COET - UDSM yajitengenezea mradi wa Kinyemela

Mdwenke

Member
Jul 16, 2012
78
55
Kitendo cha kushangaza sana miaka miwili iliyopita COET katika mradi wake wa BICO - Bureau of Industrial Cooperation walianzisha kozi mbalimbali za kkiwango cha cheti, diploma hadi diploma ya uzamili. Kozi hizo ni katika fani ya utunzaji kumbukumbu, manunuzi, raslimali watu n.k. Wakiwa wanaendelea na hizo kozi kumbe UDSM hawakuwa na taarifa na hivyo basi kukawa na akaunti za fedha ambazo zilikuwa chini ya COET na BICO ambazo signatories wake walikuwa wanaendelea kuzichukua tu pesa bila UDSM kujua nini kinaendelea. Tatizo limekuja kujitokeza pale wale wanafunzi kundi la kwanza, baada ya kumaliza kozi wakawa wanafuatiia vyeti na kupigwa danadana, mpaka habari zilipofika UDSM kwenyewe ndipo imetokea mshangao mkubwa. UDSM wamejaribu kushughulikia tatizo hilo na inavyoonekana wanataka kuwaonea wanachuo ambao tayari wanaendelea na masomo na wale waliomaliza huku wakichukua pesa zao kama karo na zinginezo kama vitambulisho, nk ingawa hata vitambulisho hawajawahi kutoa. Sasa hivi COET nao wameanza kuwafukuza hao wanachuo na kuwashawishi watafute nafasi sehemu zingine ilihali wakiwa tayari wameshachukua pesa zao na wengine wameshasoma miaka miwili. Mbaya zaidi bila kutatua tatizo kwa wanachuo UDSM imemsimamisha kazi Profesa Katima aliyekuwa Mkuu wa COET na kutoa wafanyakazi wengine waliokuwa wakishughulika na akaunti hiyo na huku wakiendelea kukwepa kushughulikia tatizo la wanachuo hawa eti kwamba UDSM inadhalilishwa.

Jambo kubwa la kujiuliza ni kwamba, inakuwaje UDSM na COET wanaanza kuwakana hawa wanafunzi mamia ambao walichukua pesa zao? Kwa nini COET pai wanazuia hawa wanachuo wasionekane pale chuoni? Mbona akaunti za BICO ambako pesa zilizokuwa zikilipwa na wanafunzi hawa zianajulikana? Kwa nini COET na UDSMA wasimalize mgogoro huu, ama wanataka iwe kama ile kesi ya wanafunzi wa UDSM walioingizwa Chuo cha Ardhi kinyemela? Matokeo ya kesi hiyo yanajulikana na kama hili halitashughulikiwa ipasavyo tunasubiri kwa hamu kwenda mahakamani palipo haki zetu wanyonge.
 
Nawasihi wnfnz wadai vyao ndo waondoke wasitake kuwachezea akili dah mbn kila kona ni ubadhirifu tu?
 
ndio mkuu......usisahau hata pale ucc...ule mradi wa unawao rubuni wazazi wengi

Kila chuo lawamani aaah!!who is responsible to solve these institutions issue,waziri husika?lakini mbona hapo UCC kuna watu ninaowafahamu wamemaliza hapo na wapo kazini sasa,na wengine wamepita na wanajiendeleza kielimu kwengine.....acheni lawama someni vijana,comment za vyuo ni lawama tu!la BICO na CoET sina comment
 
Kila chuo lawamani aaah!!who is responsible to solve these institutions issue,waziri husika?lakini mbona hapo UCC kuna watu ninaowafahamu wamemaliza hapo na wapo kazini sasa,na wengine wamepita na wanajiendeleza kielimu kwengine.....acheni lawama someni vijana,comment za vyuo ni lawama tu!la BICO na CoET sina comment

Kwa nini la BICO na COET huna comment?
 
Back
Top Bottom