Compassion: Somo maalumu la kuwa na Huruma

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Posts
36,440
Reaction score
110,076
6be86cef148e60d3b850837fce5e0786.jpg

Habari
Binaadamu tumeumbwa tukiwa ana kitu ndani yetu Kinachitwa Huruma tunapozaliwa jinsi tunavyoendelea kukua ndio huruma hiyo inazidi kupungua au kuzidi kuimarika kutokana na mazingira tunayoishi. hua tunasikia huruma pindi tunapoona familia zetu, marafiki wanapokua katika mawazo na mateso mbalimbali ya dunia, lakini pia hata wanyama hua wanaona huruma wakiona watoto wao wakiwa katika maumivu. Huruma ni mbegu ya Mungu (kwani yeye ni Mwingi wa Huruma na rehema) kama twahitaji kua wana wa Mungu hakuna budi kuikuza na kuimarisha mbegu hii ya huruma ya Mungu.

Huruma ni akili ambayo inatengenezwa na kuwajali wengine pia kuwatakia viumbe hai vyote mema. Muda mwingine kutokana na ubinafsi hua tunawatakia mema na kuwaonea huruma watu ambao tunawafahamu au tunahusiana na, mfano pindi rafiki au ndugu anapoka kwenye mawazo au magonjwa hua tunamtakia heri apone haraka ili tuweze kuendelea kufurahia uwepo wake tena. Sio huruma ya kweli inayotakiwa , huruma ya kweli ni kuwaonea huruma viumbe hai vyotee bila kujali ni Fulani namfahamu,ni ndugu yangu,nakadharika.
Watu wengi hua tunawaonea huruma watu amabao tunawafahamu tu lakini tunasahau kuwaonea huruma hata wale ambao hatuwafahamu wala hawapo kwenye mazingira yetu lakini baya zaidi hua tunawaonea huruma wale watu ambao wapo kwenye maumivu makali mfano magonjwa, Umaskini, nk tunasahau kuwaonea huruma pia hata wale ambao wana maishha mazuri. Inatakiwa tuwe na upendo kama wa mama zetu, mama zetuu huwaonea huruma watoto wote bila kujali mtoto Fulani ana afya na hali nzuri na huyu ana afya na hali mbya.

Tufanyaje ili kukuza na kuendeleza huruma yetu….?
Kuna hatua mbili amabazo zitatuwezesha kuipata Huruma kuu, Kwanza kabisa tunatakiwa tuwapende viumbe hai wote pia inatakiwa tuwasaidie katika mateso na matatizo yao. Kama hatutampenda mtu Fulani hatuwezi kumuonea huruma hata kama yupo katika maumivu makubwa, hii ndio sababu inayofanya kuwaonea huruma rafiki na ndugu zetu pekee lakini sio kwa wale tusio wapenda. Kuwajali wengine ndio msingii mkuu a kukuza huruma, hivyo basi inatakiwa tutengeneze akili zetuziweze kuwaone huruma na kuwajali wengine walioko kwenye matatizo.
Kwa kuanza, tunaweza kuwafikiria wale wote ambao wapo katika maumivu na mateso makubwa muda huu unaposoma andiko hilo, kuna watu wengi wapo katika mateso makubwa ya kimwili na kiakili mfano UKIMWI, cancer, nk. Waza ni watu wangapi wamepoteza wanao wapendwa, ndugu,jamaa kwa ugonjwa wa ukimwi, unamuona mwanao anadhoofu na kudhoofu kwa gonjwa la ukimwi na ukijua kabisa halina dawa…. Kila siku maelfu ya watu wanafariki kwa ajali au magonjwa bila wao kupenda wanatenganishwa milele na ndugu zao.. hebu fikiri bibi kizee anampoteza muwe mpenzi aliyeishi nae miaka mingi anabaki pekee yake katika ukiwa na upweke.
Watu wanakufa kwa njaa, mafuriko, mauaji,vita, matetemeko ya ardhi wengine wanabaki na ukame na njaa, umaskini bila makazi. Hebu fikiri hivi utajisikiaje kama haya yakatokea kwetu?
Pia inatakiwa tuwafikirie na wanyama wa porini amabao wanateseka kutwa kucha kwa baridi,joto,njaa, ukame na kiu. Kila siku tunaona mateso ya wanyama, wanyama wa porini wapo katika uoga wa hatari ya kuliwa na wanyama wanokula nyama, hebu fikiria ni maumivu gani anayoyapata kifaranga naponyakuliwa na mwewe au kuku kisu kinapopita shingoni mwake..wanyama wengine wamefugwa na wanadamu kwa kufanyishwa kazi,kwa chakula,kwa burudani na ulinzi. Unafikiria huwa wanajisikia vipi wanyama hao??
Lakini pia tukumbuke pia hata wale ambao hawapo kwenye mateso na maumivu makubwa muda huu na wanapata maumivu ya namna nyngine. Kila mwanadamu ana mateso ya kutotimiza matakwa/haja zao, watu wengi imewawea vigumu kutimiza hata mahitaji ya kawaida kama vile chakula, mavazi na malazi lakini hata kama matakwa yao yakitimia inatakiwa bado tuwaonee huruma maana jinsi tunavyopata yale tunayoyahitaji ndio matatizo yanazidi kuongezeka, na jinsi matatizo yanavyozidi kuongezeka ndio mtu inamuwea vigumu kuridhika. Hakuan mtu wa kawaida duniani ambaye kayatimiza matakwa yake…ni wale tu ambao wameweza kuvuka/kuondoa nafsi ya ubinafsii akilini mwao.
8e5ac04a67d55b20e3fb74d796d09047.jpg

Mateso yote ni matokeo hasi ya yale mabaya tuliyofanya, kama tutakua na huruma kwa wale wanaoteseka kutokana na mabaya waliyofanya kwanini tusiwaonee huruma pia wale wanaofanya mabaya (dhambi) ambapo watapata mateso baadae (motoni)? Maana mateso watakayoyapata baadae yatakuwa makubwa na mabaya kuliko ya mabaya aliyomfanyia mtu Fulani. Kama mtu aliyefanyiwa mabaya atayapokea maumivu bila chuki na kumuonea huruma yul aliyemfanyia atakua kamsaidia kutopata mateso baadae. Kwa sababu hii inatupasa kuwaonea huruma na kuwasamehe wale wote waliotutenda vibaya ili wasije kupata mateso na wao baadae, Kama mtoto kajiunguza mkono wake kwa kuushika moto hii haimzuii mama yake kumuonea huruma hata kama mtoto alikua kashatahadharishwa muda mrefu . hivyo basi tuwe na upendo na huruma kama mama zetu, hakuna kiumbe hata kimoja ambacho hakistahili huruma yetu.
Inatakiwa pia tuwaonee huruma matajiri, wenye afya njema , wanaoheshimiwa na wale wanaonekana hawana mateso, kiuhalisia hata wao wanapata maumivu ya kiakili. Wanawaza pesa zao, wanahofia usala wao, wanateseka na hasira nk.

Tupendane, Tujaliane na kutakiana mema bila ubaguzi.
Mwisho.

~Da’vinci..
 
Hii ya kuwaonea 'huruma matajiri, wenye afya njema , wanaoheshimiwa na wale wanaonekana hawana mateso" mimi naona itakuwa matumizi mabaya ya huruma!
 
Amri kuu ya Mungu ni upendo kwa wote

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
 
Mbona chama tawala hakionei upinzani huruma kila wakishinda wanageuza jamvi

USA strong nation na wachina wanaendelea kutunyonya bila huruma

Mabeberu kila uchwao wanatutisha bila huruma.

Mimi ni nani hata niwe na huruma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe unaonekana ni mtu unaependa visasi sana 99.9% unafanania na mzee wa magogoni
 
Mbona chama tawala hakionei upinzani huruma kila wakishinda wanageuza jamvi

USA strong nation na wachina wanaendelea kutunyonya bila huruma

Mabeberu kila uchwao wanatutisha bila huruma.

Mimi ni nani hata niwe na huruma.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huruma haipo kwenye chama ipo kwa watu...

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
 
ed322a0c19635b5dac8366751b16c394.jpg

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
 
6be86cef148e60d3b850837fce5e0786.jpg

Habari
Binaadamu tumeumbwa tukiwa ana kitu ndani yetu Kinachitwa Huruma tunapozaliwa jinsi tunavyoendelea kukua ndio huruma hiyo inazidi kupungua au kuzidi kuimarika kutokana na mazingira tunayoishi. hua tunasikia huruma pindi tunapoona familia zetu, marafiki wanapokua katika mawazo na mateso mbalimbali ya dunia, lakini pia hata wanyama hua wanaona huruma wakiona watoto wao wakiwa katika maumivu. Huruma ni mbegu ya Mungu (kwani yeye ni Mwingi wa Huruma na rehema) kama twahitaji kua wana wa Mungu hakuna budi kuikuza na kuimarisha mbegu hii ya huruma ya Mungu.

Huruma ni akili ambayo inatengenezwa na kuwajali wengine pia kuwatakia viumbe hai vyote mema. Muda mwingine kutokana na ubinafsi hua tunawatakia mema na kuwaonea huruma watu ambao tunawafahamu au tunahusiana na, mfano pindi rafiki au ndugu anapoka kwenye mawazo au magonjwa hua tunamtakia heri apone haraka ili tuweze kuendelea kufurahia uwepo wake tena. Sio huruma ya kweli inayotakiwa , huruma ya kweli ni kuwaonea huruma viumbe hai vyotee bila kujali ni Fulani namfahamu,ni ndugu yangu,nakadharika.
Watu wengi hua tunawaonea huruma watu amabao tunawafahamu tu lakini tunasahau kuwaonea huruma hata wale ambao hatuwafahamu wala hawapo kwenye mazingira yetu lakini baya zaidi hua tunawaonea huruma wale watu ambao wapo kwenye maumivu makali mfano magonjwa, Umaskini, nk tunasahau kuwaonea huruma pia hata wale ambao wana maishha mazuri. Inatakiwa tuwe na upendo kama wa mama zetu, mama zetuu huwaonea huruma watoto wote bila kujali mtoto Fulani ana afya na hali nzuri na huyu ana afya na hali mbya.

