Communism & Capitalism: Matokeo The World na Tanzania

Mimi ninafikiri kuwa mjadala kama huu ni muhimu sana hasa kwa sisi wachangiaji humu kukwaani. Tukiweza kuelewa na kujieleza (kwa kadri ya uwezo wa mtu binafsi) itasaidia ku-reshape thinking capacity zetu na jinsi ya kujitofautisha na wengine. Kuna mchangiaji ametoa rai kuwa watu warudi wakasome kitabu/vitabu nadhani yuko sahihi, lakini pia akumbuke mada hii inajadilika kwa vile wengi tumesoma habari za Capitalism na Communism kwa miongo kadhaa tangu tukiwa shule za msingi na hata vyuoni, kwahiyo basi ni wakati mwafaka wa kuchangia, kama mtu anaona anahitaji kupata recharge ya kuchangia anaweza kurudi kwenye vitabu na halafu akaendelea kuchangia.

Mtazamo wangu juu ya mada:

Bara la Ulaya kwa muda wa karne kadhaa lilikuwa lilitawaliwa na watawala waliokuwa wanaamini katika sera za kuongeza himaya za utawala wao. Hii hali ilizifanya tawala nyingi kutumia nguvu na vitisho ili kutimiza matakwa yao. Ukandamiza, vita vya wenyewe kwa wenyewe ilikuwa ndiyo mazungumzo ya kila siku. Mienendo hiyo ndiyo iliyowezesha kuzaliwa utawala makeke kabisa wa kijerumani. Historia inatuonyesha kuwa utawala wa wajerumani ulikuwa ni utawala wenye nguvu sana na uliweza kuabudiwa na tawala nyingine kama vile Russia na France achilia mbali nchi nyingine ndogondogo. Ujerumani ilikuwa na sauti kubwa ndani ya ulaya na iliweza kuwa na nguvu kubwa ya maamuzi dhidi ya utawala wa Austro-Hungary, ambalo lilikuwa ni eneo muhimu katika mipangilio ya kutwaa himaya zingine za ulaya.
Ujerumani iliweza kutwaa na kushikilia baadhi ya maeneo ya Russia baada ya vita kati ya nchi hizo mbili. Hali kadhalika, Ujerumani iliivamia Ufaransa na kuishinda vitani na kuchukua maeneo ya Ufaransa. Kuendelea kukua kwa Ujerumani kieneo kulileta wasiwasi mkubwa miongoni mwa mataifa mengi ikiwemo hata Uingereza. Nchi kadhaa ziliwekeana mikataba ya kusaidiana kivita endapo Ujerumani itaishambulia moja kati ya nchi zao, mojawapo ya mikataba hiyo ilikuwa ni mkataba kati ya Uingereza na Ufaransa. Ufaransa kijiografia ikiwa imebanwa na Ujerumani ilikuwa haina uwezo wa kujiongezea himaya ndani ya Ulaya na badala yake ndiyo iliyotoa ushawishi mkubwa kwa nchi za ulaya kujigawia maeneo mbalimbali dunia na kuyageuza kuwa makoloni yao.
Kwa upande mwingine, kama ilivyokuwa Ujerumani, Japan nayo ilikuwa ni tishio jingine kwa upande wa bara la Asia. Wajapani waliweza kutwaa maeneo mengi kama vile China, Korea na maeneo mengine ya Asia pamoja na baadhi ya maeneo ya Russia. Utawala wa Kijapani ulikuwa ni utawala wakikatili na uliogopewa sana. Wajapani walikuwa na silaha na jeshi kubwa ambalo liliweza kupigana vita zaidi ya moja kwa wakati mmoja.

Nini Kilitokea baada ya ubabe wa Wajerumani na Wajapani?

Kuendelea kukua kwa makeke (aggressiveness) ya wajerumani, kulihatarisha sana usalama wa Ufaransa. Ufaransa iliona kuwa bila ujerumani kupunguzwa nguvu basi taifa la ufaransa halitaweza kuwepo siku za usoni. Baadhi ya wachunguzi wa mambo wanadai kuwa mauaji ya mtawala wa Astro-Hungary (mshirika mkuu wa ujerumani) yalipangwa kama njia ya kuitingisha ujerumani. Matokeo yake ilikuwa ni Ujerumani kutangaza vita dhidi ya Poland, Russia na Ufaransa na hatimaye kuwa vita kuu ya kwanza ya dunia. Baada ya ujerumani kushindwa vita ile ya kwanza, mataifa kama Ufaransa na Russia yalitumia mwanya huo kujiimarisha kijeshi dhidi ya udhalimu mwingine wowote wa Ujerumani hapo baadae.

Wajapani ambao walikuwa na nguvu sana walisalimu amri baada ya kushambuliwa kwa mabomu ya atomic miji yake ya Hiroshima na Nagasaki. Maamuzi ya kuishambulia Japan kwa mabomu ya atomic yalitokana na kushambuliwa kwa Marekani pale Pearl Harbor.

Kwanini ukoministi ulianza kukua?

Kimsingi baada ya vita kuu ya kwanza ambayo Wamarekani waliisadia ulaya dhidi ya wajerumani, Wamarekani waliitaka Ulaya ibadilike kutoka katika mifumo ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, ukandamizaji, expansionist na badala yake ijikite katika utawala wa kikapitalist, kidemorasia zaidi na uhuru wa kibiashara (free economy). Pia Wamarekani walipendekeza kuundwa kwa mataifa huru kwa maana ya nchi za ulaya ziachilie makoloni yao yajitawale yenyewe. Ushawishi wa Marekani uliweza kuyafanya mataifa mengi ya ulaya hasa magharibi kuchukua sera za kikapitalist na hivyo kujenga upande uliokuwa na nguvu nyingi sana za kiuchumi na kijeshi. Russia ilitumia mwanya huu wa kushindwa kwa ujerumani kujiimarisha kijeshi huku ikisaidiwa na Marekani. Russia kwa vile ilikuwa nyuma kimaendeleo ukilinganisha na nchi nyingine kama vile Uingereza, Ujerumani na Ufaransa, iliamua kufanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kijamii ikiwemo kushikilia uchumi mikononi mwa serikali. Malengo makubwa ya kufanya hivyo ilikuwa ni kuwalazimisha wananchi wa Russia wautumikie utawala wao 100%. Uzalishaji wowote ule wa mtu binafsi au kikundi ulimilikiwa na serikali. Serikali iliweza kujilimbikizia na kumiliki mali zilizozalishwa na wananchi bila ya hiyari zao. Baada ya Russia kuimarika na kufuatia mapinduzi makubwa ya akina Lennin na Stalin, Russia iliamua kurudi katika sera za expansionist ambazo zilikuwa zinapigwa vita barani ulaya. Ilikuendelea kushikilia sera hizo Russia ilibidi kutafuta washirika na kuungwa mkono, mshirika wake wa kwanza akiwa ni China ambaye alinyanyaswa sana na Japan kama alivyokuwa Russia dhidi ya Ujerumani. Malengo ya Russia na China ya kukuza ukominist ilikuwa ni njia ya kuwasaidia kujijenga na kuepuka kushambuliwa na kufanywa wanyonge na mataifa makubwa.
Kama vile ambavyo Marekani ilivyokuwa inasambaza ukapitalist kwa nia ya free economy, Warusi walieneza ukomunist ili wajilinde.

Kwahiyo mimi ninaona sera za kikomunist ni sera ambazo zilikuwepo kwa wakati ule kwa malengo maalum na ndiyo maana leo hii Warusi na Wachina wanaachana nazo kwa vile sababu zilizokuwepo wakati ule hazipo tena. Lakini sera za ukapitalist ndiyo zinaonekana kuwa ndiyo sera sahihi zinazoweza kuleta mabadiliko ya kweli kutoka kwa mtu mmoja mmoja.

Nikirudi hapa Tanzania, Tanzania ilijikuta inapata uhuru wakati mivutano hii miwili ikiwa katika nguvu kubwa. Na ukifuatilia historia ya kupata uhuru kwa nchi nyingi hasa Afrika ni kwamba watawala walikuwa wanatafuta warithi ambao watakuja kuwa viongozi wa nchi zinazopewa uhuru. Kwa mfano makoloni ya mfaransa, wengi waliokuja kuwa viongozi wa nchi hizo walikuwa na mahusiano ya karibu au moja kwa moja na watawala wa kifaransa. Kwa hiyo basi wale ring leaders wa ukomunist waliweza kupandikiza na wenyewe propaganda kwa mataifa haya machanga ikiwemo Tanzania ili waweze kutengeneza block kwa malengo na faida ya Russia na China. Ninakumbuka wakati Tanzania inasherehekea miaka 10 ya Uhuru wa Tanganyika, serikali ya China ilijihusisha kwa gharama kubwa katika kusaidia sherehe zile. China ilikuwa ni recruiter wetu wa kuhakikisha tunaungana nao.
Kimsingi mwisho vita baridi kati ya Marekani na Urusi ndiyo iliyohitimisha ukomunist.
Kwa mtazamo wangu, Tanzania sasa hivi inapaswa kutamka kuwa sera za ujamaa zimeachwa na badala yake tutaendelea na hii ya kujitegemea (Ukapitalist).
 
wakati tunaendelea kuangaika na kujadili issues ambazo ni black and white, wenzetu huko wanatuachia mashimo matupu, wanachukua ardhi kulima mazao yenye faida kwao, wageni wanalilia kuja tanzania kuchukua hivyo hivyo vi nafasi vya mate vinavyotokea kwenye makazi, roho mbaya kwenye mashirika ya umma ndio vile vile.

You have to ask sometimes even if we knew what was best for us, are we really the type to implement changes.

All in all serikali inatupa hela ovyo, watanznaia ni maskini wizi ni wa wazi embu tujiulize hile stimuls package ili stimulate kitu gani. Au ni watu gani waliitumia utagundua dolla karibu millioni 200 tayari zimeshaenda kwenye mifuko ya watu tayari.

