CONFIRMED: Kigwangala atangazwa rasmi mshindi Nzega | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CONFIRMED: Kigwangala atangazwa rasmi mshindi Nzega

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Invisible, Nov 2, 2010.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Nov 2, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  CCM - 20,470
  CHADEMA - 8,056
  CUF - 5,833 (Wamepata kata ya Nzega mjini ambapo Dr. Slaa kaongoza kura za urais)
   
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Too SAD. Minyamwezi bwana, akili zetu ni Nuzri sana kuwa kwenye karne ya 16.
   
 3. P

  Pattie Member

  #3
  Nov 2, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I don believe it, kweli huyo jamaa amechukua jimbo la nzega? n then Dk kaongoza kwa kura ngapi?
   
 4. S

  SUWI JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Sad:A S angry::A S angry::A S angry::A S angry::A S angry:
   
 5. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #5
  Nov 2, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Wamechakachua
   
 6. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #6
  Nov 2, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,780
  Likes Received: 6,261
  Trophy Points: 280
  Kigwangala ni ''mwanasiasa'' mzuri. Anajua kujenga hoja. Nilikuwa namuona enzi zile wanafunzi wa Muhimbili wamegoma.

  Inaonekana wakazi wa Nzega wamefanya uchaguzi wao kwa kuangalia mtu na si CHAMA - ndio maana Dr. Slaa kapata kura nyingi za urais
   
 7. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #7
  Nov 2, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Bado kidogo nimzuie Invisible asitangaze result za kuumiza kama hizo lakini hamna jinsi.
   
 8. msikonge

  msikonge Senior Member

  #8
  Nov 2, 2010
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Akiamua kuchapa kazi watu watamtukuza na Mungu atambariki!
   
 9. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #9
  Nov 6, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Oyaa mbona wengi humu mlikuwa hamtaki nishinde? Hivi mimi kupata bahati nimekosa nini jamani?

  Mi mpiganaji tu, wengine mnadai nimeteuliwa, basi mara anafanya kazi kwa mke wa rais, mara kabebwa na riz1, mara vile! Hivi nyie hamuamini mungu yupo na anatuona sisi wachache wenye dhamira safi? Wapiganaji wa ukweli? Watafutaji tusioogopa wala kubadili nia, hata kama unajua una nafasi ndogo ya kupata? Nyie hamuoni kama nimepata kibahati sana jamani?

  Hebu angalieni wasifu wa wapinzani wangu wa karibu halafu mnitafute na mimi...kama hamtogundua Kigwangala ni mhangaikaji ambaye ndoto ya jaha ilimuangukia na pengine mungu amemtuma kazi maalum! Basi watu mmebaki mkitafuta mchawi tu! Mtamsingizia Kikwete, Riz1 na mama yake - wakati wala huyo mnyamwezi Kigwangala hawamjui wala hawajawahi kukutana naye!!! Kikwete ameniona mara ya kwanza alipokuja kupiga kampeni Nzega! Can you imagine? !

  Spirit yangu ndo imenifikisha hapa, huwa siogopi kutafuta kitu, I always believe in myself and my abilities! Huwa najiamni sana na hupigana bila kukata tamaa...ungefika Nzega ungesema jimbo limekwenda CHADEMA hilo, lkn sikukata tamaa, niliendelea kujipanga na kufanya kampeni za nguvu zaidi mpaka watu wakanifahamu vizuri, wakauona uwezo wangu, wakaniamini wakanipa kura nyingi kiasi hicho! It takes a braveheart to be in my position and to persist and win such a challenging election!

   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  Nov 6, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  hongera, kafanye kazi uliyo tumwa na wana Nzega/ watanzania....
   
 11. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #11
  Nov 6, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Dr. Kigwangalla,

  Mkuu hongera zako; ni lazima tukubali kutokubaliana. Wewe ni mmoja kati ya MPs wapya wa CCM ambao mpo JF; tunatumaini pindi Bunge litapoanza hamtatukimbia ili wadau waweze kuwasilisha kero zao nanyi msaidie kuziwasilisha mjengoni.

  Challenges unazokumbana nazo hapa JF ni sehemu ya maisha ya mtaani, wale wasiokuwa jimboni mwako ni wazi wataongea mengi kwakuwa hawajui kinachoendelea huko; huwezi kum-please kila mtu mkuu
   
 12. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #12
  Nov 6, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,206
  Likes Received: 3,620
  Trophy Points: 280
  Dr;

  Please fikisha ujumbe wangu huu Bungeni;

  Mosi,kahoji wabunge wa viti maalum wanamsadia nini mtz wa Nzega?Kawasilishe hoja kwa sababu wabunge hawa wasio na Jimbo wanatafuna sana uchumi wetu;je siyo jambo la busara kama wakifutwa?

  Pili,Ma RC na ma-DC wanafanya kazi gani tofauti na kazi za Wakurugenzi wa miji?Kwa nn vyeo hivi visifutwe na fedha tutakazo ziokoa ziingizwe kwenye miradi ya maendeleo?

  Mwisho,kwa nini TZ tusiwe tunawathibitisha Bungeni wataalam wanaoteuliwa kama vile Majaji au makamishna wa Tume mbalimbali ikiwemo ya Uchaguzi ambako pindi wakithibitishwa na Bunge Rais HAWEZI tena kuwa na uwezo wa kuwafukuza na hii itafanya wafanye kazi zao bila kuogopa kufukuzwa na Rais!

  Weka akilini kuwa baada ya mamlaka kumsafisha Kijana Bashe atakuja kukupinga huko mwaka 2015 kwa hiyo fanya kazi kweli kweli ili kujiongezea kura kwenye uchaguzi wa maoni ndani ya chama chako mwaka 2015!

  Nakutakia uwakilishi mwema Dr!
   
 13. N

  Nampula JF-Expert Member

  #13
  Nov 7, 2010
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 254
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hongera dr usisahau taaluma yako ya elimu na pia wananchi waliokuchagua............hapa jf utapambana na vichwa ambavyo vitakusaidia sana mjengoni.always maslahi ya nchi yanakuja mwanzo kabla ya maslahi yako binafsi.
   
 14. i

  ilboru1995 JF-Expert Member

  #14
  Nov 7, 2010
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,331
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ... Ana tembea kama bata, anakula kama bata, anahema kama bata, ana... kama bata; Huyo ni bata tu... huwezi kuwa mtetezi wa MAFISADI then ukasema wewe siyo kati ya hao MAFISADI... CHalii yangu unafahamu fika kuwa UMECHAKACHAU KUANZIA KURA ZA MAONI MPAKA ZA UBUNGE... YES Tunajua mlichokifanya.
   
 15. M

  Masauni JF-Expert Member

  #15
  Nov 7, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hamisi nakufahamu wewe ni mpiganaji tangu tunasoma wote MUCHS, Tatizo chama ulichopitia kitakudhibiti tu ufanye kile CCM inachoamini na inachotaka si wananchi wa jimbo lako wanachotaka. Si unaona akina Anna Kilango walivyozimwa midomo kwenye ishu za ufisadi. So dont expect you wiil do much.
   
 16. mudushi

  mudushi Senior Member

  #16
  Nov 7, 2010
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 152
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hawa wanyamiezi (mingi) wamelala wataamka kwenye operation sangara ijayo.
   
 17. luvcyna

  luvcyna JF-Expert Member

  #17
  Nov 7, 2010
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 1,034
  Trophy Points: 280
  Nakuonea sana huruma kaka,pamoja na pongezi unazostahili ila walio kuzunguka kama bado basi tegemea watahakikisha uwe mmoja wao,otherwise nakushauri jaribu kufuata nyayo za mwakyembe..n watchout
   
 18. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #18
  Nov 7, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  hongera kwa kuchaguliwa nafasi ya kuwakilisha wananchi bungeni

  kutokana na nafasi uliyo nayo, ningekuomba uanze kuji upgrade kwenye matumizi ya lugha pamoja na uandishi huku ukiendelea kuwatumikia wananchi wa jimbo lako.

  ** ni nyota ya jaha sio ndoto ya jaha.
   
 19. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #19
  Nov 7, 2010
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kigwa usitake kutudanganya, hata kama una dhamira ya kweli hutaweza kwani chama ulichomo tunajua chama kwanza wananchi baadae, unaweza kuwa na dhamira nzuri lakini chama chako kitakuangusha, kwa kuwa najua nawe utapenda tena uteuliwe kuwa mgombea tena usingependa ukiangushe chama chako, fisadi huzaa fisadi.
  Hata hivyo sidhani kama nawe ni msafi kihivyo kwani nimesikia ulitaka kuvuliwa madaraka kwa ubadhirifu wa fedha ulipokuwa kiongozi wa chama kimoja chuoni kwako ukanunua gari, sina uhakika lakini yaweza kuwa kweli.
   
 20. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #20
  Nov 7, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,173
  Trophy Points: 280
  Mbunge Kigwangalla anaamini kushinda kwa bahati? Hivi tutamaliza umaskini kwa fikra za kufanya mambo kwa kubahatisha? Anaona mzigo wa kuwatumikia watu masikini bahati? Au pengine hajui hata kama huu ni mzigo, anaona ulaji na power, ndiyo maana anaona "bahati".

  Hivi huyu si ndiye yule jamaa kaja na narrowminded notions za kutaka kulazimisha kila mtu ajitambulishe kwa jina lake la ukweli hapa?

  Mtu kupata ubunge tu kila kitu "mimi" "mimi", hata siasa za kushukuru wapiga kura wako hamna, umebaki kujitamba na "spirit yangu tu ndiyo imenifikisha hapa". Hata huyo Kiranga high priest of cockiness anakusema kwenye hili basi ujue kasheshe.

  Just goes to show you madudu tuliyonayo bungeni.
   
Loading...