Tufanyaje ili kukuza na kuendeleza huruma yetu….?
Kuna hatua mbili amabazo zitatuwezesha kuipata Huruma kuu, Kwanza kabisa tunatakiwa tuwapende viumbe hai wote pia inatakiwa tuwasaidie katika mateso na matatizo yao. Kama hatutampenda mtu Fulani hatuwezi kumuonea huruma hata kama yupo katika maumivu makubwa, hii ndio sababu inayofanya kuwaonea huruma rafiki na ndugu zetu pekee lakini sio kwa wale tusio wapenda. Kuwajali wengine ndio msingii mkuu a kukuza huruma, hivyo basi inatakiwa tutengeneze akili zetuziweze kuwaone huruma na kuwajali wengine walioko kwenye matatizo.
Kwa kuanza, tunaweza kuwafikiria wale wote ambao wapo katika maumivu na mateso makubwa muda huu unaposoma andiko hilo, kuna watu wengi wapo katika mateso makubwa ya kimwili na kiakili mfano UKIMWI, cancer, nk. Waza ni watu wangapi wamepoteza wanao wapendwa, ndugu,jamaa kwa ugonjwa wa ukimwi, unamuona mwanao anadhoofu na kudhoofu kwa gonjwa la ukimwi na ukijua kabisa halina dawa…. Kila siku maelfu ya watu wanafariki kwa ajali au magonjwa bila wao kupenda wanatenganishwa milele na ndugu zao.. hebu fikiri bibi kizee anampoteza muwe mpenzi aliyeishi nae miaka mingi anabaki pekee yake katika ukiwa na upweke.
Watu wanakufa kwa njaa, mafuriko, mauaji,vita, matetemeko ya ardhi wengine wanabaki na ukame na njaa, umaskini bila makazi. Hebu fikiri hivi utajisikiaje kama haya yakatokea kwetu?
Pia inatakiwa tuwafikirie na wanyama wa porini amabao wanateseka kutwa kucha kwa baridi,joto,njaa, ukame na kiu. Kila siku tunaona mateso ya wanyama, wanyama wa porini wapo katika uoga wa hatari ya kuliwa na wanyama wanokula nyama, hebu fikiria ni maumivu gani anayoyapata kifaranga naponyakuliwa na mwewe au kuku kisu kinapopita shingoni mwake..wanyama wengine wamefugwa na wanadamu kwa kufanyishwa kazi,kwa chakula,kwa burudani na ulinzi. Unafikiria huwa wanajisikia vipi wanyama hao??
Lakini pia tukumbuke pia hata wale ambao hawapo kwenye mateso na maumivu makubwa muda huu na wanapata maumivu ya namna nyngine. Kila mwanadamu ana mateso ya kutotimiza matakwa/haja zao, watu wengi imewawea vigumu kutimiza hata mahitaji ya kawaida kama vile chakula, mavazi na malazi lakini hata kama matakwa yao yakitimia inatakiwa bado tuwaonee huruma maana jinsi tunavyopata yale tunayoyahitaji ndio matatizo yanazidi kuongezeka, na jinsi matatizo yanavyozidi kuongezeka ndio mtu inamuwea vigumu kuridhika. Hakuan mtu wa kawaida duniani ambaye kayatimiza matakwa yake…ni wale tu ambao wameweza kuvuka/kuondoa nafsi ya ubinafsii akilini mwao.
8e5ac04a67d55b20e3fb74d796d09047.jpg

Mateso yote ni matokeo hasi ya yale mabaya tuliyofanya, kama tutakua na huruma kwa wale wanaoteseka kutokana na mabaya waliyofanya kwanini tusiwaonee huruma pia wale wanaofanya mabaya (dhambi) ambapo watapata mateso baadae (motoni)? Maana mateso watakayoyapata baadae yatakuwa makubwa na mabaya kuliko ya mabaya aliyomfanyia mtu Fulani. Kama mtu aliyefanyiwa mabaya atayapokea maumivu bila chuki na kumuonea huruma yul aliyemfanyia atakua kamsaidia kutopata mateso baadae. Kwa sababu hii inatupasa kuwaonea huruma na kuwasamehe wale wote waliotutenda vibaya ili wasije kupata mateso na wao baadae, Kama mtoto kajiunguza mkono wake kwa kuushika moto hii haimzuii mama yake kumuonea huruma hata kama mtoto alikua kashatahadharishwa muda mrefu . hivyo basi tuwe na upendo na huruma kama mama zetu, hakuna kiumbe hata kimoja ambacho hakistahili huruma yetu.
Inatakiwa pia tuwaonee huruma matajiri, wenye afya njema , wanaoheshimiwa na wale wanaonekana hawana mateso, kiuhalisia hata wao wanapata maumivu ya kiakili. Wanawaza pesa zao, wanahofia usala wao, wanateseka na hasira nk.

Tupendane, Tujaliane na kutakiana mema bila ubaguzi.
Mwisho.

~Da’vinci..

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
Broo nw day sikupat kabisa kwa simu yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa meza ya jirani jamaa anatia huruma ngoja nimuagizie vodka akate kiu
 
Back
Top Bottom