Jamani watanznaia tuna utani mmbaya nyie, alafu tunajiita great thinkers wakati tunaibiwa mchana.
 
- Communism na Capitalism maana yake ni nini hasa? zilifanikiwa au zili-fail? Nani walioanzisha na kwa nini? zilianzia wapi na lini? Nini matokeo yake kwa Dunia na hasa sisi Tanzania? Tanzania ya leo tunafuata Communism au Capitalism? Na ikibidi tufuate ideology ipi kati ya hizo mbili kwa ajili ya manufaa yetu? Do we need any of this ideologies? Tujadili wakuu!

Ahsanteni.

William.

"Less than seventy-five years after it officially began, the contest between capitalism and communism is over: capitalism has won." ( Robert L. Heilbroner 1989).

Free Market ndiyo solution ya matatizo tuliyokuwa nayo TZ.
 
- Communism na Capitalism maana yake ni nini hasa? zilifanikiwa au zili-fail? Nani walioanzisha na kwa nini? zilianzia wapi na lini? Nini matokeo yake kwa Dunia na hasa sisi Tanzania? Tanzania ya leo tunafuata Communism au Capitalism? Na ikibidi tufuate ideology ipi kati ya hizo mbili kwa ajili ya manufaa yetu? Do we need any of this ideologies? Tujadili wakuu!

Ahsanteni.

William.

Tatizo kubwa la Capitalism system ni kwamba lazima viongozi ktk private sectors lazima wawe honest. Tatizo kubwa la TZ ni Ufisadi, ktk private sectors and government. Angalia USA inaanza kushindwa na Capitalism kwa sababu Ufisadi umeshaingia ndani ya private sectors. Sisi (TZ)tuna kazi ndefu na Ufisadi.
 
- Communism na Capitalism maana yake ni nini hasa? zilifanikiwa au zili-fail? Nani walioanzisha na kwa nini? zilianzia wapi na lini? Nini matokeo yake kwa Dunia na hasa sisi Tanzania? Tanzania ya leo tunafuata Communism au Capitalism? Na ikibidi tufuate ideology ipi kati ya hizo mbili kwa ajili ya manufaa yetu? Do we need any of this ideologies? Tujadili wakuu!

Ahsanteni.

William.


William na wakuu wengine:

Nashukuru kwa kuibua mjadala huu kuhusu itikadi. Mwaka 2007, niliwahi kuweka katika makala mawazo yangu kuhusu suala hili; naamini makala zile tatu zinaweza kuwa food for thought wakati mnaendelea na mjadala huu.

Makala ya Kwanza: http://www.chadema.or.tz/makala/makala.php?id=49

Makala ya Pili: http://www.chadema.or.tz/makala/makala.php?id=50

Makala ya Tatu: http://www.chadema.or.tz/makala/makala.php?id=51

Mjadala mwema

JJ
 
William na wakuu wengine:

Nashukuru kwa kuibua mjadala huu kuhusu itikadi. Mwaka 2007, niliwahi kuweka katika makala mawazo yangu kuhusu suala hili; naamini makala zile tatu zinaweza kuwa food for thought wakati mnaendelea na mjadala huu.

Makala ya Kwanza: http://www.chadema.or.tz/makala/makala.php?id=49

Makala ya Pili: http://www.chadema.or.tz/makala/makala.php?id=50

Makala ya Tatu: http://www.chadema.or.tz/makala/makala.php?id=51

Mjadala mwema

JJ


Ndugu Mnyika:

Nimesoma makala yako. Na unasema CHADEMA ni mlengo wa kati lakini sikuona cha maana cha kuonyesha kuwa CHADEMA ni chama cha mlengo wa kati, zaidi ya kutoa historia tu.

Hata sera za CCM zilizopo sasa ni za mlengo wa kati, hivyo tafaouti zenu ni majina na bendara.
 
William na wakuu wengine:

Nashukuru kwa kuibua mjadala huu kuhusu itikadi. Mwaka 2007, niliwahi kuweka katika makala mawazo yangu kuhusu suala hili; naamini makala zile tatu zinaweza kuwa food for thought wakati mnaendelea na mjadala huu.

Makala ya Kwanza: http://www.chadema.or.tz/makala/makala.php?id=49

Makala ya Pili: http://www.chadema.or.tz/makala/makala.php?id=50

Makala ya Tatu: http://www.chadema.or.tz/makala/makala.php?id=51

Mjadala mwema

JJ

John,

What we need here ni mawazo yako wewe kama John na mwananchi wa kawaida. Sasa ukianza kuleta mawazo ambayo unawakilisha mtazamo wa chama chako huwezi kuwa mchangaji huru katika thread hii. Let's discuss hili swala kutoka katika kiini chake bila ya kuleta itikadi za vyama vyenu. I would prefer this thread to be very educational na si ushabiki.
 
Tanzania, CHADEMA, CCM na mjadala wa falsafa na itikadi, Lipi ni jibu?
na


John John Mnyika
Mkurugenzi wa Mambo ya Nje


Mjadala kuhusu falsafa na itikadi umeibuka tena rasmi. Nimesoma mahojiano ya mwanasiasa kijana David Kafulila akizungumzia CHADEMA ni Msingi na makala ya mchambuzi mahiri aliyoyapa kichwa “Itikadi ya Mrengo wa Kati si jibu. Nimesoma pia makala ya Mwenyekiti wangu-Freeman Mbowe kuhusu suala hili. Ni dhahiri mjadala umefumuka rasmi. Suala la falsafa na itikadi si la wanasiasa na vyama tu, ni suala la kitaifa; tulijadili. Katika makala yake Prince Bagenda kimsingi, amebeza itikadi ya mrengo wa kati. Si lengo la sehemu hii ya kwanza kujibu hoja kwa hoja uchambuzi wa Bagenda kuhusu mrengo wa kati. Lengo la makala ya leo ni kueleza ni nini hasa itikadi ya mrengo wa kati. Katika makala yake Freeman Mbowe amebainisha hoja mbili kubwa- Mosi, kwamba CCM haifuati siasa ya Ujamaa na Kujitegemea kwa vitendo kama inavyotangaza kwa maneno na nyaraka zake (kwa maneno mengine CCM inakiuka katiba ya nchi). Pili; kwamba kitendo cha serikali ya CCM kuweka kwenye katiba ya nchi kwamba Tanzania ni nchi ya itikadi ya siasa na ujamaa na kujitegemea ni kinyume na dhana ya demokrasia ya vyama vingi ambayo inataka uhuru wa fikra na kiitikadi. Nitachangia kwa kiasi hoja hizi (kwa maana nyingine vyama vyenye itikadi tofauti na ujamaa na kujitegemea vinakiuka katiba ya nchi). Nitajadili!

Kwa tafsiri rahisi, falsafa ni fikra na mtazamo wakati itikadi ni imani. Maneno haya mawili ni muhimu sana katika medani ya siasa na maendeleo kwa ujumla. Nimewahi kupitia katiba za vyama mbalimbali vya siasa nchini, nimewahi kupitia Azimio la Arusha, nimewahi kusoma maamuzi ya Zanzibar (ambayo wengi huyaita Azimio la Arusha) na ninayo kama rejea ya msingi Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ukipitia nyaraka zote hizi utaona kwamba mjadala kuhusu falsafa na itikadi ni suala lisiloepukika.

Mwaka 1991 Mwenyekiti wa CCM wa wakati huo, Ali Hassani Mwinyi wakati huo alijitokeza na kutoa hotuba ndefu akitetea maamuzi ya Zanzibar na kusisitiza kwamba CCM inafuata siasa ya ujamaa na kujitegemea, namnukuu: “ Inaelekea kuna hofu kwamba Azimio la Arusha linageuzwa. Kwa hiyo, tokea mwanzao, kabla ya kusema lolote, nataka tuelewane kwamba siasa yetu bado ni ile ile ya Ujamaa na Kujitegemea. (Makofi). Haikugeuka wala hatutazamii kuigeuza. Kwa hali yoyote sisi Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi hatutaigeuza Siasa hii. (Makofi) . Kule Zanzibar tulizungumza mambo mengi, miongoni mwao, ni kutoa tafsiri ya baadhi ya vipengele vya Azimio ili vifanane na wakati tulionao.”

Lakini miaka kadhaa baadaye, Muasisi na Mwenyekiti wa kwanza wa CCM, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitamka wazi kwamba CCM haifuati siasa ya ujamaa na kujitegemea, nikinukuu kitabu chake cha uongozi wetu na hatma ya Tanzania : Halmashauri Kuu ya Taifa iliketi Unguja ikabadili Azimio la Arusha bila kwanza kutafuta maoni ya wananchi. Na walikuwa na haki ya kufanya hivyo, maana sera ni yao, ubaya wao ni kwamba jambo lenyewe walilifanya kwa hila na hadi sasa wanaendelea kuwadanganya wananchi kwamba sera ya CCM bado ni Ujamaa na Kujitegemea.’ Haya ni maneno ya kiongozi ambaye alishiriki moja kwa moja kuandika Azimio la Arusha na misingi ya siasa ya ujamaa na kujitegemea! Mwaka 2000, mwaka mmoja tu baada ya baba wa Taifa kufariki, serikali ikapeleka bungeni mabadiliko ya Katiba na kuweka tafsiri finyu ya ujamaa na kujitegemea! Mwaka 2006, Agrey Mwanri-Mbunge wa CCM akichangia katika Bunge la Kwanza la Bajeti alijenga hoja nzito kwamba nchi hii haina itikadi, kinachoendelea hapa ni shughuli tupu. Mwaka 2007, Agrey Mwanri huyo huyo, baada ya kuteuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, alijenga hoja kinzani wakati wa kuchangia mjadala kuhusu muswada wa rushwa; kwamba nchi yetu bado inafuata siasa ya ujamaa na kujitegemea. Na kwamba bila siasa hii; mustakabali wa taifa utakuwa mashakani. Hapa ndipo tulipofika! Je, mustakabali wetu hauko shakani?

