Corner stories.

streat Anthem

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
395
474
Part 1( Corner stoner)

Huwa inakuwa kawaida ya vijana wengi kwenye kitaa chetu kukutana na kujadili mambo mawili matatu.

Katika hiki kijiwe cha kona nitakuwa ninawaletea stori zilizotokea hii pande. Na leo tunaangalia historia fupi ya huyu mwanzilishi wa hiki kijiwe kilichopo kwenye kona ya mtaa wetu.

Huyu kwa jina anaitwa Stoner, ukimuona maumbile yake huwezi kudhani hata kidogo kwanza ni mwembamba kiumbo halafu kapanda hewani, Ngozi yake imepambwa kwa maji ya kunde na nywele zake zimesokotwa kichwani unaweza kuhisi kaweka kamba nyingi za viatu kichwani.

Historia ya bwana Stoner inaanzia pale alipoondoka kwao baada ya kushauriwa na marafiki zake kuwa hauwezi kufanikisha Maisha ukiwa chini ya mwamvuli wa wazazi. Baada ya kusikia ivyo Stoner akajiapiza kuwa ataondoka kwao ili akatafute Maisha mtaani huku akijiamini kwa Elimu yake aliyoipata shule ya Msingi Msingini basi lazima aitumie ipasavyo.

Kitu cha kwanza Stoner alichokiona kuwa ni fursa aliangalia hitaji kubwa la vijana wa mtaani kwao wanahitaji nini?
Baasi bwana Stoner akaona vijana wengi wanataka kuwa high yani kuwa juu kuliko ardhi kwa kutumia nguvu ya Majani AKA Marijuana, akatafuta kijiwe kizuli kitakachowavutia wahusika ili aanze Biashara yake

Na kwa style hiyo ivyo ndivyo Stone ilivyoanza kitaani kwetu.

Itaendelea.........
 
Back
Top Bottom