Clouds Media Group watangaza kusitisha tamasha la Fiesta Dar

Madimba jr

JF-Expert Member
Aug 12, 2017
1,577
3,143
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Uongozi wa Clouds Media Group kupitia kwenye ukurasa wao wa Instagram wametangaza kusitisha kilele cha tamasha la Tigo Fiesta lililokuwa lifanyike leo Jumamosi Novemba 24 katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar.

Sababu za kufanya hivyo hazijawekwa wazi. Hata hivyo jana kulisambaa taarifa ambazo zinadaiwa kutoka kwa Manispaa ya Kinondoni ikiwataka CMG kusitisha tamasha hilo katika viwanja vya leaders kwa kile kinachodaiwa malalamiko ya makelele kutoka wakazi wengi wa maeneo hayo wakiwemo wagonjwa.

Walionunua tiketi kwa njia ya miamala ya simu za mkononi kurudishiwa fedha zao. Walionunua kwenye vituo watakiwa kwenda kuchukua fedha zao wakiwa na tiketi

Wawashukuru waandaaji wenza na Wananchi kwa ujumla

EBC9C475-7091-4604-9AA4-5D061165AAFD.jpeg
 
Back
Top Bottom