Kauli hizi zinahitaji kujadiliwa. Inaweza kuonekana hili ni suala dogo. Lakini hilo ndio chanzo ya matatizo ya watanzania. CCM inafuata sera ya Ubepari uliokubuhu na mfumo wa soko holela. Ndio maana leo wageni na wawekezaji kutoka nje wanapewa kipaumbele zaidi. Ukuaji wa uchumi unawanufaisha wachache na matabaka katika jamii yanazidi kuongezeka, Uzalishaji umepungua na tumegeuzwa wachuuzi wa bidhaa toka nje.Kwa upande mwingine mzigo wa huduma za kijamii katika sekta za elimu na afya unazidi kuwa mzigo kwa watanzania maskini.Chama tawala kinapokosa itikadi maana yake kimekosa dira. Chama kinapokosa itikadi yake hakiwezi kuandaa sera na kutoa mwelekeo wa Taifa!

Niweke pia bayana kwamba ujamaa ni neno tamu; ni tamu linapobeba dhana ya undugu na usawa. Lakini inapochukua sura ya dola kufanya uzalishaji wa moja kwa moja hapa hupoteza maana. Kujitegemea ni suala zuri. Hasa linapotekelezwa kwa vitendo bila kuegemea wahisani. Hata hivyo maneno haya yanapotumiwa hivyo sivyo na vyama visivyo na dira wala mwelekeo dhana hizi zinapoteza dhima na maana yake!

Bagenda amejenga hoja kwamba vyama vya upinzani nchini vinaiga itikadi za kimagharibi na ameshambulia moja kwa moja itikadi ya CHADEMA ya Mrengo wa kati. Anasahau kwamba CHADEMA ni chama hakijatoka nchi ya misingi yake ya asili. Wakati wa mabadiliko ya Katiba ya CHADEMA mwaka 2006, ambayo yalihusisha mchakato wa kutuma timu za kukusanya maoni ya wanachama toka ngazi ya wilaya, nilikuwa mjumbe katika kamati ya itikadi. Kamati hii iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Mwesiga Baregu-Profesa wa siasa na mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA. Kamati hii iliratibu mchakato wa kuweka bayana itikadi ya chama katika katiba. Hapo nyuma tulisema CHADEMA inaamini katika falsafa na itikadi ya nguvu na mamlaka ya umma. Sasa tumeamua kuweka bayana falsafa yetu na itikadi yetu. CHADEMA tunaendelea kuwa na falsafa ya nguvu na mamlaka ya umma. Huu ni msimamo wetu wa asili: Kwamba falsafa ya CHADEMA ni kuamini katika “nguvu na Mamlaka ya Umma”(People’s Power) katika kumiliki, kuendesha, kubuni na kuendeleza mawazo, raslimali, uchumi na siasa za nchi. Aidha, falsafa ya nguvu na mamlaka ya umma ndiyo msingi na chimbuko la kuundwa kwa dola ya nchi na kuwa umma ndio wenye madaraka ya mwanzo na mwisho katika kuamua hatma ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa au kughilibiwa na viongozi, watawala au wageni....hivyo basi, falsafa ya “nguvu na mamlaka ya Umma” ndiyo njia ya msingi ya kubadilisha fikra na uongozi unaokandamiza umma, ili kuibua fikra mpya na kuweka uongozi unaoweza kumilikiwa, kuhojiwa, na kuwajibishwa na umma kwa kutumia vyombo vinavyopatikana kwa utashi wa wengi kupitia chaguzi huru na haki. Hii ni falsafa tuliyokuwa nayo ambayo tunaiendeleza.

Kwa upande mwingine tulipitia madhumuni ya kuanzishwa kwa CHADEMA pamoja na sera za chama. Tumejitafakari kiitikadi na kuona tutamke bayana katika katiba yetu tuko wapi. Mkutano mkuu uliamua kwa kauli moja kwamba CHADEMA ni chama cha itikadi ya MRENGO WA KATI(center party). Kwangu mimi itikadi ni imani. Ni imani inayotuunganisha. Ni imani inayotuongoza. Ni imani inayotuelekeza. Ni imani tunayoielekea. Dhana ya “Mrengo wa kati” pengine itaeleweka vyema kama nitasimulia kisa cha dola moja ya kifalme kama ifuatavyo.

