Counter: 'Wakazi wa Dar' wapanga kuandamana kumpongeza Rais Magufuli

Kikundi hicho kinachojiita wakazi wa Dar es Salaam kimepanga kufanya maandamano hayo Aprili 12, 2018

Dar es Salaam. Wakati Jeshi la Polisi likiwaonya watu wa kada mbalimbali wanaopanga kufanya maandamano Aprili 26, 2018, kimeibuka kikundi kingine cha watu wanaotaka kuandamana Aprili 12, 2018 kwa ajili ya kupongeza utendaji kazi wa Rais John Magufuli.

Kikundi hicho kilichojitambulisha leo mbele ya waandishi wa habari kama wakazi wa jijini Dar es Salaam, kimeandaa maandamano hayo kumpongeza mkuu huyo wa nchi kwa maelezo kuwa hawana zawadi ya kumpa zaidi ya kufanya maandamano ya kumpongeza.

Mratibu wa maandamano hayo, Charles Masele amesema baadhi ya mambo yaliyowagusa katika utendaji wa rais ni; upatikanaji wa huduma bora za afya, ujenzi wa miundombinu ikiwemo reli na madaraja, ununuzi wa ndege na kukomesha rushwa.

Amesema tayari wameshaandika barua kwa mamlaka mbalimbali kuomba ridhaa ya kufanya maandamano hayo.

"Tunafurahishwa na mengi anayoyafanya kwa Taifa hili hatuna zawadi ya kumpa na tumeona tusisubiri hadi astaafu ndio tumpongeze,”amesema.

"Kwa kuwa maandamano yetu ni ya amani tumeshaandika barua kwa mamlaka husika tunachosubiri kwa sasa ni majibu yao, wakikubali tutafanya wakiona vinginevyo hatutapinga ila tutafanya kongamano."

Kamanda polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hafahamu chochote kuhusu maandamano hayo.

"Tulishasema hakuna maandamano, wasitake kuvunja sheria hiyo barua ofisini kwangu sijaiona na sifahamu chochote, wasianzishe chokochoko," amesema Mambosasa.
Hawajui bomoa bomoa hao...
 
Wewe hiyo imepangwa wajitokeze watu wakumsifia ili wazuiliwe ijulikane kama wamezuia maandamano ya kumsifiwa iweje mengine kama sio mpango waandamane baada ya 26. Akili ndogo
 
samahani wandugu lakini watu wenye meno ya hivyo hiwaga hawana akili sawasawa.
 
yaani wa Tanzania vichwa vya kuku,watu wanalalamika njaa mtaani,hakuna kazi watu wako benchi na matatizo kibao,afu wanatokea watu kama hawa wanaotaka kumpongeza Rais....kwa lipi haswaa???? mpaka aibu kujitambulisha kama ni mtanzania
Wewe fanyakazi acha kulialia unafikiri serikali itakuletea chakula nyumbani kwako!!?? Serikali kazi yake ni kutengeneza huduma za jamii na miundombinu na ndiyo serikali ya awamu ya 5 inakifanya kwa ufanisi mkubwa!!
 
huduma zipi za jamii zinazotengenezwa na awamu hii ya tano,zitaje A,B,C....tuone
 
Tunaomba jeshi la polisi likatae kwa kuwa huu utakuwa ni mtego umeandaliwa na kuratibiwa vizuri ili baadae iwe ni nafasi ya kuhalalisha maovu kwa wale wanaopinga maendeleo yanayoonekana sasa hivi.Mbinu hii wanayotaka kuja nayo ni ya kizamani ya enzi za Nuhu na Yakobo
 
yaani wa Tanzania vichwa vya kuku,watu wanalalamika njaa mtaani,hakuna kazi watu wako benchi na matatizo kibao,afu wanatokea watu kama hawa wanaotaka kumpongeza Rais....kwa lipi haswaa???? mpaka aibu kujitambulisha kama ni mtanzania

Yaani mkuu kuna mabo mengine yanatia hasira sana
 
yaani wa Tanzania vichwa vya kuku,watu wanalalamika njaa mtaani,hakuna kazi watu wako benchi na matatizo kibao,afu wanatokea watu kama hawa wanaotaka kumpongeza Rais....kwa lipi haswaa???? mpaka aibu kujitambulisha kama ni mtanzania
Biashara zinafungwa, watu wanapunguzwa kazi, fao la kujitoa wamelizuia mpaka tutakapokua tumekufa, hakuna unafuu kwenye chakula, na huduma muhimu.

Ukiachilia mbali demokrasia kubinywa, watu kupotea na kukamatwa kwa kesi zenye ukakasi.

Kuna Watanzania wengi sana wanatakiwa kupelekwa Mirembe.
 
Kama watapewa kibali nami pia nitaenda na bango language la kudai,
Katiba mpya
Uhuru wa kujieleza
Uhuru na usawa kwa mikutano ya kisiasa
Nitaandaa na watu wangu wa mabango kama 50 hiv muda wa kutoa hayo mabango hawatoamin macho yao
 
yaani wa Tanzania vichwa vya kuku,watu wanalalamika njaa mtaani,hakuna kazi watu wako benchi na matatizo kibao,afu wanatokea watu kama hawa wanaotaka kumpongeza Rais....kwa lipi haswaa???? mpaka aibu kujitambulisha kama ni mtanzania

Sura zao zilivyochoka umeziona? Hazifanani na pongezi wanazotoa.
 
Kama ni kumpongeza haina haja ya kuandika barua wao waendelee na maandamano yao tu ya amani
 
yaani wa Tanzania vichwa vya kuku,watu wanalalamika njaa mtaani,hakuna kazi watu wako benchi na matatizo kibao,afu wanatokea watu kama hawa wanaotaka kumpongeza Rais....kwa lipi haswaa???? mpaka aibu kujitambulisha kama ni mtanzania
Bora hata vichwa vya kuku deal vichwa vya mbu
 
yaani wa Tanzania vichwa vya kuku,watu wanalalamika njaa mtaani,hakuna kazi watu wako benchi na matatizo kibao,afu wanatokea watu kama hawa wanaotaka kumpongeza Rais....kwa lipi haswaa???? mpaka aibu kujitambulisha kama ni mtanzania

Aisifuye mvua imemnyeshea
Hao sio wenzako, wao wanaifaidi keki ya Taifa wanakula kwa mikono miwili
 
Hizo ni njama B! Wanazuga ili wazuiliwe, hawana lolote hao! Movie za long sana hizo. Zipo outdated kabisa
Zipo outdated kwako. Si mnajidai kutafuta justification ya kuandamana 26 April, hilo ni jibu tosha kwenu. Nchi nyingi duniani, zikiwemo Misri, Uturuki, Ujerumani na Marekani, miaka ya Hivi karibuni zimekuwa zikifanya maandamano ya kuipinga Serikali lakini hapo hapo wamekuwepo nao wanaandamana kuunga mkono Serikali hizo hizo wanazozipinga. Wewe tu ndio mambo haya ni outdated. Ujerumani wamekuwa wakisumbuka na AfD hasa katika Jimbo la Sachsen (Saxony), Marekani nako tangu Trump aingie madarakani, yamefanyika maandamano kibao ya kupingana wao kwa wao likiwemo la Hivi karibuni la Charleston, Carolina.
 
Back
Top Bottom