Copa Libertadores Final: Boca Juniors and River Plate - LIVE

BREAKING NEWS: CONMEBOL confirms Copa Libertadores will not be played at El Monumental

Nov 27 2018 - 18:48

River Plate will not be allowed to host the second leg of the Copa Libertadores final, CONMEBOL announced on Tuesday.

CONMEBOL has confirmed the second leg of the Copa Libertadores final will not be hosted by River Plate after an attack on the Boca Juniors team bus.
The second leg of the final was due to be played at El Monumental on Saturday but after windows of the Boca bus were smashed on approach to the stadium the kick-off was initially delayed and then postponed 24 hours.
But the match was not played on Sunday either amid protests from Boca, whose players also suffered injuries after pepper spray got inside the bus during the attack.
CONMEBOL held a meeting on Tuesday attended by River and Boca's presidents, after which South America's governing body said the final will be played on either December 8 or 9.
In a statement, CONMEBOL said it intends to play the final outside of Argentina, with the date and venue to be confirmed at a later date
 
Mpaka lini mkuu?

CONMEBOL held a meeting on Tuesday attended by River and Boca's presidents, after which South America's governing body said the final will be played on either December 8 or 9.
 
Hizi mechi huwa zina balaa sana hizi,
Naona kwa sababu za kiusalama kwenye both legs mashabiki wa visiting team hawaruhusiwi kuingia uwanjani, maana wanajua wahuni wana vichwa vibovu
 
Hizi mechi huwa zina balaa sana hizi,
Naona kwa sababu za kiusalama kwenye both legs mashabiki wa visiting team hawaruhusiwi kuingia uwanjani, maana wanajua wahuni wana vichwa vibovu
Hahahaa ni balaa kiongozi
 
.
Screenshot_2018-11-28-09-30-54-445_com.instagram.android.jpg
 
Vz z RIWAYA; MADAM QUEEN
imeandikwa na Halfani Sudy (777)
Whatsapp 0674 395733
Simu 0655 398390

Sehemu ya Ishirini na Nne

Majira ya saa tano na dakika kumi na tisa Mwanasheria mlevi alikuwa katika viunga vya hospitali ya taifa ya Muhimbili. Alikuwa amekaa katika benchi moja mita chache nje ya ofisi ya Dr Ngaga.

Akikaa pake kwa dakika kumi na mbili tu. Ilipotimu saa tano na dakika thelatini na moja alitokea mtu katika usawa kilipo 'control room' na kwa kasi bila hodi kuingia katika ofisi ya mganga mkuu wa hospitali ya Muhimbili, Dr Ngaga.

Mwanasheria mlevi akiwa amekaa pale katika benchi alikuwa amevutiwa na mwendo wa mtu yule, haukuwa mwendo wa kawaida. Ulikuwa ni mwendo wa wasiwasi huku macho yake yakiwa hayatulii sehemu moja.

Yule mtu, ambaye alikuwa amevaa suruali ya 'jeans' ya bluu. Shati jeupe lenye mistari meusi kushuka chini na kujenga taswira ya mnyama pundamilia, huku juu akiwa amevaa kofia aina ya kapelo aliyoishindilia vema kichwani, kwa kumwangalia kwa macho ya kijasusi lakini ilionesha kuwa alikuwa na wasiwasi mwingi sana.

Mtu huyo ndiye aliyemfanya Mwanasheria mlevi kusogea karibu na mlango wa Dr Ngaga kutoka pale katika benchi alilokuwa amekaa. Akiwa pale mlangoni Mwanasheria mlevi alitoa simu yake na kujifanya akichezea huku akili yake yote ikiwa ndani ya ile ofisi. Hakusikia chochote kile kama kuna alichotaka kusikia. Kulikuwa kimya kabisa mithili hakuingia mtu mle ndani.

Akajipa imani asubiri.

Hilo ndilo lilikuwa kosa lake la kwanza Mwanasheria tangu apewe kijiti katika kazi hii ngumu aliyoachiwa na mpelelezi Daniel Mwaseba...

Zikapita dakika tano, ikaja dakika ya sita kwa kasi, ilipokuwa inakaribia dakika ya saba Mwanasheria mlevi imani ikamshinda, akaamua kugonga ule mlango wa Dr Ngaga, hakujibiwa. ilikuwa kimya. Mwanasheria mlevi ulianza kumuingia wasiwasi juu ya usalama wa Dr Ngaga. Aliamua kugusa kile kitasa kwa lengo la kuona mlango umefungwa ama la.
Alipogusa tu kitasa kikaitika.... Mlango ulifunguka!!!
Siku zote jicho halina panzia kama wahenga walivyosema. Jicho la kwanza tu la mwanasheria kuangalia mle ndani alikuwa anatazamana na damu!!

E bwana wee!!!

