Commonwealth Games 2010-INDIA

Haki ya nani tena kuna article zinachekesha.... duuh!!!:becky::becky:

Umeona eeh!!!!!!!! yaani hawa jmaa utafikiri walianza maandalizi Januari mwaka huu. Bado ntaendelea kuwasifu South Africans, kwao issue ilionekana ni security tu sanasana. Haya mambo ya hygiene kwa keli ni aibu hata kuyazungumzia!!!!!!!!!!
 
Wadau naona kwenye tbc 2 leo ndio ufunguzi wa mashindano. Pamoja na kusemwa sana inaonekana India imejipanga vizuri kwani mahudhurio ni 90% perfect. Tusubiri sasa michuano yenyewe. Ufunguzi bado unaendelea
 
Dah! Wadau hamna ving'amuzi? Ufunguzi wa hii commonwealth games ni bomba kweli

2.jpg
 
Ilipendeza! Wazungu wameleta unafiki wao weeee! mpaka wamechoka!ooohh! eti standard ya facilities ni ndogo, mara security, mara child employment you name it. Jamaa wanafiki!!!They tried to ruin the SA's word cup as well.
 
Achana nao hao Wazungu!
 
wazungu wana choyo wakati mwingine bana...!!!
Jana tukisubiri mechi ya Sunderland na Man Utd ilibidi tuchelewe kwa dakika 20 kwa kuwa tu kuna paipu ya choo ilipasuka chumba cha kuvalia cha Man Utd, mbona hawayasemi kama ni aibu...wazungu bana!!!
 
Wahindi wana mbwembwe kweli. Wameonyesha mambo ya kisasa hadi yale ya kale kabisa, ila sikuona tembo pale

article-1286119516073-0B75CF04000005DC-216513_636x355.jpg
 
...kuna bondia watanzania alikuwa anakung'utwa muda mfupi uliopita na bondia toka Pakistan and Referee Stopped the contest.
Arrrggghhh, kichwa cha mwendawazimu.
Nitawaletea jina soon,...
 
19th+Commonwealth+Games+Day+2+Boxing+cKNLjHu6-6Rl.jpg

19th+Commonwealth+Games+Day+2+Boxing+hHc97JAQe4Zl.jpg

19th+Commonwealth+Games+Day+2+Boxing+GBlLWA30vKel.jpg

19th Commonwealth Games - Day 2: Boxing
In This Photo: Haroon Iqbal, Sunday Elias
Haroon Iqbal (r) of Pakistan in action against Sunday Elias (l) of Tanzania in the 52kg Fly weight division at the Talkatora Indoor Stadium during day two of the Delhi 2010 Commonwealth Games on October 5, 2010 in Delhi, India.

Iqbal ame score points 12 - 1 za Bwana Elias,....
 
Iqbal ame score points 12 - 1 za Bwana Elias,....

Haya mashindano ni moja kati ya yale ambayo Tanzania inatakiwa kuacha kushiriki mpaka itakopokuwa imejiandaa vya kutosha,.. aibu tupu.:A S-frusty::angry::angry:
 
Haya mashindano ni moja kati ya yale ambayo Tanzania inatakiwa kuacha kushiriki mpaka itakopokuwa imejiandaa vya kutosha,.. aibu tupu.:A S-frusty::angry::angry:

...khe khe! 'wakale wapi?'
Tuliacha kushiriki yale "yasiyo na maana" mfano UMISETA, UMISHUMTA, MAJESHI nk...
 
Tanzania yaanza vibaya Madola
SAFARI ya Tanzania kusaka medali kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola nchini India imeanza vibaya baada ya wanamichezo wake wa kuogelea kutolewa mapema.

Akizungumza na Mwananchi kutoka New Delhi, mkuu wa msafara wa Tanzania, Juliana Yasoda alisema wamepoteza medali katika michezo ya kuogelea na mpira wa meza.

Waliotolewa ni Mariam Foum, mwogeleaji wa mita 50, freestyle ambaye pia hushiriki mita 50 alishika nafasi ya nne, hivyo kutolewa.

Mwanadada huyo alishika nafasi ya sita katika kuogelea mtindo wa breast- stroke huku medali za kwanza zikitarajiwa kuanza kutoka siku ya kwanza ya michezo hiyo jana.

Tanzania, pia ilifungwa na Ghana katika mpira wa meza, ambako mashindano yanafanyika kwa mtindo wa ligi na hivyo kuondolewa, leo watakamilisha ratiba kwa kucheza na Malyasia.

Wakati huo huo, mwanariadha aliyetemwa kwenye kikosi kinachoshiriki michezo hiyo, Zakia Mrisho amesema kuwa anasikitika kushindwa kushiriki katika mashindano hayo makubwa.

Zakia aliyetemwa katika kikosi hicho aliiambia Mwananchi kuwa alitegemea kushiriki mashindano hayo, lakini alipofika nchini aliambiwa hakuna tiketi iliyoachwa kwa ajili yake kwenda India kuungana na wenzake.

"Nina uchungu kuikosa michuano hiyo, ni kweli nilikuwa Italia nikikabiliwa na mashindano ya klabu yangu ambayo ndiyo imekuwa ikinidhamini katika mashindano mbalimbali ya kimataifa.

"Baada ya mashindano hayo nilirudi nchini Septemba 27 siku moja baada ya wenzangu kuondoka , lakini nikaambiwa sina tiketi ya kuniwezesha kufika huku kuungana na wenzangu, imeniuma, " alisema Zakia.

Kabla ya wanamichezo kuondoka nchini kwenda India, serikali ilisema kuwa mchezaji yoyote atakayechelewa kurejea nchini kuungana na wenzake kabla ya kwenda India na hatimaye kukuta wenzake tayari wameondoka, atakuwa amejiengua mwenyewe kutoka mashindano hayo.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Leonard Thadeo alisema kuwa mwanamichezo yoyote atakayeshindwa kurejea nchini wakati timu inaondoka atakuwa amejiondoa.

source: mwananchi

Kweli huu ni uozo...
 
...khe khe! 'wakale wapi?'
Tuliacha kushiriki yale "yasiyo na maana" mfano UMISETA, UMISHUMTA, MAJESHI nk...

Unajua mkuu mimi huwa napata hasira sana na hii hali ya Tanzania kusindikiza ktk kila mchezo....tatizo liko wapi jamani hata kamchezo kamoja nasi tuwe tunajivunia nchi yetu. Kweli hawa watu wanakela sana , wanafanya mambo kutimiza ratiba tu na kubaki na kumbukumbu za kuwaaambia wajukuu zao kuwa mi nilkuwa India kwenye mashindano ila alichokipata ni sikio.....Sasa huyo jamaaa anapata point moja mwenzake ana 12... hiii si fedhea, ulijiandaa kweli kwa haya mashindano wewe.... hawa ndio wakuchapa bakora :A S angry:
 
...mwingine huyu naye amekula mkong'oto. Safari hii kipigo toka kwa majirani zetu hapo.

RESULTS
Early results from the first day of boxing in New Delhi:
Preliminary round:
Light-welterweight (64 kg): Blackmoses Mathenge (Kenya) bt Hashim Petro (Tanzania) on points

...PingPong, unajua hatujapeleka team bora, tumepeleka bora team ikashiriki. Wa kuchapwa bakora sio wachezaji bali Waziri wa michezo, katibu mkuu wake, wajumbe wa baraza la michezo Tanzania, wana Kamati ya Olimpiki Tanzania, na waratibu wote wa safari hizi. Msafara una 'wanamichezo' 40, lakini na mashaka iwapo washiriki wanazidi hata watu 10 hapo, waliobakia wasindikiza watalii!
 
How old is this guy?

Has he won anything since the 2006 commonwealth games?

Samson Ramadhani Nyonyi (born 25 December 1982 in Singida)
2007 alishinda Lake Biwa marathon Japan kwa kutumia 2hrs10mins43secs
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom