Clouds tv hiki kipindi cha kungwi/saa SAA 7mchana jumapili nani target audience yenu?

sambu

JF-Expert Member
Jan 12, 2011
285
283
Mambo ya mahusiano yanajadiriwa bila staha mchana kweupe. Nyie waandaaji nani kati yenu anaweza angalia likipindi hili na familia yake? TCRA hivi ndivyo mnataka jamii ya wa Tanzania tuelekee. Kwanini wasirushe kipindi hiki usiku. Yaani hili TV sijui ikoje? Mnatuharibia watoto jameni.
 
Hata mimi sikufurahishwa wanajadili mambo ya chumbani hadharani wakati wanajua kuna watoto hii ni tayari.
 
Target audience?........mkuu nani kakuambia Clouds wanafuatilia hiyo kanuni, wao bora kuwe na kipindi hewani hayo mengine yatajipanga mbele ya safari.
 
Mimi mwenyewe nilibaki najiuliza maswali mengi sana,hii tv ni jipu,
 
Clouds ni jipu wao ndio wanaharibu hii jamii kwa matamasha yao na vipindi vyao
 
Mambo ya mahusiano yanajadiriwa bila staha mchana kweupe. Nyie waandaaji nani kati yenu anaweza angalia likipindi hili na familia yake? TCRA hivi ndivyo mnataka jamii ya wa Tanzania tuelekee. Kwanini wasirushe kipindi hiki usiku. Yaani hili TV sijui ikoje? Mnatuharibia watoto jameni.

Wakirushe Usiku Wa Saa 5 Kwani Umesikia Ni Bunge La Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania? Nataka Nikupinge Kidogo Kuhusu Suala La Kukuharibia Watoto. Mimi Binafsi Nikijotolea Mfano Tokea Nikiwa Mdogo Kwanza Nilikuwa Ni Mtundu Na Mtukutu Mno Huku Nikiwa Napenda Mno Kuangalia Picha Za " Mikito ". Kama Hiyo Haitoshi Ni Kwamba Maisha Yangu Tokea Shuleni Hadi Chuoni Marafiki Zangu Wengi Walikuwa Ni Wavuta Bangi, Wauza Madawa Ya Kulevya Na Watumiaji, Vidokozi Na Walevi Ila Huwezi Amini Mkuu Ukiachana Tu Na Huu UCHAKARAMU Wangu Humu JF Sijawahi Kuvuta Hiyo Bangi, Kuuza au Kubwia Madawa Ya Kulevya, Kudokoa ( Kuwa Mwizi Japo Shule Ya Msingi Nilikuwa Napenda Mno Kuchukua Kalamu Za Wanafunzi Wenzangu Bila Ridhaa Yao ) Na Sinywi Pombe. Na Sikuishia Hapo Tu Hata Wakati Nikiwa Shuleni Tokea Chekechea Hadi University Nilikuwa Napenda Mno Kutoroka Kutoenda Shuleni au Darasani Lakini Nilishangaa Darasa La Nne, La Saba, Form Two, Four Na Six Niliweza Kufaulu With Flying Colours Ila University Ufaulu Wangu Ukawa Wa Wastani Huku Nikizizoea KUNAKOTUKUKA Supps. Tuache Kuwasingizia Watoto Wetu Kuwa Wanafanya Hovyo Shuleni Kwakuwa Wanakuwa Exposed Na Naughty Things. Tumekubali Globalization Basi Tuvumilie Na Implications Zake Katika Jamii Yetu. Unasema Clouds Tv Wanaonyesha Vipindi Vibaya Lakini Ulivyo MNAFIKI Hapo Hapo Mtoto Wako Umemnunulia SMARTPHONE Na Hadi Bundle La Wiki Umemuwekea Hivyo Anachokifanya Akiwa Tu Faragha Chumbani au Kwa Peers Wake Wana Google Styles Zote Za " Kungonoka " Na Tuvituvitu Vingine. Kizazi Hiki Cha Dot Com Kinajua Mengi Kuliko Hata Sisi Kizazi Cha Analog!
 
we wakati unakaa na hao wavuta bangi wakivuta ule moshi na wewe unauvuta bila kupenda hivyo ia umekuathiri...
 
Waweza kuwa sahihi kwa kiwango flani na hongera kwako wewe kutojihusisha na mambo yasiyofaa japo ulikuwa unajumuika na watendao hayo.

Lakini si wote na mara zote kila mtu anaweza kuhimili hicho ulichofanikiwa wewe.

Mimi nadhani ni bora kukinga kuliko kuponya baada ya madhara.

Utandawazi hatuwezi kuuepuka, ndiyo. Lakini lazima uwe rugulated kwa kujiwekea sheria na taratibu. Ndiyo maana tuna taasisi TCRA, EWURA, SUMATRA nk

Nadhani hawa Cloud TV wanachotakiwa kufanya ni kufanya marekebisho tu ya line up & timing ya vipindi vyao kulingana na walengwa hasa wa vipindi hivyo.

Sijakiona hicho kipindi. Lakini jina tu la kipindi "Kungwi" linaonesha kinachojadiliwa na kuoneshwa ni mambo yawahusuyo watu wazima 18+ yrs. Ni vyema wakakirusha muda ambao watoto wakawa wamepumzika
 
Back
Top Bottom