Corona sio siasa ya kuimaliza kwa propaganda

kakamtumishi

Senior Member
Jun 18, 2016
192
235
Maswali na hoja muhimu katika hotuba ya Rais.

Rais amesema kwamba mara zote amekuwa na wasiwasi kwamba kila wakipima majibu ni postive, postive, postive, postive...

Si jambo baya lakini wakati mwingine mtu hupata majibu kutokana na precedence aliyotengeneza mwenyewe kwa kuwa hicho ndicho alichotaka.

Maana inashangaza kwamba rais haamini majibu ya postive ila anaamini majibu ya negative kwa kipimo kilekile.

Katika utafiti mdogo uliofanywa katika maabara kwa kupeleka sampuli zisizo za binadamu kupimwa corona majibu yalikuwa kama ifuatavyo kwa kadri ya hotuba ya rais.

Sampuli: OIL
Majibu: Hakuna corona(Negative)

Sampuli: Fenesi
Majibu: Hakuna hitimisho(unconclusive)

Sampuli: Papai
Majibu: Kuna corona(Postive)

Sampuli: Kware
Majibu: Kuna corona(Postive)

Sampuli: Sungura
Majibu: Haikutambuliwa(undetermined)

Sampuli: Kondoo
Majibu: Hakuna corona(negative)

Sampuli: Mbuzi
Majibu: Kuna corona(postive)

Sampuli hizi za wanyama na matunda zilibatizwa majina bandia ya watu, zikapewa jinsia na umri bandia ili kuwaficha wapimaji.

Majibu yaliyotoka yakazidisha zaidi maswali.

Kama:-

Je, watalaamu wetu wamenunuliwa na mabeberu?

Je, watalaamu wetu hawana uwezo ama uelewa? Kitu ambacho Rais amekikataa kuwa hilo haliwezekani.

Je, vifaa vya kupimia ni vibovu?

Labda vifaa vya kupimia tulivyoletewa ikiwemo reagents, swabs na kits vimetengenezwa kwamba kila baada ya idadi fulani lazima vitoe jibu la postive.

Mimi nitajikita katika kuonesha mapungufu makubwa ya huo utafiti wa kiuchunguzi. Ambapo kama mapungufu hayo yasingefanyika basi tungekuwa na picha halisi na kuepuka kulifanyia propaganda hili swala kitu ambacho hakitatusaidia katika mapambano.

1. Utafiti haujaonesha test consistence katika madai aliyotoa Rais.

Huu ni upungufu mkubwa ambao unaacha maswali mengi.

Mfano baada ya kupima sampuli za papai likaonekana lina corona ilitakiwa sampuli zaidi za papai zipimwe hata mapapai 10 ili kama mapapai yote kumi yataonekana postive.

Pia approach nyingine ni kuchukua sampuli 10 katika papai hilohilo moja na kama pia itaonesha majibu yote ni postive.

basi tunapata uhakika kuwa ukipima mapapai kwa kipimo hikihiki majibu yanakuwa postive.

Hapa tungetaka kuchunguza zaidi kujua ni kipi katika papai kinachofanya papai lionekane na corona?

2. Utafiti hauja-expose inconsistence ya vipimo kwa sampuli ileile.

Haya pia ni mapungufu makubwa katika utafiti uliofanyika

Mfano: Baada ya kupima Kondoo na kupata negative walitakiwa tena wapime hata kondoo 10 ili kuona kama majibu yanabadilika badilika.

Another approach ni kuchukua tena sampuli 10 katika kondoo mmoja na kama majibu yakaonekana kutofanana, basi tungehitimisha kuwa vipimo havina consistence na hivyo majibu yake yangekosa kuaminika.

3. Utafiti haukufanywa kwa mtu asiye na corona.

Haya pia ni mapungufu makubwa kwa wachunguzi kushindwa kutumia sampuli za wasio na corona ili kujiridhisha juu ya usahihi wa majibu.

Mfano. Wangechukua sampuli za mtu mmoja hata sampuli 10 zikapimwa kama watu tofauti ili tuone majibu ya vipimo vyote hivyo 10 yanafanana ama hayafanani.

Kama hayatafanani basi tunahitimisha kuwa vipimo havina consistence na hivyo vinatoa majibu ya uongo pia. Bila kujali kama ni negative ama postive.

4. Consistence na inconsistence katika sampuli za mwenye corona haikuonesha katika utafiti.

Haya pia ni mapungufu makubwa kwa kuwa uchunguzi ulipaswa pia kuangalia watu wenye virusi kama majibu yao hayabadiliki badiliki kwa kuchukua sampuli 10 katika muda uleule.

Ili tupate uhalali wa kisayansi katika majibu na hoja zetu.

5. Utafiti ulizingatia tu wasiwasi wa false postive tests lakini haujazingatia wasiwasi wa false negative tests.

Kama huamini majibu ya wanaoambiwa wana corona kwa nini uamini majibu ya wanaoambiwa hawana corona wakati kipimo ni kilekile kisichoaminika?Hii ni predence setting.

Ndio maana mwanzo nilisema kwamba wakati mwingine unapata majibu kulingana na precedence uliyoset mwenyewe na lazima upate majibu kulingana na matakwa yako.

Kwa nini pia hakukuwa na wasiwasi kwamba kwa kuwa vipimo ni feki basi hata wanaoambiwa hanawa corona huenda wakawa na corona?

Na kufanya majibu yote ya vipimo iwe postive ama negative yasiaminike kabisa.

Mapungufu haya yanaweza kusababisha swala hili kufanyiwa propaganda za kisiasa zaidi kuliko kutafuta ukweli wa kuidhibiti corona.

Kwa nini nasema hivi.

1. Si mara ya kwanza vipimo feki kusambazwa.

Mwezi wa pili kituo cha kudhibiti magonjwa ya mlipuko Marekani kiitwacho CDC kilitengeneza na kusambaza mamilioni ya vipimo vya corona Marekani lakini baadae vikathibitika vipimo vyote ni feki na vyote viliondolewa na Marekani ikalazimika kuagiza vifaa vya kupimia toka China.

Lakini pia Nchi nyingi zilinunua vifaa feki baada ya kuuziwa na wahuni kutoka katika makampuni yasiyoidhinishwa na serikali ya China.

Mfano wa nchi hizo ni Uingereza, Spain, Jamhuri ya Cheki, nk nk nk.

Huenda na sisi tumepigwa katika ununuzi wa vifaa kama tuliagiza kwa makampuni yasiyoidhinishwa.

2. Si mara ya kwanza watalaamu kutojua kuvitumia vipimo vya corona.

Mfano nchi ya Slovakia ilinunua vifaa vya kupimia toka China katika makampuni yaliyoidhinishwa kutengeneza test kits.

Baadae ikaonekana vifaa hivyo vyote ni feki kwa kuwa vilikuwa vinatoa majibu ya uongo.

China ilituma watalaamu ikabainika kwamba vifaa vyote vilikuwa orijino lakini watalaamu wa Slovakia walikuwa wanavitumia kimakosa. Slovakia ililazimika kuomba radhi.

3. Tafiti zote hazijaondoa uwezekano wa wanyama kuambukizwa corona.

Kwa asili virus vina uwezo wa kuambukiza binadamu, bacteria, wanyama na mimea.

Swala la mbuzi kuonekana ana corona ama papai kuonekana lina corona huenda kukawa na sababu za kisayansi kwa kuwa vipimo havipimi kirusi chenyewe bali enzymes zinazotolewa na kirusi.

Lakini vilevile inawezekana kwamba hao wanyama na mimea wakawa na corona pia japo wasipate madhara kama sisi.

Huenda enzymes hizo zikawepo katika mimea mingine na wanyama kwa kuwa virusi huwa vinauwezo wa kuambukiza wanyama na mimiea pia.

Ndio maana Sokwe anaambukizwa corona na ametumika katika majaribio ya chanjo huko Uingereza na kuonesha ufanisi wa chanjo kuzuia maambukizi ya corona.

Pia Marekani Simba alikutwa ameambukizwa corona na akatibiwa mwezi wa tatu kama nakumbuka vizuri.

Kwa hiyo swala la mbuzi kukutwa na corona hii ya covid-19 si geni kwa wanyama maana tayari imetokea huko Marekani.

Mwisho hili swala si la kisiasa bali ni swala la kisayansi na linahitaji majibu ya kisayansi yanayozingatia procedures sahihi za kisayansi na si kuset precedence flani for political propaganda wakati ambapo mambo mengi kuhusu kirusi hiki cha SARS-Cov2 yakiwa hayafahamiki na tafiti zinaendelyea kutafiti mambo mengi yasiyofahamika mpaka sasa.
 
Mh Rais amelenga uchumi tu, hana jambo lingine wave watu au wapone yeye anataka watu wafanye kazi ili serikali ipate fedha, hataki watu wawe na hofu watashindwa kufanya kazi na hatimaye serikali itakosa mapato. hayo mengine ni mbwembwe tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KIkubwa cha kwanza ni kuwa rais anawaza pesa tu, cha pili inawezekana ni ule utaratibu wa kawaida wa kutoa sadaka kipindi cha uchaguzi, cha tatu anajua watu wakijifungia watamkumbusha kuhusu zile fedha za akiba alizosema tunazo za kutuwezesha kuishi hata miezi 6 bila kukusanya kodi.
 
Jiwe linajifanya mkemia mkuu sasa hivi, mtu ambaye hua kila kitu anasingizia mabeberu, swali langu ni moja, hao mabeberu ni akina nani hasa? Naomba mtaje kua beberu ni nchi A au B sio kila kitu mabeberu tu wakati Tanzania yenyewe ni nchi ha kibeberu.

Tunaye kiongozi anayeamini conspiracy theories finally, waliopita angalau walikua wanasikiliza wataalamu wanasemaje, huyu sayansi weka pembeni anafata sayansi anayoiamini yeye mwenyewe aliyosoma miaka hiyo ya nyuma kwa kuungaunga alafu anaamini na mauzauza ya uchawi na vitu vya kijinga. Dunia nzima yeye tu ndoyo alikaa akasema tuombe, angekua Kenya huyu kwa ushenzi huu wangekua tayari washamtoa urais, kwa kua ni Tz watu watamuunga mkono sishangai vilaza Tanzania ni zaidi ya 80% kwa stats za haraka haraka.

Kuna sababu nyingi kwa nini sample inaweza kuja positive, jiwe hataki kuzisikia anataka anachoamini yeye kua mabeberu wamepanga ndicho kiwe ukweli na wengine wote tuamini. Haha nyoooko, kama hatuamini machine zao si tutengeneze za kwetu wenyewe? Characteristics za corona hatuzijui? Genome hatuijui? Kila kitu kipo online. Jiwe ni kalio tu hatujawahi kua na mtu ovyo kichwani ka jamaa, haamini ugonjwa upo atoke ajichanganye na watu kama zamani aone korona itakavyomfyeka
 
Back
Top Bottom