Law(LLB), BA (sociology), BA (Geography &environment studies), Bsc(urban planing), BA ( Fine and perfoming arts), BA (Journalism), BA (Political science and public administration), Human Resources management, Social work, Education, Linguistics
Ukisoma LLB, unaweza kuwa hakimu na Mungu akikujalia utakuja kuwa Judge.
Pia unaweza kuwa mwanasheria wa kujitegemea,
Sociology : Unaweza kuwa Afisa maendeleo wa jamii katika wizara na idara mbalimbali, pia unaweza kuajiriwa TAKUKURU, Police, Magereza, Jeshini, Uhamiaji, Zimamoto, na Usalama wa taifa
Urban planing : Utaajiriwa kama afisa mipango miji. Lakini pia unaweza kuajiriwa kama nilivyoainisha kwa mtu wa Sociology.
Journalism : Unaweza kuajiriwa kama mwandishi wa habari, ama ukawa mwandishi wa habari wa kujitegemea, pia unaweza kuajiriwa kama msemaji wa kampuni au shirika. Na hapa pia unaweza kuajiriwa kama nilivyoeleza kwa mtu wa sociology.