Computer science ni sahihi kweli?

papatunde jr

Member
Joined
Jun 30, 2016
Posts
56
Reaction score
33
Wakuu a.aleykum
Selection za chuo zimetoka nimepata computer science ifm,kwangu naona sawa kwa sababu ya kukua kwa teknolojia hivyo demand ya wataalamu itaongezeka,tatizo napata upingamizi mkubwa toka kwa ndugu wakinipa sababu tofauti pasipo kutaka kujua kitu gani ninachokipenda, naomba mitazamo yenu wakuu,computer science ni sahihi kwangu?
 

Mambo ya kusoma Computer bado kidogo yatapitwa na wakati.
Vinginevyo uisome Computer kweli kweli kwenye vyuo husika,sio hicho chuo cha wahasibu.
Na tena uchanganye na ma certification tofauti tofauti CCNA,MCSE ma A+ etc etc
Fikiri sana
Hakuna shule inayofundisha utumiaji wa simu....lakini kila mtu anatumia sio????
 
Karibu sana kwenye ulimwengu wa TEHAMA, ila usifikirie kuajiriwa halafu ukicheza utatoka kapa hata computer yako ikushinde kufungua
 
Computer science nzr mkuu na kama unaipenda usiwasikilize ndugu zko ,c.science kuna fani nyingi ndani na ukachagua wapi ujikite zaidi

Unaweza kuajiriwa kwenye makampuni,mashirika na unaweza kuanzisha kampuni yako ukiwa na wenzako,nk nk unaweza kuwa developer mzr

Kapige code mkuu utafurahi ase ,achana na mabiashara huko ,usije ukajutia mbeleni piga c.science

Kingine ushauri hapo ifm usizembee haipiti wiki 2,3 paper,presentation usikose assignment Fanya ,tutorial usikose kuhudhuria ,hicho chuo kigumu wanafuatilia sana kuwa makini ,
 
Mbona IFM imetoa watalaamu kibao, baadhi yao wameweza hadi kuhack line za wasanii. dogo usitishike sana soma unachokipenda ili upate wepesi katika kujua vitu.
 
shukhrani sana mkuu
 
Karibu sana kwenye ulimwengu wa TEHEMA, ila usifikirie kuajiriwa halafu ukicheza utatoka kapa hata computer yako ikushinde kufungua
Shukhran mkuu ndo naingia hivyo kwenye ulimwengu wa tehama,Mungu anifanyie wepesi
 
Ahsante sana kwa ushauri mkuu,nivyema nisome kitu nitakachokiweza,kuliko kulazimisha na mwisho wa siku nije kudisco na kuanza kujilaumu nafsini mwangu
 
Kikubwa sio kuwasiliza wazazi au ndugu!
Lakini je, utaweza kuondoka home baada ya kumaliza chuo? Unaweza ukawabishia wakakuacha ila nao wakasubiri umalize chuo.....hapo ndio mziki huwa unaanza!Tulikwambia sasa unaona!!Ko jiandae kisaikolojia siku wakikuona upo tu home
 
Mbona IFM imetoa watalaamu kibao, baadhi yao wameweza hadi kuhack line za wasanii. dogo usitishike sana soma unachokipenda ili upate wepesi katika kujua vitu.

Hopefully unamlenga mleta mada,vinginevyo mie ni babu yenu..ikiwa na maana wanawake wenye umri kama bibi aliye mzaa baba yako walikuwa mademu zangu miaka hiyooo.
 
dogo = huyo first year wa IFM, hahahhahahahhah sawa mkuuu
 
Computer Science ilikuwa deal sana kwenye miaka ya 2008 hadi 2013 huku tuendako watu wanaosoma Computer Science wanazidi kuongezeka na Vyuo vinavyotoa hiyo kozi vinaongezeka zaidi kila kukicha, Tanzania tuna wasomi wengi wa Computer Science lakini wenye utaalamu wa Computer Science ni wachache sana, Wengi wanatoka Vyuoni hawana kitu specific ambazo wanaweza kuajiriwa wakawa competent, ni kudonoa donoa tu ukimuuliza mtu anakwambia najua Networking kidogo, Code kidogo, Database kidogo hili ndo tatizo.

Ushauri wangu kwako, kwanza ni wewe mwenyewe JE UNAPENDA kusomea Computer Science? una brain za kusoma Computer science? mana inahitaji akili za kudadisi dadisi, kutumia akili yako sana especially kwenye Programming inahitaji uvumilivu na moyo wa kutokata tamaa. Programming inawashinda wengi kwakuwa inahitaji kutokata tamaa.

Kama una interest na Computer basi nenda kasome, ni kozi ambayo hutohitaji kuajiriwa kama utakuwa umeiva, ni kozi ambayo kwenye kujiajiri hutohitaji MTAJI wowote zaidi ya laptop yako.

Computer Science kwa Tanzania bado ina upungufu wa WANAOJUA VITU ila wenye vyeti wako wengi sana.

NB: Nimegraduate Computer Science UDSM miaka MITATU iliyopita, hope utaokota kitu kwenye huo ushauri wangu.
 
Ukisikiliza ndugu hutofanikiwa.

Hapo ukute wanakwambia ukasome sheria au education.

Hiyo inalipa.
 
Kweli kabisa mkuu ndio maana namuomba mungu anifanyie wepesi maana meng nitaanza kutana nayo na mengine yanaweza nivunja moyo kabisa
 
you are wrong my friend ....this is a wrong turn ....wrong way .....U turn make another decision
 
Ninaipenda computer science,na naamini nikiisoma nitakuwa happy,confortable and comptent,nashukuru sana mkuu
 
Computer science dah, mi ningekuwa wewe ningesoma hiyo but ningebase sanaaa kwenye multimedia haswa graphics design if and only if unataka kujiajiri.
 
Kweli kabisa mkuu ndio maana namuomba mungu anifanyie wepesi maana meng nitaanza kutana nayo na mengine yanaweza nivunja moyo kabisa
Kikubwa dogo jiamini ukienda chuo kasome sana! Ukisoma kitabu kinaitwa Think big and grow rich kuna kitu anazungumza kuhusu quality and quantity! Saivi kuna wahitimu wengi(quantity) wasio na ubora ,ila kuna wahitimu wachache waliobora!Nenda kakomae ,soma vizuri....
Ila ukicheza ujaze makarai kwenye cheti......utakuja kuwaumiza sana hao ndugu zako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…