Concept ya uvumilivu katika Ndoa.

Concept ya uvumilivu katika Ndoa.

Joined
Mar 6, 2013
Posts
13
Reaction score
3
Hivi hii concept ya uvumilivu huwa ina maana gani katika ndoa au mahusiano?
Imagine mwanume ameshaku cheat na wanawake kama nane hivi na unawajua na ni wa uhakika sio wa kuhisi (still bado upo unavumilia) hao ndo unaowajua pia kuna wale usiojua kabisaaa! This ni within six years since umemjua.

And sometimes mwanaume anakujibu its true that am doing this and this outside (akitamka lile neno tendo )we amua utakavyoona.
Anaweza asikusemeshe mwezi mzima anaingia na kutoka, nyumba inakuwa kama changing room.
Na mtu haonyeshi dalili za kuja kubadilika maana ni kama vile hizi tabia zimekuwa sehemu ya maisha yake , waswahili husema ni kama kachanjiwa .

Mtu ambaye haombi msamaha kwa mke wake wa ndoa! , mtu ambaye ha feel guilt! Mtu ambaye haoni hata chembe ya aibu kwa matendo yake. Tena atakujibu mbona fulani anafanya hivi na wanaishi vizuri na mke wake !!!

Is this love ? is how marriages / relationships supposed to be??
Au maana ya ndoa ni huzuni , machozi ....etc

Kwa concept hii ya UVUMILIVU imepoteza sana maisha ya watu esp akina KE kuliko akina ME .

MFANO:
1) Juzi kuna rafiki yangu alikuwa anahadithia kuwa alimpoteza mama mkwe wake kwa sababu ya hii concept ya uvumilivu . Kivipi? Huyu mama alikuwa na amekuja dar kumsaidia huyu rafiki yangu alikuwa kajifungua sasa mama mkwe kila akimpigia simu kumfahamisha mumewe kuwa siku fulani anarudi home mume anajibu oooh endelea kukaa huko mtoto bado mdogo . Sasa mama mkwe wa huyo dada akaamua kufunga safari kurudi kwa mumewe mkoa alipo fika kuingia chumbani kwake akakuta (pichu) nguo ya ndani pamoja na kanga chumbani kwake , mara akaanza presha kalazwa siku mbili akafariki. Uvumilivu umepelekea mpaka mpaka kifo cha huyu mama.

2). Kuna rafiki yangu alikuwa na boyfriend wake siku nyingi sana , huyo boyfriend alikuwa ana mambo ya kucheat kweli my friend alikuwa mvumilivu sana lakini ikafika siku akaamua kufanya maamuzi ya kuendelea na mambo yake. Yule kaka akaja akaoa kaoa nadhani alipata mpaka na mtoto lakini hivi ninavyoongea amefariki mwaka jana kwa HIV , mke wake kafariki mwaka huu . Yaani Rafiki yangu huwa anamshukuru Mungu kwa kumpa ujasiri wa kuweza kuachana na huyo BF wake maana leo angekuwa marehemu pia.

3)Mwingine ni dada yangu mtoto wa mjomba nae alikuwa mvumilivu sana kwa bwana wake , kwani alikuwa akishauriwa kuvumilia kila mara at the End akafariki kwa presha na msongo wa mawazo. Na hivi ninavyoongea huyo aliyekuwa mume wake ni HIV +. REST IN PEACE MY SISTER .
*these are true examples*

JE HII CONCEPT YA UVUMILIVU INA MAANA GANI??

MI NAHISI CONCEPT YA UVUMILIVU IWE APPLIED LAKINI IWE NA KIKOMO PIA.

ALWAYS TOO MUCH IS HARMFUL.
 
Dada yangu tatizo ni watu kutojitambua na wajibu wao katika ndoa. Any sisi ambao hatujaoa na kuolewa ni fundisho kwetu.
 
Moja na moja = mbili
Moja na moja = sifuri
 
Thread nyingine unapozisoma unapata shida sana, maana unahisi hadi maumivu ya roho na mwili, inakugusa kana kwamba wewe ndio umetendwa.

Pole dada kwa hayo ambayo umepata kuyashudia na kuyanena hapa kwenye jukwaa, hakika haya yapo tena mengi sana ijapokuwa lazima tuwe wakweli haya yote yanatokea kwa pande zote namanisha jinsia zote mbili (Me & Ke) ingawa kwa upande wa Ke imekuwa rahisi sana kusikika kwenye public tofauti na upande wa Me ambao walio wengi hukaa kimya kwa kuona aibu fulani huku ndoa ikiliwa na mchwa.

Uvumilivu unatajwa kwenywe viapo vya ndoa, wanandoa wanakubali kuishi katika shida na raha, ni kweli ni jambo jema kufanya hivyo, lakini pia imeandikwa ya kwamba "Ndoa na iheshimiwe na watu wote". Hapa utaona kwamba kumbe uvumilivu unaotajwa ni juu ya mambo mengine ya kimaisha ambayo yanaweza kuwa ya kupita nk, ila maandiko yanapotuasa kuiheshimu ndoa kwa pamoja yanatuambia tupendane kwa dhati kwenye ndoa yetu ili kutimiza mapenzi ya Mungu kwa kuitika wito wetu hapa duniani.

Kumbe basi tunaposaliti ndoa zetu kwa kigezo kuwa tuliapa kuwa na uvumilivu tunafanya kosa kubwa sana mbele za Mungu na wenza wetu. Tunavunja amri ya sita na tisa kwa kisingizio cha kwamba tutaombwa tuvumiliwe, na nani sasa ili hali tunamkosea na Mungu pia, hii haikubaliki hata kidogo.

Endelea kumuomba Munngu akusaidie ili mweza wako amuche Mungu na kwa kufanya hivyo hatakuumiza wewe binafsi na familia yako.
 
Mhhh kweli ndoa zina mengi na huu muda wa uchumba na mapenzi yana mengi sana. Ndoa na iheshimiwe na watu wote na kila mmoja awe na wajibu na atimize wajibu huo
Inapotokea kuna upande haujui wajibu wake na unashindwa kuyatimiza basi mahusiano hayo yana shida
Sidhani kimeandikwa kuwa uvumilie tuu kw akuwa imesemwa kwenye viapo hata utakapoona mumeo au mkeo anakuletea nyumba zake ndogo mpaka chumbani kwako na bado wewe uendelee kuvumilia tuu kwa kuwa kuna kiapo
Kuna sehem inabidi uwe na kikomo cha uvumilivu na kusema sasa basi, hapana, kama ni kuunyanyasa utu wako ushanyanyasika vya kutosha na kama ni kukuumiza imetosha na unatakiwa kuendelea mbele na maisha yako. Huwezi kuvumilia wakati unaona kabisa kuna hatari ya kupata HIV au kuna hatari ya kuuwawa eti kwa vile tuna kiapo
Uvumilivu una kikomo na wala sio muda wote unaweza kusema wacha tuu nivumilie yataisha kuna watu wengine hawana break na hawaoni kama kile wanachokifanya kinaumiza au kina madhara
 
.. Uvumilivu una mwisho wake, especially kama mvumiliaji anajitambua na anajua nini thamani ya maisha yake na hayo mahusiano aliyopo.

Ktk post yako .. Nimeshangaa na kuchoshwa sana na huyo aliesema mbona mume wa flani anafanya hivi na mkewe hana shida na hilo.. Kaaaaaa.. Kanichefua kweli.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Concept ya uvumilivu katika ndoa mara nyingi inawekwa kwa wanawake. Yaani vumilia kila kitu , no matter what, hadi kifo. Mradi unaingia kaburini bila mhuri ya "DIVORCED" basi umefanikiwa kila kitu. This is an old way of thinking. Imagine wanaume wangekuwa wanafanyiwa hivi vituko vyote wangevumilia? Kuletewa mahawara, kuishi kama maadui, magonjwa, watoto wa nje, matusi juu!

Mwaka juzi nilirudi nyumbani kusalimia nikakuta mama mdogo (mke wa mdogo wake baba) ana bonge la kovu juu ya jicho. Mama aliniambia alikuwa anasema alianguka toka kwenye bodaboda, kumbe ni mume wake alimchoma kisu. Na ni mama mzuri kwa sura na tabia, but there they were wameambatana na mmewe kwenye sherehe. Miaka kama 10 iliyopita aliletewa watoto wa nje wawili. Akaletwa mke mwenza lakini alifariki muda mfupi baadae.

Wanawake wanapitia mengi, we acha tu. Suluhisho ni kuelimisha wanawake na mabinti ili wajitegemee. Hiyo ni dawa ya mfumo dume.
 
Hapo kwenye uvumilivu kweli kunasababisha watu waonekane kama wagonjwa,au wadhoofu ukiona uvumilivu unapelekea kuathiri afya yako ni bora kuachana kwa vile uhai wako ni kitu muhimu kuliko penzi unalopigania ambalo limeshakuwa chanzo cha kero.
 
Uvumilivu wa ndoa ni 'a two-way street'. Uvumilivu huo hauna maana bila tija chanya upande wa pili.
 
Concept ya ndoa ngumu sana, na ndo maana Yesu aliamua kufunga talaka. Katika ndoa za Kikristu kama talaka zingeruhusiwa ingekuwa balaa. Hebu angalia nina rafiki yangu mmoja, aliolewa na mtu aliyem bikiri baada ya kuwa kwenye relation miaka 6. Baada ya ndoa mwaka mmoja na nusu na wakiwa na mtoto wa kiume (mtoto mzuri sana yule aisee), ndoa chali. Dada analalamika since November 2011 hajaliona tendo la ndoa. Mbaya zaidi jamaa kazaa na muhudumu wa bar (jamaa ni mlevi sana), kachukua binti mwingine na anataka kufunga ndoa bomani.
Chukulia maisha ya yule dada, zaidi ya mwaka bila haki ya ndoa, na mtu mwenyewe kicheche, akilewa hachagui. Jamani tuziombee hizi ndoa, na KILA MWENYE NDOA AIHESHIMU NDOA YAKE.
Bwana awabariki sana wapendwa.
 
nimesikitika, nimefadhaika, nimenyong'onyea
inaumiza, inagusa moyo, inasononesha
poleni nyote mpitiao magumu haya
maombi ndio silaha yenu, kinga yenu
 
..JE HII CONCEPT YA UVUMILIVU INA MAANA GANI??

MI NAHISI CONCEPT YA UVUMILIVU IWE APPLIED LAKINI IWE NA KIKOMO PIA.

ALWAYS TOO MUCH IS HARMFUL.
Inategemea sana na principles unazotaka kutumia katika kufanya maamuzi. Kama umeegemea kwenye dini (ukristo?), tunaambiwa tusamehe 7x70 na pia mtu akikupiga kibao shavu la kushoto, unamgeuzia na jingine! Kama Bwana angehesabu mauvu yetu, ni nani angesimama? So kwa misingi wa imani ya kikristo naamini uvumilivu ni kama vile hauna kikomo.

Lakini hii haina maana kuwa tunavumilia bila kuchukua hatua! "Tunaomba" vya kutosha? Tunamtegemea Mungu kwa kiasi gani katika kutatua matatizo yetu?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom