Kwa uelewa wangu nahisi hivi,
Faida1, kwakuwa wameongeza vigezo vya kujiunga vyuo vikuu basi lengo lao itakuwa ni kupata wahitimu wachache na wenye kuimudu vizuri taaluma yao na kuipenda pia, zamani mtu alikuwa anaweza enda kusomea kitu kingine kwakuwa nafasi zimejaa na hatimae anakuwa hana uzalendo na hiyo taaluma, hii ni faida kwa serikali ambayo inadai itakuwa ya viwanda kwakuwa itakuwa inapata watu sahihi
Faida 2, kwakuwa pesa zinazotumika kusomesha wanafunzi vyuo vikuu waga ni nyingi mno na mwisho wake serikali waga haina mpango dhabiti wa kuipata kutoka kwa wadaiwa (mikopo) kwakuwa wengi wao waga hawapati ajira hivo serikali inakuwa km inakula hasara hivo kwa kupunguza wasomi vyuo vikuu serikali kuna hela zitakuwa zinabaki hivo nahisi zitatumika katika ujenzi wa taifa katika nyanja tofauti tofauti, km vile kuongeza fursa za kazi na kuwaajili wale ambao hawakupata kazi ila walitumia mkopo na hatimae kukatwa mkopo waliotumia vyuoni
Hasara, sidhani kama Nchi yetu ina wasomi wa kutosha kukidhi mahitaji ya nchi sasa unapoongeza vigezo kwa nia ya kupunguza wasomi ilhali bado mnawahitaji matokeo yake sijui ile issue ya kutoa wataalamu rwanda itakuwa endelevu
Hasara, kwa nionavyo nahisi wasomi wengi watakuwa na hasira na serikali na hii kupelekea wengi wao kufanya kazi bila morali kwakuwa wafanyakazi wengi wa serikali ukiacha nafasi zao za juu yani ukurugenzi kupanda juu, waliochini ya hapo % kubwa wana elimu ya diploma sasa mtu alikuwa na nia ya kujiendeleza na alisoma kipindi GPA inahitajika 2.7 na leo imepaa hadi 3.5 na wapo wachache ambao wanazo hiyo GPA ila wanakuja kufungwa na issue ya ukienda kusoma hupati salary ss kwa mishahara yetu ya serikali ilivo ni wachache wataweza kwenda kusoma na kuacha mshahara, hapo razima huyu mtu ajenge chuki kwakuwa malengo yake yamekufa hivo ataona km atadharaulika sana, hii itapelekea wasomi pamoja na wafanyakazi kutafuta kazi katika mashirika binafsi au kutoka kabisa nchini na kwenda kutafuta kazi nchi za jirani