CNN: Dr. Slaa awa gumzo na hatari serikalini Tanzania

CNN: Dr. Slaa awa gumzo na hatari serikalini Tanzania

MAGAMBA MATATU

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2011
Posts
646
Reaction score
1,234
Habari zilizotolewa na kituo cha habari cha kimataifa cha CNN jana usiku kilikuwa na mjadala uliochukua takribani dakika 15 huku wakijikita zaidi kuhusu jinsi serikali ya Tanzania inavyoendeshwa na hatimaye wakasema kuwa kuna upinzani mkubwa sana ambao uko chini ya chama kikuu cha CHADEMA huku wakimtaja Dr Wilbrod Slaa kuwa amekuwa ni kiongozi anayetikisa viongozi wa nchi hiyo na hadi kufikia chama tawala kubadili mfumo wao wa utawala ndani ya chama tawala bila kujijua.

CNN walienda mbali zaidi na kueleza kuwa Dr Slaa ameonekana ni mtu makini na mpembuzi mkubwa wa nyaraka za wizi wa mali unaotokea nchini TZ.

Baada ya CNN kumaliza mjadala huo walihamia mjadala wa kujadili vifo vya watoto 20 vilivyotokea huko Marekani huku wakumuonyesha. Rais Obama akilia machozi kutokana na vifo hvyo.

Rai yangu ni kuwa hiki kituo cha CNN kitapingwa tena na CCM kuwa Dr Slaa si mtu anayewanyima usingizi kama serikali ya CCM kupitia waziri Membe alivyoamua kukipinga hiki kituo cha CNN pale kilipokuwa kinajadili mpaka wa Malawi na Tanzania?
 
Safi sana, mwendo mdundo kwenda mbele.
Bahati mbaya hiyo kitu imenipita na hivyo nimeshindwa kuiona.

Mkuu kwani huwa CCN wanarudia documentary zao ili tuone tena?

Vipi wanaweka U-Tube?

Kuna link yoyote unaweza kuiweka ili tuone?
 
Utaskia tamko la sekretarieti, waache wao waendelee kugaragara na kadi, akili fupi zina taabu kwelikweli
 
Ndio uzuri wa CNN.Wanaweka mambo hadharani sana!Na hapo serikali itataka iombwe radhi?
 
Yeah! Dr.Slaa ndio kiongozi mkuu wa upinzani Tanzania, wewe ni MKOMBOZI wetu na tunakuombea Mungu akupe nguvu, afya na kibali zaidi machoni pa watanzania wengi, Usikate tamaa sisi vijana tumehaidi kukulinda na kulinda chama chetu CHADEMA kwa nguvu zote.

Tolerance gives power.
Long live our hero.
 
Safi sana wao CCM wamebakia kulipia card ya Dr Slaa badala ya kutekeleza ahadi lukuki walizoahidi 2010
 
Hapo na bado ndo kwanza safari imeanza, Dr Slaa kaza uzi wabadili tena sekretariet hata mara 4
 
Dk slaa kiboko ya magamba, jamani nape na membe kawashika pabaya sana, ccm chalii
 
Dr Slaa ndiye kiongozi pekee atakayeleta mabadiliko ya kweli kwani tumeish naye,tunamwona na yupo miongoni mwetu,hana woga,ni mchambuzi wa mambo,hakurupuki,hakika udaktari wake siyo wa Madesa au wa kupewa kama wa akina mjomba na baadhi ya mawaziri wake.
 

wape na hii:

....
majangili wamekulaban......pilau..kanga..buku kumi kumi.... kwisha!!! wamebanana Lumumba!!!


 
Hii nayo sijui Nape Mapepe ataipokea na kuipondaje. Maana yeye akisikia jina Slaa anaweweseka kama yuko usingizini na kama yuko mtaani lazima aangalie huku na kule. Jamaa amewashika na kuwaweka pabaya.
 
Safi sana, mwendo mdundo kwenda mbele.
Bahati mbaya hiyo kitu imenipita na hivyo nimeshindwa kuiona.

Mkuu kwani huwa CCN wanarudia documentary zao ili tuone tena?

Vipi wanaweka U-Tube?

Kuna link yoyote unaweza kuiweka ili tuone?
Mkuu, CNN si local television, hiki kituo cha matangazo huwa kiko straight forward,,huwa hakirudii kumeza matapishi kilichotapika kama hizi TV zetu za bongo,,,guys knows what they are doing hawatoi documentary za kubahatisha,,,waandishi wake wako makini na ndio maana baada ya kutoa documentary iliyokuwa inahusu mpaka wa Malawi na Tanzania.Ikabidi serikali ya TZ itoe tamko kuwa CNN wamekosea inabidi wawaombe serikali ya TZ msamaha na wala CNN hawakufanya upuuzi huo,,,sasa sijui NAPE na secreatary yake nao watakuja na tamko gani
 
Wiki ijayo Al Jazeera watarusha nao kipindi maalumu juu ya Daktari Slaa na hatua zake imara na madhubuti azipitiazo kuelekea Magogoni kwa msaada wa Umma.

Mkuu tutajie siku na saa ili tujipange kutembelea bar na pub zenye ving'amuzi tushuhudie hiyo kipindi!
 
Back
Top Bottom