CountDown kwa miaka Hamsini ya Uhuru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CountDown kwa miaka Hamsini ya Uhuru

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Chifunanga, Jan 3, 2011.

 1. Chifunanga

  Chifunanga JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 291
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  1- Presidents

  Tanzania imekuwa na marais wanne - Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete
  Marekani kwa kipindi miaka hamsini yao ya kwanza walikuwa na marais nane - Washington, Adams, Jefferson, Madison, Monroe, Adams, Jackson, na Buren

  Je huku kuwa na marais wengi kunaonyesha kuwa marekani imekuwa na demokrasia kubwa kuliko tuliyonayo sisi au?
  Pia ilikuwaje Nyerere akawa rais kwa kipindi kirefu? Katiba ilikuwa inasema nini kuhusu hii, na ilibadilishwa lini?


  2. African Independence and Development

  Ukiacha Ethiopia na Liberia ambazo zimepata uhuru wao kabla ya karne ya 20. Nchi nyingi za Magharibi zimepata uhuru kabla ya Tanzania
  (eg: Libya 1951,
  Sudan 1956, Ghana 1957, ) na katika Afrika Mashariki Tanzania ndio nchi ya kwanza kupata uhuru,
  tukijiringanisha na nchi hizi, maendeleo yetu yamekaaje?


  3. Peace

  Kitu kimoja ambacho ni nakifurahia kuhusu hii nchi yetu ni Amani. Tanzania ni moja ya nchi chache africa ambazo hazijapigana vita (ndani ya nchi)
  kwa sababu za kisiasa au kijamii.


  4. Patriotism
  Hivi watanzania bado ni wazalendo kama tulivyokuwa zamani? Sio mbaya mtu kwenye familia akichemsha lazima tumwambie, lakini je, mbele ya wageni
  na majirani tunaonekana kuwa ni wamoja? Tuna dira moja, na nia moja.

  5. Achievements
  Hivi Tanzania kama nchi inajivunia vitu gani (vya kufanya, sio natural resources), je na wewe kama mtanzania umefanya nini kwenye kuchangia
  achievement za nchi. Kama hujafanya lolote, kwa nini? na kwa nini unadhani wewe huwezi au hauhusiki?...kwa sababu kila mtanzania anauwezo wa
  kufanya kitu extra ordinary....miaka hamsini hii.

  Nilikuwa nataka kulist vitu hamsini ili kukamilisha miaka hamsini, ila muda hauruhusu...wadau nawakilisha.
   
Loading...