Moyo ukampiga mithili ya ngoma ipigwayo hovyo. Harakaharaka aliitoa bastola yake kiunoni na kuishika imara kwa mkono wake wa kulia tayari kwa lolote.
Alipiga hatua ndogo kuungia mle ofisi huku bastola yake nyeusi ikitangulia mbele. Alipopiga hatua ya pili ndio aliona vizuri. Ofisi yote ilikuwa imetapakaa damu!!!.
Macho ya Mwanasheria mlevi yalifanya kazi kwa haraka. Lengo ni kuuona yule mtu pamoja na Dr Ngaga walikuwa wapi? Lakini hayakuona kitu...

Ndani ya ofisi kulikuwa kimya kama hakuwahi kuwa na uhai hata siku moja. Zaidi ya damu mbichi zilizotapakaa hovyo mle ofisini hakukuwa na lengine lolote. Mwanasheria mlevi akitanguliwa na bastola yake alipiga hatua na kwenda kule nyuma ya meza lilipokuwa faili la Fabian Kombo ndani ya droo lililopo upande wa kulia. Droo nalo kwa nje nalo lilikuwa limetapakaa damu!
Akalifungua kwa tahadhari kubwa sana...

Asalaleeee....!!!

Alikuwa anatazama na kichwa kisicho na kiwiliwili cha Dr Ngaga kikiwa kimetapakaa damu!!. Mwanasheria alistuka sana. Moyo ulimpiga kwa pupa!!. Pamoja na ujasiri wake lakini leo hii Mwanasheria mlevi aliingiwa na uwoga. Haikuwa kazi ndogo kushuhudia kichwa cha mtu uliyekuwa unaongea nae dakika chache zilizopita kikiwa bila mwili na damu tele...

"Jamaa kamchinja Dokta halafu kalichukua faili la Fabian Kombo..." Mwanashera mlevi aliwaza. "Sasa yule jamaa niliyemwona akiingia humu yupo wapi? Ametokaje humu ndani bila kumuona wakati mimi nipo hapo nje tangu huyu jamaa alivyoingia?"

Mwanasheria mlevi akalifungua droo la chini yake upande uleule wa kulia ambalo mwanzo alipokuja kwa mara ya kwanza hakulifungia. Alichokiona humo nusura atapike. Alikuwa anatazamana na utumbo mbichi wa binadamu uliokusanywa hovyo ukiwa na mabaki ya damu!!! Kama alikuwa anadhani kama aliwahi kukutana na muuaji katili hapa duniani kabla ya leo, basi alikuwa anajidanganya. Leo ndio alikutana na muuaji katili, katili kupitiliza. Jamaa alikuwa ameua kinyama sana na kuyeyuka kwa mtindo usioeleweka kibinadamu.

Mwanasheria mlevi alibaki akiwa amekaa kitini amechoka. Hajui afanye nini? Hajui wapi ashike, wapi aache...

"Huyu jamaa ametokaje humu? Nilikuwa mlangoni muda wote pindi tu alipoingia humu ndani sasa huyu jamaa katokaje?. Jamaa kamuua mtu vibaya sana. Halafu yule jamaa hafanani kabisa na ali..."

Mwanasheria mlevi akiwa katikati ya mawazo ghafla katika mlango wa ofisini uliokuwa wazi waliingia askari wanne kwa kasi, wote walikuwa wameshika bunduki mikononi.

"Upo chini ya ulinzi bwana Songelael!! Tumepigiwa simu na msamaria mwema kwamba umemuua mganga mkuu wa hapa, Dr Ngaga..." Askari mmoja mrefu alisema.

Mwanasheria mlevi alistuka sana. Alikuwa amepatikana kizembe sana. Lilibaki tumaini moja tu kwake kama alitaka kubaki salama. Ni Mungu. Mungu pekee wa mbinguni. Aliangalia juu ili amuombe Mungu amtoe katika kisanga kile kibaya sana.

Kule juu hakumwona Mungu aliyekuwa anataka kumuomba. Alikutana na kamera za CCTV zikimwangalia kimadaha.
Zikimchekea..
Zikimrembulia..
Mwanasheria mlevi akakata tamaa kabisa. Moyoni mwake akajua huo ndio ushahidi utakaotumika kumfanya asote sana jela.
Alimkumbuka Daniel Mwaseba.
Akamkumbuka Dr Yusha.

"Weka silaha yako chini na nyoosha mikono juu!!" Mawazo yake yalikatishwa na sauti ya yuke askari mrefu.

Alivuta pumzi kidogo halafu akazimwaga kwa nguvu.

"Mfyuuuuu.. "

Akilini mwake alijua kwamba suala la Fabian Kombo linabaki kuwa siri, huku akipoteza matumaini kabisa na Dr Yusha, alijua kwamba naye hatafika popote pale katika uchunguzi wake, atabambikiwa kesi kizembe kama ilivyomtokea Daniel Mwaseba, kama ilivyomtokea yeye. Aliitupa bastola yake juu ya meza kivivu. Alinyoosha mikono yake juu kuruhusu kusachiwa na wale askari.

Alikuwa amepatikana...

Mwanasheria mlevi naye yanamtokea ya Daniel Mwaseba? Je yule jamaa aliyeingia katika ofisi ya Dr Ngaga yupo wapi? Nani kawapigia simu Polisi? Maswali ya majibu hayo yapo katika Madam Queen...

Tchaoo..
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom