Ngalikihinja
JF-Expert Member
- Sep 1, 2009
- 31,310
- 31,500
Hawajui bomoa bomoa hao...Kikundi hicho kinachojiita wakazi wa Dar es Salaam kimepanga kufanya maandamano hayo Aprili 12, 2018
Dar es Salaam. Wakati Jeshi la Polisi likiwaonya watu wa kada mbalimbali wanaopanga kufanya maandamano Aprili 26, 2018, kimeibuka kikundi kingine cha watu wanaotaka kuandamana Aprili 12, 2018 kwa ajili ya kupongeza utendaji kazi wa Rais John Magufuli.
Kikundi hicho kilichojitambulisha leo mbele ya waandishi wa habari kama wakazi wa jijini Dar es Salaam, kimeandaa maandamano hayo kumpongeza mkuu huyo wa nchi kwa maelezo kuwa hawana zawadi ya kumpa zaidi ya kufanya maandamano ya kumpongeza.
Mratibu wa maandamano hayo, Charles Masele amesema baadhi ya mambo yaliyowagusa katika utendaji wa rais ni; upatikanaji wa huduma bora za afya, ujenzi wa miundombinu ikiwemo reli na madaraja, ununuzi wa ndege na kukomesha rushwa.
Amesema tayari wameshaandika barua kwa mamlaka mbalimbali kuomba ridhaa ya kufanya maandamano hayo.
"Tunafurahishwa na mengi anayoyafanya kwa Taifa hili hatuna zawadi ya kumpa na tumeona tusisubiri hadi astaafu ndio tumpongeze,”amesema.
"Kwa kuwa maandamano yetu ni ya amani tumeshaandika barua kwa mamlaka husika tunachosubiri kwa sasa ni majibu yao, wakikubali tutafanya wakiona vinginevyo hatutapinga ila tutafanya kongamano."
Kamanda polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hafahamu chochote kuhusu maandamano hayo.
"Tulishasema hakuna maandamano, wasitake kuvunja sheria hiyo barua ofisini kwangu sijaiona na sifahamu chochote, wasianzishe chokochoko," amesema Mambosasa.