CNN: Kenya inaongoza kwa matumizi ya ICT, Tanzania kwa uchawi!

Ni kweli kabisa mkuu.

Mostly kwenye neno la Mungu, Wakenya wanajiuliza sana,kwanini watanzania badala ya kulitangaza na kufundisha neno la Mungu, huwa wanazungumzia majini, watu kupelekwa chini ya bahari, watu kunyeshwa damu za watu, na wenyewe wanashangaa kuona mpaka baadhi ya redio zikitangaza hadharani haya mambo.
 
Wabongo kwa ushirikina ndio wenyewe. Hata wanaoamini katika miujiza/uponyaji kwenye mikusanyiko ya kiimani hawana tofauti sana na washirikina.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Tanzania ndio kuna imani za kichawi lakini kusema kuwa tunaongoza duniani hapo nina mashaka. Sijui huyo Errol Barnett/CNN amefanya utafiti 'independently' na kujirishisha kweli Tanzania inaongoza?

Kwa upande mwingine hii ni wake up call. Waziri mkuu alikuwa kanda ya ziwa na aliambiwa kuhusu tatizo la kuuwa vikongwe, lakini badala ya kusema hatua za kisheria zichukuliwe ameishia kusema 'tukemee!
 
Ni kweli watz una amini sana nguvu za giza, nina ndugu yangu wa damu ambae mambo yake yalimuendea vibaya hapa Dar akambilia Arusha na kujifanya mganga.Na sasa anamalizia nyumba yake Mbezi ya Kimara.

Hii inathibitisha jinsi watz tulivyo na imani za kishirikina,na ndio maana atuendelei, huko maofisini ndio mchezo wa kulogana umekithiri hadi wengine wanaenda kuwaloga wenzao wawe wendawazimu iliwasiondolewe kwenye vyeo vyao.
 
Mimi kinachonishangaza ni kwanini serikali inaachia watu kutangaza uchawi hadharani. Mfano mganga anatangaza anatibu majini, mapenzi, kutoa dawa ya biashara nk lakini bado serikali haioni ubaya wa huu ujinga na utapeli?

Ni kwa kuwa viongozi wa serikali wenyewe wanaamini kwenye uchawi. Wako ofisini kwa nguvu za waganga akiwepo rais wa nchi. Wakiwa hadharani wanamtaja Mwenyezi Mungu lakini sirini wana hirizi hadi kwenye makalio. Kila kona waganga, hasa wenzetu wanaoamini imani ya waarabu ndio usiseme. Sasa ni uchawi wa kiafrika changanya na uchawi wa kiarabu kwa jina la dini fulani jibu rais anaongozwa na jopo la wachawi. Nani atapiga marufuku huu upuuzi?

Tanzania tunatia aibu jamani.
 
Hapa ndipo napowapendea wabongo, kwa sababu huwa hawataki kusikia ukweli, huyo mtangazaji yupo sahihi kabisa kwa sababu yeye kafanya utafiti hajakurupuka kama wewe uliyeleta hii thread
 
Hakuna fitna, ni kweli kabisa watanzania wanaendekeza ushirikina wakiongozwa na kiongozi mkuu wa nchi.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
nikweli jamani mimi ninaushahidi kuhusu hilo.ni nadra kenya kukuta bango la mganga wa kienyeji.wakenya nafanya nao kazi walipofika cha kwanza waliuliza mbona matangazo ya tv mengi ni vileo na uzinzi! Waganda pia wanahusudu waganga wa tz wanasema tuko juu!

Mabango ya waganga yapo Kenya, ila mengi yanatangaza "mganga kutoka Tanga" au "kutoka Sumbawanga" wanasema huko ndio mwisho wa mawazo.

Mimi nasema mtoto mchanga akiwa na neno la Mungu kinywani atamtimua shetani mwenyewe, licha waganga. Je wewe mwenye uwezo zaidi? Ukimwachia Mungu kuyatawala maisha yako , japokuwa matatizo ni kawaida kwa binadamu lazima utashinda. Mungu Mwenyezi akiamua upate matatizo au uwe masikini kubali na umshukuru kwa yote, kwa kuwa hakuna anaye weza kubadilisha mipango ya Mungu. Huwezi kuyabadilisha maisha yako kwa kwenda kwa mganga, huyu ni mfuasi wa shetani ambaye kutoka kinywa chake utoka uongo, kuua na kuangamiza pekee,hana zawadi anaweza kukupa wewe. Vitu vyote vizuri utoka kwa Mungu.

Shetani hana shukrani, wakala wake ni mganga. Unapoenda kwa mganga ufalme wa Mungu unaomboleza. Ndugu yangu au dada yangu fikiria mara mbili kabla kuamua kujikabidhi kwenye imaya ya shetani. Hakuna kitu kibaya zaidi duniani unachoweza kuwaachia wanao au mkeo, au mmeo kama nguvu za giza.
 
Rais wetu husafiri na wachawi
Siku hizi huna mpinzani hapa baada ya kuondoka malaria Sugu.Lakini huenda ni kweli mbona Sheikh Yahya (alale vyema pale anapostahili) alisema yeye ni mlinzi wake hatukusikia msemaji wa Rais (Salva Rweyemamu) akikanusha bali alisema hayo ni maoni yake na mpaka leo hakuna aliyekanusha kashfa ile halafu watu wanafikiri CNN wananababaisha kama TBCCM. Juzi nimepata habari toka kijijini kwetu nilishtuka kwamba robo tatu ya kijiji chetu wanashukiwa kuwa wachawi wakiwemo vijana wa chini ya miaka 30. Hii ndio Tanzania
 
Vikongwe na Albino wanauwawa kwa Imani za kishirikina! Wanasiasa na wafanyabiashara wanakwenda kwa sangoma ili wafanikiwe malengo yao.Hata marehemu Sheikh Yahaya alisema atampa ulinzi usionekana Dhaifu.Na mpaka leo ikulu haijakanusha ulinzi huo wa kimazingara.
Kule Mbeya kuna mtindo wa kupiga watu kwa nondo na wanadai zinatumika kutundikia nyama buchani ili kuvutia wateja. Wewe unakwenda kununua kitoweo cha sikukuu kumbe unakula na damu ya binadamu mwenzio. Bado kuchuna ngozi na mengineyo. Wapi kuna haya mambo duniani kama sio Tanzania?

We fikiria eti tangazo la mganga linasema kuna dawa ya kupandishwa Cheo... Sijui kama definition yenyewe ya kupanda Cheo ndio hii iliyopo kwenye Sheria ya Utumishi wa Umma?
 
Huo ndio ukweli.... Kuanzia presdaa ushuke hadi chini, wengi wanaamini wanafanikiwa mambo yao wakienda kwa sangoma, wanasiasa uongozi, wafanyabiashara utajiri... yaani tafrani!
 
Tanzania kushika namnba 1 kwa ushirikina duniani, siamini kama ni kweli.

Sidhani kama watanzania tunawazidi wanigeria. Huyu mchunguzi hatutendei haki kabisa. Ila kwa upande mwingine tusikatae tuko mabingwa wa uchawi. Ni sisi watanzania ndiyo tunaongoza kwa kuua watu wenye ulemavu wa ngozi (maalbino); ni sisi magwiji wa kuchuna ngozi wengine kwa malengo ya utajiri; ni sisi maexpert wa kuua vikongwe wenye macho mekundu; ni sisi tunaongoza kwa kukimbilia kunywa vikombe vya madawa ambayo hata hayajathibitishwa na kitengo cha utafiti wa tiba; ni sisi tuko juu katika mambo ya juju na ndumba kwenye michezo (uchawi wa michezoni); ni viongozi wetu wengi wa ngazi za juu wanaojiganga kila kukicha na kuongozwa na wapiga ramli; ni sisi haohao ambao matukio mengi ya vifo na ajali tunayaunganisha na uchawi.

Fikiria mf. ajali ya Kafumu kule Igunga, Mwigulu alisemaje! Katika mazingira haya tutakataa kweli kwamba sisi si moja ya mataifa yanayoweka uchawi katika chati ya juu?? Kwa hali hiyo mataifa ya nje na vyombo vya habar vya nje vitashindwaje kujua imani yetu ya uchawi ilivyokithiri? Tafakari, chukua hatua.
 
Eti leo wanajifanya wamesahau!

Ni KWELI KABSAA! Ni nchi gani ambayo albino wanauawa kwa wingi kwa imani za kishirikina? TZ. Ni serikali gani ambayo inatumia jeshi lake la polisi na usalama wa taifa kuwakamata majangiri walioua faru ndani ya masaa 48 na kukamata majambazi walompora na kumuuwa mama wa kichina kwa saa12 tu lakini imeshindwa kukamata wauaji wa albino? Serikali ya CCM.,
 
Ni ukweli unaohuzunisha,we have to change our mind set on superstitution!
 
Tusipoangalia sana taifa letu na kizazi kijacho kitakuwa na misingi ya ulozi. Wanamaombi hamna kuchoka. It pays to pray and trust in God.
 
****. Tuelezwe vyema namna utafiti huo umefanyika katika nchi zote duniani na namna ya kudraw sample iwekwe wazi na maswali yote yaliyoulizwa na waliofanya huo utafiti wajulikane (profile yao)!

Tusikubali kuwa tunatukanwa tu na watafiti uchwara na kauli za ujumla jumla kama hizi
 
Kule Mbeya kuna mtindo wa kupiga watu kwa nondo na wanadai zinatumika kutundikia nyama buchani ili kuvutia wateja. Wewe unakwenda kununua kitoweo cha sikukuu kumbe unakula na damu ya binadamu mwenzio. Bado kuchuna ngozi na mengineyo. Wapi kuna haya mambo duniani kama sio Tanzania? We fikiria eti tangazo la mganga linasema kuna dawa ya kupandishwa Cheo... Sijui kama definition yenyewe ya kupanda Cheo ndio hii iliyopo kwenye Sheria ya Utumishi wa Umma?
bado kuna dawa ya KUFUTA KESI,SIKU HIZI KUNA WAGANGA WANATOA DAWA ZA KUJIUNGA NA FREEMASON,KWA BAHAT MBAYA NATUMIA MOBILE DEVICE NINGEWEKA PICHA HAPA
 
Serikali nzima inaenda Loliondo kwa babu Mwasapile utategemea nini? Au ushasahau viongozi ni kioo cha jamii?

Siyo tu CNN hata ETV ya Afrika kusini walishawahi onesha documentary film ya mauaji ya Albino Tanzania

la loliondo halikuwa ushirikiana bali imani ya mungu kama vile watu wsanavokwenda kwa akina mama lwakatare na wengine wengi waliofungua makanisa hapa tz
 
Back
Top Bottom