Corona ni uzembe wetu isingetufikia, na itatumaliza tusipoamka sasa - ukweli mchungu

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,854
35,861
Corona umeanzia China sote tukiusikia na kufahamu unaambukizwa vipi na namna gani unaweza kutufikia. Tulijua namna gani tunaweza kufanya usitufikie.

Nchi kama Uganda hadi sasa wako salama na wamejizatiti haswa usiwafikie. Hiyo si ajali bali ni utashi.

Japo tulijua: Sisi na viongozi wetu hatukufanya lililostahili na leo tuko hapa tukiwa na wagonjwa waliothibitiswa sita na mamia wa kufuatiliwa.

Dunia nzima ulikoingia kasoro ya China, wagonjwa wanaendelea kuongezeka, (Vifo vinaongezeka), hali kadhalika wa kufuatiliwa nao wanaendelea kuongezeka.

Yaani kwa ufupi kunazidi kuwa rojo juu rojo.

China kaushinda vipi? Huu nao ni ukweli mwingine ambao sisi bado hatutaki kuuona wala kuuzingatia.

China kaushinda ugonjwa huu ndani ya miezi 3. Waliopania kuushinda wanajiwekea lengo hilo hilo la miezi 3 kwa utaratibu ule ule wa China.

Marekani, Uingereza, Ujerumani na wote waliodhamiria kwa dhati wako kwenye njia hizo hizo za Mchina:

Jimbo la California latangaza amri ya kukaa ndani kudhibiti

Boris Johnson: UK can ‘turn the tide’ on coronavirus by June

French President Macron says 'we are at war' as he orders lockdown | DW | 16.03.2020

Bila kuamuru watu wote kusalia majumbani, ugonjwa huu utakuwa bado upo upo sana nasi na utatutesa kweli kweli.

Serikali tutendeeni haki kwa kuwataka watu wote wasalie majumbani japo kwa siku 14 kwa kuanzia sote tuupime upepo unaenda wapi.

Huu ndiyo ukweli mchungu, tusipousema wazi wazi kama hivi tunakuwa hatujitendei haki sisi wenyewe.
 
Hebu tuache upuuzi was kujifananisha na mataifa yaliyoendelea.Kwa nchi zetu za Afrika ukisema watu wakae majumbani hata kwa siku tano wengi watakufa njaa.
Kuna maelfu ya familia hapa nchini hawana hats akiba ya 10000 ndani wanategemea day work ndipo wapate chakula.
Ukisema wasifanye kazi utawalisha?
Kila siku wastani wa watu elfu nane wanakufa kwa njaa duniani na hakuna hatua inayochukuliwa,Leo korona iliyoua watu 10000s kwa miezi minne mnajifanya kujali uhai wa mwanadamu?
 
Kuna mchungaji amewaambia waumini wake sadaka ipo palepalee,, na akatoa namba ya M-PESA kusiwe kunakisingizio..

Sent using Jamii Forums mobile app

Jitihada lazima zifanyike kuwaweka watu nyumbani. Kenya wameacha kutoza commission kwenye miamala ya mpesa kuwajengea watu uwezo wa kujikimu.

Malipo ya kodi yamesogezwa mbele.

Rwanda kuna babu kama wa Loliondo alikuwa na tiba ya Corona yuko mbaroni.

Watafuta sadaka uchwara hao wanapaswa kupewa makavu.
 
Hebu tuache upuuzi was kujifananisha na mataifa yaliyoendelea.Kwa nchi zetu za Afrika ukisema watu wakae majumbani hata kwa siku tano wengi watakufa njaa.
Kuna maelfu ya familia hapa nchini hawana hats akiba ya 10000 ndani wanategemea day work ndipo wapate chakula.
Ukisema wasifanye kazi utawalisha?
Kila siku wastani wa watu elfu nane wanakufa kwa njaa duniani na hakuna hatua inayochukuliwa,Leo korona iliyoua watu 10000s kwa miezi minne mnajifanya kujali uhai wa mwanadamu?

Hawa ndiyo wale watanzania wenye uelewa finyu katika ubora wenu.

Kenya wamechukua jitihada kumwezesha mkenya wa kawaida kujimudu kukaa nyumbani. Tozo za kwenye miamala ya mpesa imefutwa. Kodi mbalimbali zikiwamo za pango zimeahirishwa kwa at least 3 months nk.

Mh. Zitto kaandika bandiko Zuri tu lenye kuhusiana na survival katika kipindi hiki.

Bila watu kusalia nyumbani kila mgonjwa mmoja hesabu watu wa kufuatilia kama 1,000. Watakapofika wagonjwa 40,000 basi tena, tutakuwa sote tuko njia moja.

Ukipenda ufahamu tofauti na ebola, mgonjwa wa ugonjwa huu, huyo huyo anaweza ugua hata mara 1,000.
 
Mnavyoyapa kiki hayo mafua inaboa sana. Takwimu huna unaleta uharo tu

Hawa ndiyo wale watanzania wenye uelewa finyu katika ubora wenu.

Kenya wamechukua jitihada kumwezesha mkenya wa kawaida kujimudu kukaa nyumbani. Tozo za kwenye miamala ya mpesa imefutwa. Kodi mbalimbali zikiwamo za pango zimeahirishwa kwa at least 3 months nk.

Mh. Zitto kaandika bandiko Zuri tu lenye kuhusiana na survival katika kipindi hiki.

Unatoka ulikotoka unahara halafu unadhani wanaohara ni wengine. Elimu ni uhuru. Kama elimu yako ndogo usidhani kila mtu ni hivyo. Tunaandika tukawa na data na research zakutosha.

Bila watu kusalia nyumbani kila mgonjwa mmoja hesabu watu wa kufuatilia kama 1,000. Watakapofika wagonjwa 40,000 basi tena, tutakuwa sote tuko njia moja.

Ukipenda ufahamu tofauti na ebola, mgonjwa wa ugonjwa huu, huyo huyo anaweza ugua hata mara 1,000.
 
Njaa imetuponza

Sent using Jamii Forums mobile app

Sana. Kwa hilo hatuna wa kumlaumu bali ni sisi wenyewe. Kabudi alisema hawawezi zuia wachina kuja ni trafiki zetu.

Sina hakika kama anambuka alivyokuwa akiweza press conference na balozi wa China ukitupa updates za huko.

Ajabu haja tokea sasa kutupa za kwetu.
 
Hawa ndiyo wale watanzania wenye uelewa finyu katika ubora wenu.

Kenya wamechukua jitihada kumwezesha mkenya wa kawaida kujimudu kukaa nyumbani. Tozo za kwenye miamala ya mpesa imefutwa. Kodi mbalimbali zikiwamo za pango zimeahirishwa kwa at least 3 months nk.

Mh. Zitto kaandika bandiko Zuri tu lenye kuhusiana na survival katika kipindi hiki.

Unatoka ulikotoka unahara halafu unadhani wanaohara ni wengine. Elimu ni uhuru. Kama elimu yako ndogo usidhani kila mtu ni hivyo. Tunaandika tukawa na data na research zakutosha.

Bila watu kusalia nyumbani kila mgonjwa mmoja hesabu watu wa kufuatilia kama 1,000. Watakapofika wagonjwa 40,000 basi tena, tutakuwa sote tuko njia moja.

Ukipenda ufahamu tofauti na ebola, mgonjwa wa ugonjwa huu, huyo huyo anaweza ugua hata mara 1,000.
Acha uzwazwa wewe
 
Tungekuwa tumezuia wageni wote kuingia nchini bila kuwa cleared na sisi baada ya siku 14 za quarantine balaa hili lisingetupata.

Kwa bahati mbaya, tulijua na hatukufanya.

Hata sasa tunajua watu wote wakisalia majumbani, hakutakuwa na misongamano masokoni, kwenye madaladala, misikitini, makanisani nk. matokeo yake ugonjwa utadhibitiwa.

Ni vyema kuwa wazi uchaguzi mkuu? Potelea mbali. Bora tuwe hai bila huo uchaguzi. Tuipige vita Corona kabla haijatumaliza.

Hili si suala la utani au mzaha wa kina Mwana FA. Italy juzi tu wamekuja watu 475.

Kama yupo haoni dharura kwenye hili mbona itakuwa ni hatari kubwa?
 
Sasa mkuu, si mtu ukitumia muda kurumbana na akili ndogo kama yako hapo sasa, si ndiyo waungwana hawawezi note the difference?
Kabisa unajiona unaakili kwa huo uharo? Tatizo hujijui kama hujui
 
Hii nchi ni tajiri. Kwa hali ya dharura sana ni muda Sasa wa serikali kusitisha miradi yote mikubwa.

Serikali ijipange kuwawezesha wananchi wake kubakia nyumbani sasa kukiwa kungali mapema. Kwa hali ya sasa tukijipanga vizuri hali haijawa mbaya sana. Siku 15 - 30 zinaweza kuwa ndiyo tunazohitaji.

Huenda ahueni wananchi wanayoweza jirani toka kwa serikali inaweza hata ni kiasi kidogo tu.

Tuwe wakweli ukiwa unauguliwa ujenzi wa nyumba hata kama ilikuwa muhimu kiasi gani husimama.
 
Acha kutisha watu basi mkuu..

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu sidhani kama kuna mtu anatishwa.

Hapa tulipo tumejifikisha wenyewe. Tungaliweza kuzuia.

Kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi. Tunakwenda je mbele kutoka hapa. Namna walikofanikiwa ni kwa kuwataka watu kukaa nyumbani na kudhibiti wageni kwa njia ile ile tuliyokuwa tumeipuuza pale awali.
 
Acha kutisha watu basi mkuu..

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu sidhani kama kuna mtu anatishwa.

Hapa tulipo tumejifikisha wenyewe. Tungaliweza kuzuia.

Kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi. Tunakwenda je kutoka hapa?

Kulipofanikiwa ni kwa kukaa nyumbani na kuudhibiti wageni kwa njia ile ile tuliyokuwa tumeipuuza pale awali.

Hebu tujihoji wapi katishwa mtu kwenye ukweli huu?
 
Back
Top Bottom