COMPUTER MPYA

TEK

Senior Member
Jul 13, 2015
184
34
Heshima kwenu wanajamvi!

Samahani ndugu zangu, nipo kwenye mchakato wa kununua PC kwaajili ya matumizi yangu ya kimawasiliano na mengine yanayoweza kufanywa electronically lakini kabla sijaenda dukani naomba ushauri wenu katika mambo haya yanayoweza kunisaidia kutafuta bidhaa bora zaidi:-

Ni kampuni gani PC zake ni nzuri au bora kati ya haya au lingine DELL, APPLE, SAMSUNG, LENOVO?

Ni PC ya aina gani inauwezo mkubwa kwa kuzingatia RAM, GB nk?

Naomba pia ushauri wako wa kitaalam ambao utanisaidia kupata kilichobora zaidi
 
kama pesa ya kununulia Apple unayo usihangaike na hizo zingine nunua Apple tu ila ikishindikana chukua Dell au Hp
 
unapo enda dukan kununua pc usiangaike sana kuhusu RAM au HARD DISK kwa sababu hivyo unaweza kubadilisha mwenyewe hadi kiwango unacho taka .unatakiwa kuangalia hiyo pc ina kiwango gan cha processor eg.core i3,core i5,core i7. hayo ndio mambo ya kuzingatia
 
Back
Top Bottom