Core i5 vs Core 2 Duo!

Ryzen

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
7,305
8,655
wale wajuzi leo nimerudi tena naombeni nijuzeni kati ya CPU izo tajwa yaani core i5 na core 2 duo ipi bora kwa matumizi na ambayo haistack stack ovyo yaani yenye high performance mpaka mtumiaji unakuwa hujutii kuinunua!
 
hakuna hata ushindani hapo, core i5 ni nzuri zaidi (most of time)

hakikisha tu hio i5 sio 1st gen maana hio haina tofauti na core 2.

pia kustack stack sio cpu tu inayosababisha, kwa ufupi core 2 duo mambo mengi haitasababisha computer istack.

hard disk ikiwa slow, ram ikiwa ndogo pia husababisha computer kustack.
 
ahsante sana utajuaje Hard disk ipo slow? na kama ipo slow unaeza kuifanya kuwa faster kivipi
 
ahsante sana utajuaje Hard disk ipo slow? na kama ipo slow unaeza kuifanya kuwa faster kivipi
unaifanya faster kwa kununua nyengine,

utaijua kama ipo slow kwa kuangalia task manager au resource monitor pale unapohisi pc ipo slow.

ukiona tu pc ipo slow we fungua task manager kisha angalia cpu, ram na hdd uone kipi ndio kinakukwamisha.

kufungua task manager right click kwenye taskbar kisha chagua task manager au bonyeza kwa mpigo ctrl na alt na delete.
 
nimeclick sasa najuaje kwamba flani ndo inakwamisha boss
 
siku hizi watu wanatumia kitu kinaitwa ssd badala ya HDD.

unaeka ssd hata ya 128gb then operating system unaieka kwenye hio ssd, hdd unaitumia tu kuhifadhi vitu kama movies, documents, miziki etc huku ssd inahifadhi programs.

ssd ina speed sana zaidi ya mara 100 ya HDD
 
nimeclick sasa najuaje kwamba flani ndo inakwamisha boss
angalia hii picha

Windows-10-task-manager-pro-mode-600x558.png

kama huoni kitu kama hiki click show more detail hapo chini itatokea kama hivyo.

hapo unaoneshwa kwa asilimia jinsi cpu, ram, storage na network inavyotumika, ikikaribia 100 ujue hicho kitu kinatumika sana.

mfao ikionesha cpu ni 100% basi cpu yako ipo slow ila ram na HDD havina tatizo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom