Comb ya HGL unaweza kusoma kozi gani degree?

kilukunyenge

Member
Dec 21, 2016
20
16
Habari, naomba kujua mtu anayesoma comb ya HGL anaweza akasoma kozi gani degree na ipi ni nzuri zaidi kwa utafutaji wa ajira?
 
habari naomba kujua mtua anaesoma comb ya hgl anaweza akasoma kozi gani degree na ipi ni nzuri zaidi kwa utafutaji wa ajira
Education
Sociology
Law

Na nyinginezo nyingi Mkuu. Inategemea we unapenda nini haswa.

Kila kozi ina ajira,what matters is how competent you are. Soma kitu unachokipenda kwa bidii.

Education ina uwanja mpana zaidi wa kujitafutia ajira lakini sasa hivi walimu wa masomo ya Sanaa (Arts) washaanza kuzinguliwa. Ingekua miaka ile ambayo tulisoma sisi,ilikua ni dili sana. Kwa sasa soma tu ili uondoe ujinga kisha rudi mtaani kupambana kwa njia zote za halali.
 
Mkuu Combi Hiyo Jiandae Kisaikolojia Kufungua Tuition! Vinginevyo Utaishia Kutembea Na Bahasha...
 
Kombi zote za biashara na uchumi kama ulufaulu hesabu olvl pia mamb ya ardhi mipango sheria logistics uasibu
 
Law(LLB), BA (sociology), BA (Geography &environment studies), Bsc(urban planing), BA ( Fine and perfoming arts), BA (Journalism), BA (Political science and public administration), Human Resources management, Social work, Education, Linguistics

Ukisoma LLB, unaweza kuwa hakimu na Mungu akikujalia utakuja kuwa Judge.
Pia unaweza kuwa mwanasheria wa kujitegemea,

Sociology : Unaweza kuwa Afisa maendeleo wa jamii katika wizara na idara mbalimbali, pia unaweza kuajiriwa TAKUKURU, Police, Magereza, Jeshini, Uhamiaji, Zimamoto, na Usalama wa taifa

Urban planing : Utaajiriwa kama afisa mipango miji. Lakini pia unaweza kuajiriwa kama nilivyoainisha kwa mtu wa Sociology.

Journalism : Unaweza kuajiriwa kama mwandishi wa habari, ama ukawa mwandishi wa habari wa kujitegemea, pia unaweza kuajiriwa kama msemaji wa kampuni au shirika. Na hapa pia unaweza kuajiriwa kama nilivyoeleza kwa mtu wa sociology.
 
Back
Top Bottom