Kassim Awadh
JF-Expert Member
- Mar 12, 2012
- 884
- 187
Wakuu kuna huu usafiri wa Mbeya - Dar kwa kutumia Coaster wenyewe wanaziita hakuna kulala, Zinaanzia Uyole pale jijini mbeya na kwa Dar zinapakilia Kidongo Chekundu, Zinaondoka around saa 9&10 jioni sehemu kubwa ya safari ni usiku, ni usafiri usio rasmi kwa maana ya kutambuliwa na Sumatra maana hawana TLA ya PSV bali Tours hivyo kuwa na kibao cha "private", Concern yangu hapa ni uendeshaji wa hatari unaofanywa na madereva hawa, muda wote wako katika haraka ya ajabu, timings zao ni kuwahi wapite check point iringa kabla ya saa 6 na morogoro mjini muda ambao kwa sheria zetu ndo mwisho kwa magari ya abiria, nilisafiri na mmoja akawa na mwendo wa hatari, overtake za hatari more worse kila abiria walipomkanya ndio kwanza alizidisha mwendo na madoido mengine. Rai yangu kwa Sumatra watupie jicho na kuona namna ya kuwadhibiti hawa halikadhalika Polisi ambao hata hivyo ndio wachukua posho wakuu kutoka magari haya