Conspiracy one

Conspiracy one

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,392
Reaction score
7,873
"Oya kijana"
"Naam bro, karibu"
Alifungua mlango kama haamini vile
"Aisee tumshukuru raisi wa awamu ya sita, anaupiga mwingi, Nimeweza kukuta nyumbani leo, yuko kazini..."
"Yuko site unaambiwa, anaupiga mwingi sana mpaka umeweza kunikuta home leo, kazi iendelee"
Nilimalizia utani ule kama trending ya sifa za ujinga anazopewa raisi wa nchi na vijana kadhaa.

Alikuwa ni brother wangu wa siku zote, huwa anakuja kunitembelea hapa geto na ni siku kadhaa hatujaonana sasa, sijaenda hata kumtembelea, aliingia ndani, sasa leo anakuta mambo hata hayako sawa.
"Vipi kijana umepotea sana aisee, ulikuwa wapi?"
"Nilienda kufatilia baadhi ya job si unajua nipate ugali... "
"Zile job zako za Construction, hivi bado unafanya kumbe ile mifumo ya majitaka sio"
"Ndio bro, si unajua tutumie skill kusaidia mazingira na tupate na Ugali"
"Yeah nakubali, anaupiga mwingi"

Alianza kukagua chumba, na kama kawaida kuniponda hakosi kwa namna yeyote, hii ni kawaida yake,
"Kijana utakuja kufa na njaa humu, yaani hamna hata kilo ya unga, kijana haupiki siku hizi, ndo nyie watoto wa Mama mnakula kwa mama ntilie?"
"Tulia wewe, mafuta yenyewe unayasikia.!? Lita 7500 siku hizi, ngoja nikipata ya mawese kutoka Kigoma nitaanza kupika"
"Usishangae na mafuta ya mawese kutoka Kigoma utaambiwa yamepanda bei"
"Mama yenu yupo kazini, anaupiga kama Magwaya"
Nilimalizia kwa utani.

"Ujue nini bro... "
Nikaanza story nyingine
"Juzi ile naenda Tegeta kuna kazi ya kumjengea mtaja Biodigester Septic Tank nilipata Daladala yenye Wi-Fi nikazama kidogo kwenye Mtandao kuangalia madudu ya wahuni huko, unaambiwa yule Profesa niliekupa story zake amegundua ile CRISPR Technology ya kutengeneza wale watoto amefunguliwa huko China, alikuwa amefungwa"
"Uliniambia lini.!?"

"Hukumbuki niliwahi kukuambia kuna CRISPR ni technology ya Gene editing unaweza kuchukua yai la binadamu na kulifanyia manuva fulani kutumia technology hiyo na akazaliwa binadamu mwenye sifa kadhaa kama unavyokuwa umem-formulate wewe unavyotaka"
"Mmmh, wewe nae umezidi kwa uongo"

"Haya nilikuwa nakwambia sayansi inafanya upandikizi wa moyo unakataa, upandikizi wa ubongo unakataa, hibernation unakataa, figo na maini kuamishwa, unakataa, tena sio figo tu, ni mtu kupewa figo ya Kitimoto, unacheza nini.!? Sasa unaambiwa kijana na team yake ya Gene editing walifuma mayai ya mtu na kuyapandikiza kwa wanawake kadhaa, ilikuwa juzi tu hapo 2018, hukusikia.!?, Watoto wameshazaliwa mbona, wanaitwa Lula na Nana, ila mshikaji wakamfunga wachina, sasa ndo niliona ameachiwa tena"

"Sayansi itakufanya uwe kichaa kijana wangu, na nyie wanasayansi mtakuja kutuua aisee"
"Sio tutakuja kuwaua, tumeshaanza kuwaua"
"Wewe kijana umegundua nini sasa na wewe wazungu wakikuita utawaonesha nini maana wao kila siku unasema wanaonesha kipya"
"Kabla sijakuonesha nilichogundua au mpango wangu, kwanza niwaoneshe ambao sio wanasayansi kile ambacho wanasayansi uchwara wanafanya huko nyuma ya pazia, huo mpango wa kupoteza dunia upo kwenye mikono ya baadhi ya wanasayansi wanaoongozwa na wanasiasa"

"Kama upi.?" Aliuliza
"Kama huo wa Metabiota niliokuambia juzi"
"Alafu nimekumbuka, ulisema Metabiota inahusika na Corona, yenyewe iko Marekani, Virusi vilianzia huko China inahusikaje?"
"Cha kufahamu bro, mpango wote wa hicho kinachoitwa Virusi ni mchongo, siku nyingine nitakupa maana ya Virusi na nikusanue mchongo wa Classification of living things, virusi havimo, utashangaa"

"Kwanza Metabiota ni kampuni la Kimarekani, Lakini lilitumika huko Ukraine kuunda virusi vya Corona na kuvisindika China ambapo daktari kwenye ile maabara iliyokuwa inalengwa kuwa na uhusiano flani hivi wa kiuchunguzi hakujua ni nini kimo kwenye zile sample... "

"Unajua Virusi vilipotapakaa, Dakitari kadhaa walikamatwa na kufungwa huko China kwa kosa la kuvujisha Virusi walivyotengeneza kwenye maabara, lakini baada ya kugundua ni mchongo wa Ukraine uliosimama kwenye nguzo ya Marekani, waliamua kuwaachia wale madaktari na kuanza kutafuta neno lolote la kuficha ukweli huo mpaka watakapo jiridhisha...."

"Walichokifanya, ni kuanza kutafuta aina fulani za vyakula ambavyo china wanakula lakini vinapigwa vita Magharibi na kusingizia kuna uhuasiano wa Virusi kutoka kwenye wanyama na Vyakula hivyo, zile popo, sijui Nyoka, sijui Farasi na wadudu wa kichina walisingiziwa tu kufunika kombe...."

"China ilichokifanya ni kutafuta dawa walau ya kupunguza maumivu kwa watu wake, unajua China wala haikujihusisha na kutoa chanjo duniani, ilikaa zake tu kimya wakawa wanapiga makelele wengine utafikiri wao ndio ugonjwa umeanzia kwao, China walitafuta njia za kuondoa virusi hivyo kwenye mazingira, alafu sasa wakavi-boost mara mbili zaidi na kuvisambaza tena Ulaya..."

"Kilichotokea Italy na nchi nyingine za Ulaya ni Mungu anajua, Ulaya ikatetemeka kama Mayele, Marekani alishajua kimenuka huko, alikuwa kiherehere wa kwanza kuomba WHO kutoa rai ya karantini na kufunga mipaka si wanajua china watavileta virusi, China wakaona kumpata mmarekani wataanzia Kusini huko, Kitu ikatupwa Rio De Janeiro, Brazuka huko, mpaka shida inafika Mexico Marekani walikuwa wameshaweka Ukuta, lakini hawakuchomoka..."

"Likawapata, Serikali ikajua ule mchongo kimeumana, ilitoa kandarasi kwa makampuni makubwa matano kwao, na formula ya kirusi wakaiweka live bila chenga, 'Jamani kirusi ni hiki Tafuta antidote', chap kwa haraka ndani ya miezi miwili Chanjo ikapatikana...."

"Unafikiri kama lingekuwa swala la kuanza kutafiti dawa ya kirusi wangeipta ndani ya miezi.!?"
"Sidhani, hata HIV imewazengua" Akajibu
Nikaishia kuguna tu...

Hii ni Conspiracy.!
Itaendelea....
 
Back
Top Bottom