Corona: Orodha ya wahanga, sampuli

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,840
35,848
Katika ule mukthadha wa kukubali kutokubaliana, ikumbukwe kuwa iliombwa watu kuweka orodha ya wahanga wote wa hizi changamoto za kupumua, kila inapowezekana.

Kuondoa tashwishi hapa ninaweka tarehe tulizopoteza wanasheria nguli hadi kufikia 09.07.2020 idadi yao mbele katika mabano (kama sampuli). Hawa na tarehe zao ni kutoka katika orodha halisi:

1. 01.04. (1)
2. 02.04. (1)
3. 06.04. (1)
4. 27.04. (1)
5. 28.04. (3)
6. 30.04. (1)
7. 03.05. (2)
8. 04.05. (2)
9. 05.05. (1)
10. 16.05. (1)
11. 20.05. (1)
12. 30.05. (1)
13. 06.06. (2)
14. 09.07. (1)

Hii na ionekane kama wito wa kuamshwa.

Orodha hizi zinaendelea kuhuishwa kwa wahanga wote. Orodha kamili zikizingatia taarifa zote kwa kila mhanga.

Kwa hakika siku moja, jina moja moja litasomwa mbele zetu sote kila mmoja kwa mchango wake.
 
Duh! Wejamaa kweli ni vacuous popinjay

Niambie unafaidika na nini tukiwa na wagonjwa wengi na vifo vingi?

Wanaotutoka ni jamaa zetu, ni ndugu zetu, ni colleagues wetu nk.

Kwa hakika hawatapotea bure.

Kama wewe haikuhusu usidhani ni hivyo kwa wote.
 
Duh! Wejamaa kweli ni vacuous popinjay

Niambie unafaidika na nini tukiwa na wagonjwa wengi na vifo vingi?
Kwani tukiamua kujitoa ufahamu kuwa hakuna ugonjwa wa corona Tanzania huku watu wakiwa wanakufa Kila siku ndo unapata faida gani?Siku huyu aliyeondoa ubongo wenu kwenye vichwa vyenu akifyekwa na corona labda akili zitawarudia
 
Nani alisema hakuna corona?

Corona ipo na tunaishi nayo. Maisha yanaenda. Hao wanaopukutika wako wapi?

Acha kuleta chuki binafsi za kisiasa kwenye mambo mazito
 
Watu ambao wanaishi nje ya Tz wanatupa tabu sana na hili suala la corona,yani mtu yupo huko nje anabishana na sie tuliyopo nchini.

Hivi kweli watu tuzike ndugu zetu kwa vifo vya corona halafu bado sie tuishi kama hakuna corona hali ya kuwa ndugu zetu wamekufa na corona na tunajua! Hili mbona haliingii akilini. Ni mtu asiyekuwe Tz tu ndio ataamini hili et tunaficha ,sasa tunamficha nani? Hao viongozi wa serikali wenyewe tumeona hawavai barakoa na wanasalimiana kwa kushikana mikono kabisa,hivi kweli utasema hao watu wanaficha corona kwa kutupumbaza sie wananchi?
 
Nani alisema hakuna corona?

Corona ipo na tunaishi nayo. Maisha yanaenda. Hao wanaopukutika wako wapi?

Acha kuleta chuki binafsi za kisiasa kwenye mambo mazito
Kwani wake waliolala makaburi ya Kinondoni,ununio na kwingineko wanatoka wapi?
 
Malaraia yanaua zaidi ya Corona lkn bado usiku watu wanapiga kazi kama kawaida.So at the ends of the day lazima maisha ya endelee kama kawaida.Manake unavyo ongea utafikiri miaka mingine wanasheria walikuwa hawafi au labda mwaka huu magonjwa mengine yame acha kuua.

Wewe kama unaona Corona itakuua kaa ndani na familia yako hujakatazwa kwani UNA UHAKIKA NA KIPATO CHAKO,ila wenzako wasiokuwa na uhakika na maisha yao,wanao ungaunga waache waka zitafutie ugali familia zao.

Wee endelea kupiga ramli lkn mwisho wa siku MAISHA LAZIMA YA ENDELEE.
 
Ni lipumbavu tu! Majitu mengine sijui yakoje? Hili jamaa si ndilo lilikomalia kwamba kwenye shule zilizofunguliwa kuna vifo vingi vya Corona?

IMG_20200718_200657_098.jpg

Katika wawili hao kuna mmoja mpumbavu zaidi kuliko mwingine.

Ama kweli nyani kuona *undule ni habari kubwa.
 
Watu ambao wanaishi nje ya Tz wanatupa tabu sana na hili suala la corona,yani mtu yupo huko nje anabishana na sie tuliyopo nchini.

Hivi kweli watu tuzike ndugu zetu kwa vifo vya corona halafu bado sie tuishi kama hakuna corona hali ya kuwa ndugu zetu wamekufa na corona na tunajua! Hili mbona haliingii akilini. Ni mtu asiyekuwe Tz tu ndio ataamini hili et tunaficha ,sasa tunamficha nani? Hao viongozi wa serikali wenyewe tumeona hawavai barakoa na wanasalimiana kwa kushikana mikono kabisa,hivi kweli utasema hao watu wanaficha corona kwa kutupumbaza sie wananchi?

Endeleeni kuuchonga ila fahamuni kuwa orodha itaendelea kuhuishwa hata kama wengine sisi tutakuwa wahanga wa ugonjwa huu kabla ya kuwajibishana. Inafahamika ni kwa maslahi gani wengine kuwa vifo vya watu wasiowahusu, nyie haiwahusu:

Kutoka kwa wahanga watarajiwa wa Covid-19

Habari ndiyo hiyo.
 
Kwani tukiamua kujitoa ufahamu kuwa hakuna ugonjwa wa corona Tanzania huku watu wakiwa wanakufa Kila siku ndo unapata faida gani?Siku huyu aliyeondoa ubongo wenu kwenye vichwa vyenu akifyekwa na corona labda akili zitawarudia
Tatizo sio Magufuli,kama Corona ingekuwa inapukutisha watu basi Magufuli asingekuwa na jeuri ya kusema corona imepunguwa na kuruhusu shughuli kuendelea kama kawaida maana uhalisia ungepingana nae watu wangejiona wanavyopukutika na wengi kuumwa.
 
Mkuu kwa sasa hao wanakufa hatuwaoni,Ila siku akifa yeye ndo tutaanza kuwaona,acha twende kwenye kampeni Kama tutakuwa tumefika huko lakini
 
Endeleeni kuuchonga ila fahamuni kuwa orodha itaendelea kuhuishwa hata kama wengine sisi tutakuwa wahanga wa ugonjwa huu kabla ya kuwajibishana. Inafahamika ni kwa maslahi gani wengine kuwa vifo vya watu wasiowahusu nyie haiwahusu:

Kutoka kwa wahanga watarajiwa wa Covid-19

Habari ndiyo hiyo.
Mkuu sijui unalizungumzia kundi gani maana tumeona makundi yote hayana tahadhari na hiyo corona kuanzia wananchi hadi hao viongozi wakubwa wa nchi,sasa sijui nani anamficha mwenzie kuhusu corona? Ajabu hata Zitto na Membe ambao walikuwa wakipigia kelele hili suala nao tunaona wanafanya yaleyale.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom