Confession of mad philosopher

Confession of mad philosopher

Marcovicsavic

Senior Member
Joined
Nov 14, 2020
Posts
132
Reaction score
308
Maana ya uhuru huisha baada ya utambuzi

Baada ya kutambua kwamba uhuru si maamuzi

Maana Kifungo na mipaka vinafanana
Aliyekuambia kuna uhuru utaupata kakudanganya

Ipo asili inayofanya mwili wako mashine

Kufanya Ugonjwa uwe jela alafu afya ni jela nyingine

Mjamaa amemwaga damu tayari
Awe huru ili akawe mtumwa kwa mabepari

Chagua kufa ukiona waja hawalipi wema

Kufa wokovu kilichokufa hakifi tena
Kufa ni uhuru kamili tabu ni nini
Haupo huru sasa uhuru wa kweli ni kaburini

Unakumbatia uhuru wa kuambiwa
Wakati unaishi na haukuchagua kuzaliwa

Uhuru hautafutwi msafiri pumzika kubali chai
Hauwezi kuwa huru ungali hai

Uhuru si halisi jamaa badili umbo
Uhuru sio jibu hata usikariri fumbo
Uhuru ni falsafa ya vitabu iliandikwa na mababu
Tutaisoma na mwisho itabaki huko

Anayehitaji uhuru aelewe
Kuogopa kufa ni utumwa kwa maana kufa ndio uhuru wenyewe
Hata uwe mfalme ambaye anatoa idhini

Huwei kuwa huru uhuru wa kweli ni kaburini

Ukikumbatia mwanga jua utaificha nuru
Uhuru si kwa mwafrika kumkimbiza mkabulu
Kuutaka uhuru sana jamaa si dalili njema
Kama upo hai na unahisi uko huru fikiri tena

Cheo huleta nuru pahala nuru haifiki
Na pesa ndio njia ya uhuru ukiimiliki
Pesa na cheo upita kule hakuingiliki
Alisema mlevi mmoja ambaye pombe tu imemdhibiti

Mwathirika ambaye dawa za kulevya zimefunga
Na anahisi yuko huru mara baada tu ya kuvuta
Labda si kweli haupo huru ukijiongeza
Maana ukishaujua uhuru tayari ushaupoteza

Je utaniona chizi au mwivi
Au pumbavu au mshenzi ninayeongea vituko
Au utaamua ukae chini utafakari
Kisha ukakubali ndoa ajira navyo pia vifungo

Aliye huru ni nani nieleze mtoto anayeenda kwa viboko
Au mlokole mtenda mema baada ya kutishiwa moto
Au msomi elimu mpaka chuo kihakiki
I swera kama uhuru ndio huo siuafiki

Anayehisi yuko huru pita mbele
Piga kelele maana hata Mungu wako hayuko huru
Hawezi kubadili mipango hawezi kumuumba
Mungu mwingine mkubwa kupita yeye

Unaetafuta uhuru wa kweli utateseka
Utapoteza damu utatoa machozi na utakesha
Hauwezi kuupata maana hakuna ulipouweka
Uhuru haupatikani kwa fedha

Uhuru is priceless kwakuwa si bidhaa halisi
Wenye chapaa walihakiki
Utaniangusha sana ukishindwa kuamini
Upo uhuru ila uhuru wa kweli ni kaburini
 
Hizi tungo zingekaa kwenye vitabu na kuhifadhiwa kama hamlet au macbeth za william shakespear ingependeza sana
 
Back
Top Bottom