Cote d'ivoire wafanya uchaguzi na matokeo tayari


B

Bi. Mkora

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2010
Messages
375
Likes
5
Points
33
B

Bi. Mkora

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2010
375 5 33
Wananchi kwa Cote D'Ivoire walifanya uchaguzi 31 Oktoba 2010 baada ya miaka 10 bila kufanyika uchaguzi. Kulikuwa na wagombea nafasi ya uraisi 14. Na matokeo yametoka jana na kuwa katika hao 14, mmoja amepata 38% na mwingine 32% na waliobakia wamepata chini ya 30%. Hivyo uchaguzi utarudiwa mwisho wa mwezi huu kwa hao wawili waliopata above 30%.
 
M

Mtu Mmoja

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2010
Messages
596
Likes
4
Points
0
M

Mtu Mmoja

JF-Expert Member
Joined Mar 18, 2010
596 4 0
walishapana sana hao kwa hiyo wanheshimiana, subiri kenya watakapofanya, utashangaa utakavyokuwa huru na haki
 
B

Babuyao

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2009
Messages
1,734
Likes
32
Points
145
B

Babuyao

JF-Expert Member
Joined Jun 6, 2009
1,734 32 145
Yaani tanzania tunashindwa demokrasia hata na Ivory Coast? Aibu!!
 
hashycool

hashycool

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2010
Messages
6,465
Likes
1,527
Points
280
hashycool

hashycool

JF-Expert Member
Joined Oct 2, 2010
6,465 1,527 280
Yaani tanzania tunashindwa demokrasia hata na Ivory Coast? Aibu!!
dawa kuchapana tu! hivi watu 41ml tuendeshwe kishenzi na watu 10! mura chapa panga mabazazi wote! idumu tarimeee!
 
Safari_ni_Safari

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2007
Messages
23,231
Likes
7,043
Points
280
Safari_ni_Safari

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2007
23,231 7,043 280
Hata chakula chenye sumu huchukua muda mrefu kuiva
 
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
45,451
Likes
31,735
Points
280
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
45,451 31,735 280
Kura kurudiwa tena


101029083027_ivory_coast_laurent_gbagbo_226x170_ap.jpg
Rais anapambana na muungano wa upinzani


Matokeo ya awali ya uchaguzi nchini Ivory Coast yamebainisha kuwa hakuna mgombea aliyepata zaidi ya asili mia 50 ya kura na hivyo itahitaji duru ya pili ya kutafuta mshindi na safari hii watashindana wagombea wawili.
Hao watakuwa mshindi wa kwanza na wa pili. Rais wa sasa Laurent Gbagbo aliongoza kwa asili mia 38 ya kura akifuatiwa na aliyekuwa Waziri Mkuu Alassane Ouattara aliyepata asili mia 32 ya kura. Rais wa zamani Henri Konan Bedie alimaliza wa tatu akizoa asili mia 25 ya kura.
Ingawa Rais Gbagbo alishinda duru hiyo, lakini ameshindwa kutimiza kiasi cha kura zinazohitajika huku akikabiliwa na upinzani mkali kutoka ushirika wa vyama vya wagombea katika duru ijayo, inayokisiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Novemba.
Matokeo haya yamewasilishwa kwa Mahakama ya kikatiba kuidhinishwa wakati Umoja wa Mataifa unahitaji kuthibitisha matokeo. Matokeo haya ni ishara ambayo huenda mkongwe wa siasa Henri Konan Bedie amefikia kikomo cha uwezo wake kisiasa.
101028154015_henri_konan_bedie_226x170_afp.jpg
Mkongwe afika kikomoRais huyo wa zamani ametangaza kuwa atapinga matokeo hayo, ambayo msemaji wake ameyataja kama yaliyodhihirisha 'njama ya kuiba matokeo'
Hata hivyo wasimamizi wa Kimataifa wameutaja mchakato mzima kama uliofanyika kwa uwazi na usawa, licha ya kuwepo mapungufu ya mipango.
Na baada ya siku nyingi za wasiwasi na hali ya sintofahamu, Biashara nyingi huenda zikafunguwa milango kuanza shughuli zake mjini Abidjan ingawa duru hii ya pili itakuwa kali.
Ouattara anashirikiana na muungano wa upinzani ulio na mgombea mwenza Bedie na vyama vingine vidogovidogo vilivyomuezesha kushinda asili mia 60 katika duru ya kwanza.
Hata hivyo kuna hofu kama kura zote za Bedie kutoka sehemu ya kati mashariki itaelekea katika kambi ya Bw.Ouattara ambayo inamiliki eneo la kaskazini lenye idadi kubwa ya Waislamu.
Majuma kadhaa yajayo kabla ya duru hiyo ya pili inatazamiwa kuwa majibizano makali na madongo yatarushwa wakati Rais aliyekua madarakani akijitahidi kuzoa kila wapiga kura kutoka kwa muungano wa upinzani.

BBC Swahili - Mwanzo
 

Forum statistics

Threads 1,239,097
Members 476,369
Posts 29,342,182