Chukua like mkuu!
 
Mimi huwa sielewi pale mnapopima usomi na uwezo wa mtu kwa ufaulu wa darasani ambao unakuwa determined kwa siku moja. Hebu jaribuni kunielewesha labda siku moja nitaelewa. Mitihani ya Kidato cha nne na sita hapa kwetu inapima ni nani aliyekariri maswali mengi na si nani aliyesoma vitabu vingi. Usomi wa kuhangaika na past papers na si vitabu.
Nafikiri hukunielewa vizuri,usomi sio mtihani mmoja wakumpima mwanafunzi ndani ya siku moja.

Pia kusoma vitabu vingi huo pia sio usomi,unaweza kuwa unasoma vitabu vingi lakini mwisho wa siku hakuna kinachobaki kichwani.Kwangu Mimi usomi ni ile hali yakujitambua na kupambana na mazingira katika maeneo yanayokuzunguka.

Usomi pia nihali yakupeleka maandishi yaliyopo katika vitabu katika maisha halisi.Msomi hatambuliwi au kuonekana kwa idadi ya mitihani au vitabu.Msomi anatambuliwa kwa kuonyesha kile alichokipata darasani kukiweka katika maisha halisi yajamii.

Mtihani pia nimuhimu kuwapima wanafunzi,ingawa mtihani hauonyeshi elimu stahiki(kuelimika,usomi) wa mlengwa.Lakini hulka za wanafunzi wengi wakiafrika husoma kwa bidii na juhudi pale wanaposikia mtihani.
 
Hatutaki kuwa na wahandisi uchwara, hivo tunafanya mchujo mkali sana. Asanteni
 
Eti n kwl hawa watainiwa wa kujitegemea {(PC) form six mwaka} huu hawaruhusiwi kuomba course za sayansi na education
 
Hatutaki kuwa na wahandisi uchwara, hivo tunafanya mchujo mkali sana. Asanteni
Wahandisi uchwra tayali mnao kwenye kada ya uhandisi.Miaka miwili imepita imejaza wahandisi wengi wasio na uwezo,jaribuni labda kuwafata vyuoni muwafukuze kitu pia msichokiweza kukifanya.
 
Kijana we apply usiangalie watu sijui wachache hao wanajaaga mpaka kero.
 
Nafikiri hukunielewa vizuri,usomi sio mtihani mmoja wakumpima mwanafunzi ndani ya siku moja.

Pia kusoma vitabu vingi huo pia sio usomi,unaweza kuwa unasoma vitabu vingi lakini mwisho wa siku hakuna kinachobaki kichwani.Kwangu Mimi usomi ni ile hali yakujitambua na kupambana na mazingira katika maeneo yanayokuzunguka.

Usomi pia nihali yakupeleka maandishi yaliyopo katika vitabu katika maisha halisi.Msomi hatambuliwi au kuonekana kwa idadi ya mitihani au vitabu.Msomi anatambuliwa kwa kuonyesha kile alichokipata darasani kukiweka katika maisha halisi yajamii.

Mtihani pia nimuhimu kuwapima wanafunzi,ingawa mtihani hauonyeshi elimu stahiki(kuelimika,usomi) wa mlengwa.Lakini hulka za wanafunzi wengi wakiafrika husoma kwa bidii na juhudi pale wanaposikia mtihani.
Ni kweli ulichoandika. Ila nitatetea hoja yangu ya kuhusu vitabu. Elimu na maarifa yanapatikana katika vitabu, hili la kuyatafsiri maarifa hayo katika uhalisia ni matokeo ya mifumo yetu ya elimu. Haimjengi kupata maarifa bali kusoma kwa ajili ya mitihani. Unakuta shule ina utaratibu wa mitihani kila wiki, unatarajia mwanafunzi atafanya nini zaidi ya kujiandaa kimtihani zaidi. Walimu nao hawana namna nyingine ya kuwaandaa wanafunzi ili wafaulu mitihani yao ya mwisho. Kwa mfano, mtaala wa masomo ya sayansi A-level siyo rafiki kabisa. Inabidi mtu ajikite kwenye mitihani tu.
 
Ndo tunakoelekea kuwazika wanasayansi na wataalam mbalimbali rasmi...kwa mfumo huu tegemea kuanzia 2019 kila mtu anasoma arts pekee yake ili atusue pointi 4....unadhani ni wise kiongozi eti sio lazima kila mtu aende chuo kikuu! Nope! Big Nope!

Ni vizuri tutebganishe ukweli kwamba watu wa arts ni wengi zaidi ya wa sayansi kutokana na upungufu wa miundo mbinu na ufaulu wa wanafunzi-ukipitia shule zilizofanya vizuri mwaka huu utagundua watu wa sayansi ndio wanaotusua kunzia point 3 hadi 6. Wakali wengi wa arts ni kuanzia 7-10. Bahati baya NECTA hawatoi mchanganuo wa kutosha kujua kwa takwimu kinachotokea kutokana na walivyo panga madaraja.

Pili sijui kama TCU wamenyumbulisha vya kutosha kujua athari ya vigezo walivyoweka kwa vyuo. Haitoshi kujua unataka upunguze ufaulu wa kwenda vyuo vikuu ni vizuri ujue pia uamuzi wako utapunguza ufaulu kwa kiasi gani na kama uamuzi huo unaendana na matamkwa ya taifa. Sasa sijui ni wadau wangapi (pamoja na wataalamu) wamehusishwa kwenye maamuzi haya. Vyovyote vile tushishangae yakijitokeza ambayo hayakutarajiwa.
 
Back
Top Bottom