Colman Massawe mmiliki wa Skol Building Contractors afariki dunia kwa ajali ya gari Bagamoyo

IMG-20170823-WA0124.jpg
 
Gari imeisha yote yani, kweli ajali ni ajali tu...Huwa nashangaa wanaosema Toyota zipo less secured ila je hata ingekuwa ni Range Rover apo angetoka mtu pamoja na ma airbag yote!?
Mimi huwa naamini siku yako ikifika hayo mengine yote inakuwa ni vijisababu tu vya Israeli kuchukua roho.
Kuna ajali niliwahi kuishuhudia Dakawa nilishangaa sana watu kutoka wazima kabisa na kuwa na michubuko tu mkuu. Kifo kina siri nzito sana ndugu.

Kuhusu masuala ya gari nafikiri teknolojia sasa hivi iko juu kwenye baadhi ya haya magari ya kifahari ie: Range Rover, Merc Benz and the likes. Tatizo kubwa kwenye ajali huwa ni speed na kupoteza control ya gari.
Haya magari ya sasa yamefungwa sensor za kutosha kuweza kupunguza athari za ajali zinazotakana na uzembe wa kibinadamu. Na airbags za siku hizi zinatoka mpaka pembeni ya milango na kuwakumbatia kabisa watu ndani ya gari. Tofauti na zile za kutoka kwenye sterling wheel.

Hiyo ajali inaonekana dhahiri mwendokasi ndio chanzo cha yote.
 
Back
Top Bottom