Mabibi na mabwana heshima kwenu.
Siku baada siku tumekuwa watu wa kupokea taarifa za tanzia za watu wazito wazito. Jana huyu, yule nk na leo hivyo hivyo.
Si kuwa wale kina wenzangu na miye hawamo kwenye hiki kitim timi. Ama kwa hakika hao ndiyo wanaokufa kwa wingi zaidi kuliko hata hao vigogo ambao taarifa zao tunazipata.
Tuiache hali hii kuendelea hivi hadi lini? Au iwe hivi hivi hadi nasi kwa wakati wetu, mmoja mmoja kwa wakati wake atakaposhindwa kupumua jumla jumla?
Kama taifa siyo siri kuwa tuko vibaya. Kama nchi tumegawanyika. Pana mambo ya wazi ambayo kimsingi hatukubaliani. Hali si hali kiasi wengine tunaona tunaburuzwa.
Maisha ni kuridhiana, kushawishiana, kuelewana nk. Si kuburuzana.
Akipenda kusema hayati Baba wa taifa (rip), "tushawishiane kwa hoja."
Ni wazi kuwa hii si hali ya afya sana. Zanzibar wameyaona hayo, wameanza na wanakwenda vizuri.
Huku kwetu pia yanahitajika maridhiano katika mambo kadhaa likiwamo hili la ugonjwa huu ambalo hilo ni la dharura mno kuliko yote. Hii ni kwa sababu watu wanakufa na haipo hakika baina yetu hapa tulipo anayefuata anaweza kuwa nani.
Hivi tumekwama wapi kama taifa hata kulifanyia siasa janga hili ambalo kila leo linatuondolea wapendwa wetu kwa kasi tuionayo?
Hatuna muda zaidi wa kuendelea kuufumbia macho ugonjwa huu. Wanaume na wanawake wa Dar tayari wameanza kuchukua hatua zao binafsi kwa kutambua kuwa hatuko vizuri wala hatuko katika njia iliyo sahihi:
www.jamiiforums.com
Hongereni wana dar es salaama. Mmeonyesha njia na ni wazi upepo huu hautaishia Mbezi mwisho.
Ni muhimu kwa serikali kuona hatua binafsi hizi za wana Dar es salaama, na kutambua kuwa kama raia:
"Hatuwezi kuendelea kuwasubiri ninyi indefinitely mnapoendelea na siasa zenu hizi kuhusiana na ugonjwa huu zisizo tusaidia. Tambueni kuwa mnacheza na relevance yenu nyie wenyewe.
Kwa hakika si muda mrefu sana umebakia, msipofumbua macho yenu sasa, mtapwelewa. Kwenye hili hamna wa kumlaumu bali mchawi wenu ni nyie wenyewe.
Ni kipi hicho ambacho hamkuambiwa directly au indirectly ili kuwaonyesha kutokuridhishwa kwetu na hatua zenu kuhusiana na ugonjwa huu?"
Ama kweli sikio la kufa halisikii dawa!
Ni wazi kuwa, kukubaliana kuwa na njia muafaka za kukabilia na janga hili ni kwa maslahi yetu sote. Hiyo ndiyo demokrasia yenyewe ambayo sisi kama wananchi tunaihitaji.
Kwa hakika tusipoiona kupewa, tutaidai. Kwa hili na tupeane yaliyo makavu kweli kweli.
Mtu mmoja, au kikundi chochote cha watu hapa nchini hakiwezi kujimilikisha hata haki zetu za kuishi au kufa.
"Tambueni kuwa tunatambua sisi ni wahanga wa ugonjwa huu zaidi kuliko milivyo ninyi."
www.jamiiforums.com
Ninawasilisha.

Corona: Dar es Salaam Wananchi wafanya kweli. Hongereni sana
Mabibi na Mabwana hapa ni Dar katika mapambano dhidi ya Corona. Kwa hakika hawa wameonyesha njia kwani hizi ni jitihada binafsi baada ya kutambua ugonjwa huu upo na biashara ni asubuhi. Kama vifaranga vya kuku vile kwa hakika hawa wana chakura kivyao kivyao: Wa mikoa mingine zingatieni...
Hongereni wana dar es salaama. Mmeonyesha njia na ni wazi upepo huu hautaishia Mbezi mwisho.
Ni muhimu kwa serikali kuona hatua binafsi hizi za wana Dar es salaama, na kutambua kuwa kama raia:
"Hatuwezi kuendelea kuwasubiri ninyi indefinitely mnapoendelea na siasa zenu hizi kuhusiana na ugonjwa huu zisizo tusaidia. Tambueni kuwa mnacheza na relevance yenu nyie wenyewe.
Kwa hakika si muda mrefu sana umebakia, msipofumbua macho yenu sasa, mtapwelewa. Kwenye hili hamna wa kumlaumu bali mchawi wenu ni nyie wenyewe.
Ni kipi hicho ambacho hamkuambiwa directly au indirectly ili kuwaonyesha kutokuridhishwa kwetu na hatua zenu kuhusiana na ugonjwa huu?"
Ama kweli sikio la kufa halisikii dawa!
Ni wazi kuwa, kukubaliana kuwa na njia muafaka za kukabilia na janga hili ni kwa maslahi yetu sote. Hiyo ndiyo demokrasia yenyewe ambayo sisi kama wananchi tunaihitaji.
Kwa hakika tusipoiona kupewa, tutaidai. Kwa hili na tupeane yaliyo makavu kweli kweli.
Mtu mmoja, au kikundi chochote cha watu hapa nchini hakiwezi kujimilikisha hata haki zetu za kuishi au kufa.
"Tambueni kuwa tunatambua sisi ni wahanga wa ugonjwa huu zaidi kuliko milivyo ninyi."
Corona: Tusidanganyane hatuko sawa sote mbele ya ugonjwa huu
Mabibi na mabwana na tuambizane ukweli tu, kwani haisaidii kuukimbia ukweli. Pia msema ukweli ni mpenzi wa Mungu. Hongera Dar kwa kuanza kutupia barakoa kujaribu kujihami na kuwahami wengine japo kwa jitihada binafsi. Inatia moyo kwani mmedhihirisha "kifaranga hafunzwi kuchakura!" Ninaamini...
Ninawasilisha.