“Katika ufalme huo palikuwa na baraza ambalo lilikuwa na wajumbe wa makundi matatu. Kundi moja lilikuwa upande wa kulia: Hili lilikuwa ni kundi la watawala, wakati wote lilitetea utawala, nidhamu ya kijamii na maslahi ya watu binafsi. Kundi la pili lilikaa upande wa kushoto: Hili lilikuwa likitetea umuhimu wa dola kuhudumia wananchi ikiwemo umiliki wa pamoja wa njia zote za uzalishaji mali na kuweka mkazo katika haki za matabaka. Kundi la tatu lilikaa katikati: Hili lilikuwa likitetea umuhimu zaidi wa dola kuwawezesha wananchi, likiweka mkazo katika uhuru na uwezekano wa kuboresha maisha ya mwanadamu na jamii. Kundi hili la tatu ndio asili ya itikadi ya mrengo wa kati.

CHADEMA ni chama cha mrengo wa kati kwa mujibu wa madhumuni yake na sera zake. Mathalani, ukipitia madhumuni ya kiuchumi ya CHADEMA, utabaini kuwa ni chama kinachoamini kukuza na kuimarisha uchumi wa nchi kwa kutumia raslimali za nchi yetu bila kuathiri uhuru wa Taifa, na kuhakikisha kuwa umma kwa ujumla unanufaika na raslimali zao. CHADEMA inaamini katika kujenga na kuimarisha uchumi wa soko huru ama soko la kijamii, utakaoheshimu na kulinda haki na mali za watu, biashara huru na sekta ya watu binafsi bila kupoka mamlaka ya umma katika maeneo nyeti. Tunaamini katika soko huru sio soko holela. CHADEMA inaamini kuhakikisha matumizi bora ya raslimali asilia za nchi ili zichangie kikamilifu katika pato la taifa na hasa kuboresha huduma za kiuchumi zinazotumiwa na wananchi wote.

Pia CHADEMA kinayo misingi muhimu katika sera na ajenda zake inayokiweka chama katika Mrengo wa Kati. Tunaamini katika uzalendo na kuthamini mila na desturi zetu zilizo nzuri. Tunaamini katika uhuru chini ya sheria zilizo nzuri. Tunaamini katika siasa ambazo ziko juu ya vyama zenye kusimamia zaidi maslahi ya Taifa. Tunaamini katika umuhimu wa dini katika kujenga maadili ya mwanajamii mmoja mmoja bila kuifanya dini kuwa sehemu ya dola. Tunaamini taifa linaundwa na watu, hivyo uhai wake unawategemea watu, na mabadiliko yake yanatokana na watu. Tunaamini kumiliki raslimali na mali miongoni mwa wananchi kunawapa uhuru zaidi hivyo tunataka kujenga chama na baadaye taifa lenye kutoa fursa, ambapo kila mtu bila kujali asili na hali yake anaweza kutimiza na kufanikiwa kadiri ya vipaji vyake. Hizi ni baadhi tu ya sababu zinazofanya CHADEMA kuwa chama cha mrengo wa kati.

Hatahivyo, hatuamini kwamba itikadi ni suluhisho pekee la matatizo katika taifa. Tutaendelea na utamaduni wetu wa kuwa na itikadi laini (relaxed ideology) badala ya itikadi iliyojibana (restrictive ideology). Tutaendelea na msimamo wetu wa kutaka mabadiliko kwa vitendo (pragmatism). Hiyo ni imani, matumaini na mwelekeo wetu. Tunahitaji vyama viwe na falsafa na itikadi ili wananchi wachague ni chama gani kiwaongoze katika wakati gani. Lakini hatuhitaji itikadi ya chama kimoja ndio iwe itikadi ya taifa lote kikatiba. Ingawa tunahitaji mjadala wa kitaifa. Ili tuwe na misingi ambayo tutakubaliana kwa pamoja kama taifa katika katiba mpya, misingi hii kila chama kitaonyesha ubunifu na umahiri wa kuizingati, kuitafsiri na kuitekeleza kupitia falsafa, itikadi, sera na shughuli zake. Nawasilisha hoja hizi kuendeleza mjadala tujiulize- Tanzania, CCM, CHADEMA na mjadala wa falsafa na itikadi; lipi ni jibu?
 
- Jamani wandugu kuuliza sio ujinga, mrengo ni mtu gani?

Respect.

FMEs!
FMES,
Mrengo ni neno linalotokana na neno "mrengu" ambalo maana yake ni bao linalofungwa pembezoni mwa ngalawa ili kuifanya iwe na mizani sawa pande zote mbili. So in this instance wanalitumia kuelezea "right wing" na 'left wing".
Kwa hiyo ukisikia wanasema "mrengo wa kulia" maana yake ni right wing na mrengo wa kushoto ni wale "leftists ambao wengine wanawaita wanamapinduzi.
 
Teh teh teh...yaani weye kijana wa kigogo umeanza darasa evening class sasa unaleta humu mjadala ili tukusaidie uandike pepa....!!! Ebo, haya maji marefu kwako, ile field nyingine ndo yakufaa.....
 
FMES,
Mrengo ni neno linalotokana na neno "mrengu" ambalo maana yake ni bao linalofungwa pembezoni mwa ngalawa ili kuifanya iwe na mizani sawa pande zote mbili. So in this instance wanalitumia kuelezea "right wing" na 'left wing".
Kwa hiyo ukisikia wanasema "mrengo wa kulia" maana yake ni right wing na mrengo wa kushoto ni wale "leftists ambao wengine wanawaita wanamapinduzi.

Jasusi, darasa la wapi hili? Kivukoni? Just checking kwi kwi kwi.

Afu nchi yenyewe haitumia ngalawa toka ukoloni sasa Mrengu wa nini tena?
 
FMES,
Mrengo ni neno linalotokana na neno "mrengu" ambalo maana yake ni bao linalofungwa pembezoni mwa ngalawa ili kuifanya iwe na mizani sawa pande zote mbili. So in this instance wanalitumia kuelezea "right wing" na 'left wing".
Kwa hiyo ukisikia wanasema "mrengo wa kulia" maana yake ni right wing na mrengo wa kushoto ni wale "leftists ambao wengine wanawaita wanamapinduzi.


- Ahsante mkuu, yaani kwa kunijibu hoja kwa hoja badala ya viroja maana humu kama anavyosema Sophia na Rais, watu wamejaa chuki na wivu tu wa kukosa u-Rais na U-firts Lady, unauliza swali linajibu viroja, Bwa! ha! ha!

Respect.

FMEs!
 
Ujamaa wa Nyerere ulianzia kwenye misingi hiyo hapo chini, nadhani labda tungejaribu kuangalia ni wapi alipokuwa amechemsha

1. 'WATU WOTE NI SAWA'
"...Kama hukubali hilo, yaani kama unadhani watu wengine ni miungu wengine, malaika, wengine nusu-nyani, basi hukubali ujamaa. Ujamaa kwako hauna maana, kwa sababu ujamaa unahusu usawa wa watu: hapo ndipo unapoanza...Sisemi usawa wa urefu wala ufupi; kwa urefu namzidi Kawawa, sana tena. Sisemi maguvu, hata; nasema utu, watu, na ubinadamu wao. Kuna binadamu zaidi ya mwenziwe? Kama huliamini hilo, utakuwa mjamaa? Hilo la kwanza... mkaliulize-ulize, mlielewe maana yake. Na mtu anayepinga ujamaa naye ajiulize kama anapinga hilo nalo. Mtu mpingaji ujamaa aseme, 'Hilo nalo, usawa wa watu, napinga; kwamba binadamu wote hivi si sawa'" - Mwalimu Julius K. Nyerere

2. 'LAZIMA MTU AFANYE KAZI'
"...Binadamu hao unaotuona hapa, na hao waliosambaa dunia nzima wanaishi kwa kazi. Hawana namna nyingine ya kuishi. Wakiacha kufanya kazi watakufa; hawana namna nyingine; kuishi kwao, na kuendelea kuishi, lazima wafanye kazi...Lakini binadamu haishi kama farasi. Binadamu haridhiki kuishi kama farasi au punda; binadamu ana kitu anakiita maendeleo; lazima aendelee...Wakati mwingine ili kusudi maendeleo haya yaje wana shughuli za kupigana misasa akili, wanapanuana mawazo tu, nayo ni kazi...nendeni mkaulizane...kama kazi si kitu cha lazima, kama binadamu anaweza kujikalia tu hafanyi kazi, akaishi, na maendeleo yakaja bila kazi. Na huyo anayepinga ujamaa naye ajiulize kama hilo analipinga? Na hilo la kufanya kazi analipinga au kuna jingine analopinga?" - Julius K. Nyerere

3. 'HAKUNA MTU KUMNYONYA MTU'
"...Kama binadamu ni sawa, tunalikubali hilo...Pili tunasema kitu kazi ni jambo la lazima kwa kila mtu, hakuna aliyesamehewa kazi. Basi siwezi kukufanyia kazi. Kukufanyia kazi maana yake ni kwamba wewe unasamehewa kazi! Siwezi kukufanyia kazi. Wewe utafanya kazi, na mimi nitafanya. Sio mimi nifanye, wewe hufanyi; lazima ufanye kazi. Kwa hiyo wewe utafanya kazi, na mimi nitafanya kazi; kila mtu atafanya kazi. Yaani namna ya kulitamka hilo ni kwamba kunyonyana hakuna. Hakuna mtu kumnyonya mtu; sasa tena msingi wa kumnyonya unatoka wapi? Tumesema watu sawa; na mtu ili aishi hana budi afanye kazi, na kazi ndio msingi wa maendeleo. Sasa mwanachama... ajiulize kama anaweza kuwa mjamaa na huku ananyonya! Unamnyonya mkeo; mkeo anakwenda kufanya kazi wewe unakwenda kupiga chibuku; hivi kweli mjamaa wewe? Tunasema kazi jambo la lazima, lakini wewe hufanyi kazi, unamnyonya mkeo. Wewe mjamaa? Nasema na hilo mjiulize...Unaweza kuwa mjamaa na huku unanyonya? Na anayepinga ujamaa ajiulize hilo nalo analipinga, kwamba yeye anaona kunyonya ni sawa tu! Sawa yeye kunyonya mwingine au wengine kumnyonya yeye, huyu anayesema kunyonya ni sawa. Kama kunyonya ni sawa baba, sasa tuanze kunyonya, au mkuki kwa nguruwe?" - Julius K. Nyerere

4. 'VYOMBO MUHIMU VIMILIKIWE PAMOJA'
"...Kama watu ni sawa; binadamu wote ni sawa; kazi ni jambo la lazima kabisa; kunyonya ni haramu; la nne linafuata: Vyombo vyote vya lazima, vinavyohitajika kwa maisha ya binadamu kwa kufanyia kazi lazima vimilikiwe kwa jumla. Ardhi lazima imilikiwe kwa jumla maana tusipoimiliki ardhi kwa jumla tutamwachia Rashidi Kawawa na Sheikh Karume wao wawe ndio wenye ardhi, na ardhi ni kitu cha lazima kwa maisha, hebu tuone kwanza usawa utakuwaje. Itakuwa lazima twende kwa Rashidi na kwa Karume, 'tafadhali bwana nataka ardhi'. Umekwishamwita 'Bwana' huyu; usawa umekwisha. Lakini vilevile kama Sheikh Kawawa ana ardhi, na Sheikh Karume ana ardhi, hawa hawalazimiki kufanya kazi. Kwa nini wafanye kazi? Hawawezi kufanya kazi. Tumesema kazi ni kitu cha lazima kwa kila mtu, lakini hawa hawawezi kufanya kazi, watakaa tu wanatutoza kodi kwa ardhi yao. Ndiyo wanatunyonya hivyo tena. Mimi nafanya kazi; mimi nalima. Halafu Rashidi anasema, 'Ukishalima mahindi ukapata magunia matano, moja langu'. Ndio ananyonya hivyo. Anavunja kanuni ya usawa; anavunja kanuni ya kazi; anavunja kanuni ya kutonyonya. Kwa nini? Kwa sababu tumemruhusu amiliki yeye vitu ambavyo vinastahili viwe vya wote. Mtu ambaye yeye ana ardhi; umemkabidhi viwanda, ukishakuwa umemkabidhi majambo mengine haya, umemwongezea nguvu zake, yeye utu wake umeongezeka-ongezeka na wangu mimi umeupunguza-punguza. Kwa hiyo vitu vilivyo vya lazima kwa kila mtu, kama ardhi ambayo ni ya lazima kwa kila mtu, lazima vimilikiwe na wote. Sasa...mjiulize kama unaweza kuwa mjamaa kweli huku unajidai ardhi yangu? Na wanaopinga wanatakaje? Hao wanaosema ujamaa mbaya. 'Eti vitu vyote viwe vya ujumla'; wengine waongo, 'Eti wanasema hata wakina mama wawe wa jumla'. Tunasema ardhi, hatusemi kina mama, tunasema ardhi viwanda, madini: kwa nini mtu mmoja anakwenda kuvinyakua vikawa vyake hivi!" - Julius K. Nyerere

5. 'KUUNDA NCHI BILA MATABAKA'
"..Kama tunakubali kuwa watu wote ni sawa; na watu wote ni lazima wafanye kazi, mtu asimnyonye mtu; na mali, mali kubwa, sikusema shati langu liwe la Rashidi: misingi ya uchumi kama mabasi yale yanapita iwe kwamba tunasema mabasi yetu, asiweko mheshimiwa mmoja pale anasema 'Basi langu lile!' Basi lako! Yupo dereva mle anaendesha, anasema dereva wake! 'Dereva wangu' - dereva wako, wewe unaweza kuwa na dereva? Dereva anaweza kuwa dereva wa umma, sio dereva wako. Dereva ni sawa sawa na mwalimu; mwalimu wa umma, daktari wa umma, dereva wa umma. Huyu anakuwaje 'wako'? Hata askari siku moja utasema wako. Kama tunakubali watu wote ni sawa; watu wote lazima wafanye kazi, hakuna kunyonyana; mali,vitu vyote vile vya jumla lazima viwe vya umma; maana yake ndio kusema tunataka kuunda nchi ambayo haina tabaka: hakuna mabwana na watwana." - Julius K. Nyerere
 
Teh teh teh...yaani weye kijana wa kigogo umeanza darasa evening class sasa unaleta humu mjadala ili tukusaidie uandike pepa....!!! Ebo, haya maji marefu kwako, ile field nyingine ndo yakufaa.....

- Una maana ile field yetu ya kwanza tulipofika majuu na nguo za zambarau nini mkuu, yaani kulea wazee na matahira au ya sasa tukiwa na PhD ya online huku tukihesabu hela benki na online abusing? Bwa! ha! ha! ha? Bwenga bwana una mayai yanakuwasha nini mkuu si utage tu! Bwa! ha! ha!

- Haya sasa kafungue thread kule chini kwamba umechokozwa na umetukanwa maana ndio zako hizo! Bwa! ha! ha! ha!

es!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom