Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,753
huu ndo ubinafsi, it is all about nitapata nini toka kwa hawa watu....Fuata nyuki..................,ukikaa karibu na waridi...............ukitembeana na mchina lazima utajua katare
hapo kwenye RED nimewahi kuulizwa na watu siku "inawezekanaje fulani ni rafiki yako lakini mna tabia tofauti? mbona wewe hauko kama yeye?"Ndege waliofanana huruka pamoja, so haiwezekani mkawa marafiki wakati Tabia zinatofautiana, ni lazima kuna tabia zinazofanana. Ni sawa na kukaa na Mwizi lazima nawe iko siku utaiba tu, Au kukaa karibu na Uaridi lazima unukie vile, au kukaa na mtu mwenye Pesa kwa vyovyote nawe utakuja pata pesa, So be care kwa uambiwacho.
Ndege waliofanana huruka pamoja, so haiwezekani mkawa marafiki wakati Tabia zinatofautiana, ni lazima kuna tabia zinazofanana. Ni sawa na kukaa na Mwizi lazima nawe iko siku utaiba tu, Au kukaa karibu na Uaridi lazima unukie vile, au kukaa na mtu mwenye Pesa kwa vyovyote nawe utakuja pata pesa, So be care kwa uambiwacho.
asante sana kwa mchango mzuri.....Swala la kuwa "bendera fuata upepo" sio la watoto tu, hata watu wazima wapo wanaofuata mkumbo sana tu. Na watoto wapo wengi tu wenye misimamo wasioiga iga mambo hovyo, niliwahi kuwa mmoja wao.
Binafsi naamini mtu wa kupotoka atapotoka tu hata awe na marafiki wazuri namna gani, maana asiposhawishiwa na marafiki atashawishiwa na wapita njia. Na mtu mwenye msimamo wake hawezi kuwa na tabia za ajabu ajabu kisa tu ndo marafiki zake walivyo. Kama mimi marafiki zangu wengi wanatumia pombe ila mie sijawahi na wala sitarajii japo wapo wanaoshawishi hata nijaribu tu. Ukiwa mtu mwepesi kufuata mkumbo na kutaka kufurahisha (please) kila mtu ndio huo msemo wa "Ndege wafananao huruka pamoja" unakuhusu.
Umeona eeeh!Hahahahah, kaaazi kweli kweli.
Eti "ukikaa na mtu mwenye pesa kwa vyovyote nawe utakuja pata pesa".
huu ndo ubinafsi, it is all about nitapata nini toka kwa hawa watu....
kwa nini usiamue wewe kuwa waridi kwa hao wenye tabia zisizofaa? i.e. wao wanukie toka kwako
Nilichokuwa namaanisha ni kwamba utajua njia zooote afanyazo kupata pesa zile so nawe utazifuata na kupata pesa.Hahahahah, kaaazi kweli kweli.
Eti "ukikaa na mtu mwenye pesa kwa vyovyote nawe utakuja pata pesa".
Nikiwa darasa la 5 tulihama mji na kuhamia sehemu nyingine. Mama alinitambulisha kwa mtoto wa rafiki yake (binti) ambaye tulikuwa tunasoma darasa moja.Chances are 50/50 to influence or to be influenced with.But its more likely if u hang up with bad company in one way or another,direct or idirect u will be affected by it.
kuna wengine marafiki lakini wachoyo kwenye michongo ya hela!Nilichokuwa namaanisha ni kwamba utajua njia zooote afanyazo kupata pesa zile so nawe utazifuata na kupata pesa.
Thank you rafiki na mwalimu.....binafsi huwa siamini dhana hii kwa mtu ambaye ni mzima na anautashi wake, ila tu hili linaweza kwa watoto ama wanafunzi.
mfano sio kwamba marafiki zangu wote nilionao wanatabia njema ila wapo ambao nawajua kabisa tabia zao ni mbaya na kuwa rafiki yao mimi natumika sana kuwarudisha kwenye mstari kila iitwapo leo.
mara nyingi sana ni vyema kumrekebisha mtu mwenye tabia mbaya kwa kuwa rafiki yake na kila siku akajifunza jambo toka kwako ama kwa kukusudia ama wakutokukusudia.
mf, ninaye wifi yangu ni MD sasa anapoishi kuna kijana mmoja mzazi wake alikuwa mkuu wa wilaya na sasa ni marhem huyu kijana kwa kukosa mtu wa kumwongoza amekuwa ni mlevi wa kupindukia hadi anajikojolea. sasa wifi yangu huyu kawa rafiki wa huyu kijana kiasi kwamba hata kwake anakuja wanaongea na wanatoka nae kwenda kunywa nia ya wifi ni kumbadilisha so anapokunywa nae yeye wifi anakunywa malta kijana anakunywa bia ila ana muhesabia zikifika 3 anamwambia haya sasa tuondoke uende nyumban ukalalale, kweli kijana kwa kuheshimu urafiki wake kwa wifi ananyanyuka na kurudi home kabla hajalewa. mumewe wifi imebidi amchukue huyu kijana awe anaenda nae kwenye kazi zake as a friend ili tu abadilike na kuacha pombe kabisa. kwangu mm niliwapongeza sana nikamwambia wifi yangu atakuwa na baraka sana manake anabadili wale ambao jamii inawadharau na kuwatenga.
rafiki ni rafiki mtani..... hata wale wa jinsia nyingine......Unazungumzia pia kuwa na marafiki toka jinsia nyingine............Wale vipanga ambao sketi haikatizi kwao.!
Labda kabla ya kuchangia tujiulize urafiki ni nini hasa? Na unajengwa na nini? Na kigezo cha kuwa na rafiki ni kipi? Na yapi yanawaunganisha ktk urafiki?Jamani tumesalimika ndugu zangu?
Nina hili jambo huwa naliwaza sana na labda sielewi kwa nini watu wengi wana mtazamo tofauti na ninavyoamini mimi...
Ni hili swala la marafiki wa kuambatana nao (hapa naongelea marafiki wa kawaida tu na siyo wapenzi).
Watu wengi wanasisitiza sana watu wasiambatane na marafiki wenye tabia "mbaya" kwa sababu wanazozijua wao. na hili limenichanganya zaidi baada ya kulisikia jana kwa mtu ambaye sikutegemea angewaza hivi.
Mimi naamini unaweza kuwa na marafiki wenye hizo tabia na wewe usiwe/usiige hizo tabia zao.
Labda mimi sielewi mtu mzima unawezaje kuwa influenced na tabia ya mtu mwingine ambayo unaona siyo nzuri?
NOTE: HII NAONGELEA WATU WAZIMA AMBAO WANAJUA KUTOFAUTISHA JEMA NA BAYA, TUSIHUSISHE WATOTO KATIKA MJADALA HUU
rafiki ni rafiki mtani..... hata wale wa jinsia nyingine......
ukipanga wake unakuwa influenced na huyo rafiki, au ni tabia yake tu?