Corona imetupa picha ya kwanini ilikuwa rahisi kutawaliwa

mzalendo iq1

JF-Expert Member
Mar 10, 2020
1,258
1,541
Poleni na majukumu jana nimesoma habari mbili na kusikia moja inasema Kenya amefunga mipaka yake na nyingine inasema Italia imefungua mipaka ya nchi yake na kuruhusu usafiri wa ndege kuanza kufanya kazi Kama awali pia imepunguza masharti ya Lockdown.

Nikajiuliza hivi Italia ambayo bado ni ya pili duniani kwa vifo vya Corona na maambukizi ya Corona imeona waziwazi kuwa kufungia watu ndani haisaidii chochote it means hatua walizochukua hazikuwa sahihi. Ila anatokea mwafrika anafata njia zile zile mpaka najiuliza au Mungu katuumba waafrika na wazungu kama mfano wa ukuaji lazima waafrika wapitie hatua zote ambazo walipiatia wazungu? Hata Kama ni njia mbovu?

Embu jiulize Corona ilianzia kwa watu weupe wakakaa Lockdown Corona haikuisha. Wakaanza kutoaruhusa watu watoke wakafanye kazi kwani kujifungia ndani haisaidii na kufungua mipaka ya nchi zao. Korona ikafika Africa wakat kwa watu weupe bado ipo na wamesha vunja Sheria za kujifungia ndani sababu hazina msaada waafrica tupo na tume bahatika kuona kila hatua kwa wenzetu wazungu ajabu na sis tumeanza kufanya hatua zile zile Lock down tunaenda kulegeza mashart ya Lock down pia tutaenda kufungua nchi baada ya Corona kuto kuondoka na tutaruhusu wananch watoke kufanya kazi Ila wachukue taadhar.

Sasa najiuliza kuna ulazima Gani wa sisi kuzifata hizi njia kwann baada ya kuona wao wameshindwa kwa lock down tusinge ungana nao kwenye njia ingine ambayo kipindi Corona inafika AFRICA ndio walikua wameanza kuitumia na sio mpaka tuanzie moja?

Ukiwa Makin katika kufatilia haya Mambo utagundua waafrika tuna shida kubwa yani tuko nje ya muda
au huenda wazungu wapo mbele ya maisha yetu uku Yan hatuish nao future moja sababu lazima tupite kwenye kila atua wanayo pitia wao kwann?

Mimi nampongeza magufuli sababu yeye alikua mbele ya dunia mzima na alijua kua Vita hii itaisha kipindi watu wametoka nje wanafanya Kaz zao Ila wanavaa barakoa na kunawa na maji tiririka so hakusubir muda ufike wa watu wote kuliona ilo akaamua aanze alafu wazungu waarabu wa Asia na baadh ya misukule AFRICA itamfata baadae na kweli ulaya yote sasahivi mwendo ni barakoa na osha mikono Ila dunguzetu wa AFRICA muda wao bado mafuta yalio ganda kichwan mpaka yaje yachemke wajue kua ni muda wa barakoa na osha mikono na kuchukua tahadhar dunia mzima itakua imesha maliza hayo ikiongizwa na magufuli

Ila nawahurumia wanatesa wananchi wao ili hali wanajua mwisho utakuaje na ukweli haufichiki sio kwamba watakuwa wameshamaliza Corona kwenye nchi zao sijui watawezaje kutangazia Wana nch kua turud tukafanye kazi vaeni barakoa na osha mikono?
 
Huwezi kwenda tofauti na nature

Huwezi kufungia watu Ndani hiyo sio nature ya mwanadamu
 
Back
Top Bottom