Clouds Media Group Jisafisheni; rudisheni fedha

Clouds Media Group Jisafisheni; rudisheni fedha

zandrano

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Posts
8,416
Reaction score
9,324
Njia pekee ya kujisafisha kutoka ktk uchafu huu ulio tolewa na ripoti ya CAG na kuhusisha clouds kupokea Tz sh. zaidi ya million 600 njia pekee ya kujisafisha ni kurudisha pesa ya serikali maaana utaratibu ulikiukwa na hivyo kubatilisha utaratibu wote, hakuna uhalali wa clouds kupokea fedha ambayo haikuzingatia utaratibu vinginevyo lazima kulikuwa na njama au nia ovu ya kuiibia serikali.

Kwa sasa baada ya ripoti njia pekee ni kurudisha fedha ya watanzania badala kuanza kujisafisha kupita media zenu hiyo haisaidii kwa sasa. kwa sasa ripoti ya CAG ndio inasimama kwa uzito.

Kwa sasa Clouds Media Group hamna uhalali wa kujadili ripoti ya CAG kwa sababu nyinyi ni wachafu, kwani mnatuhumiwa kukwapua fedha za umma kwa kushirikiana na watu wasio waadilifu.

Clouds njia pekee ya kujisafisha ni kurudisha pesa ya watanzania mlio ipokea kinyume na taratibu.
 
Yaani mpaka nimechoka kabisa, yaaani hii nchi kila mtu mpigaji dili tu, watu wanapiga diliii tu, wanakwapua tu fedha za Watanzania. Halafu Watanzania wanazidi kuwa masikini. Wajanja wanakula tu bila hata kuvuja jasho.
 
Walishafanya kazi ni vp warudishe pesa? Njia bora ni wataje kiasia halali walicholipwa
hata kama walifanya kazi, ile pesa haikuwa kwenye budget ya serikali hivo basi warudishe alafu wamnai kigwa kwa sababu hakuna mkataba baina ya serikali na clouds
 
Wamesema wana risiti na walilipa TRA.. ingekuwa wewe ungerudisha pesa ulizofanyia mtu kazi!!!!

Kama unataka wakuonyeshe waombe wafanye hivyo..
 
Walishafanya kazi ni vp warudishe pesa? Njia bora ni wataje kiasia halali walicholipwa
ujanja umefanyika kati ya upande mmoja na upande mwengine, kisha dili likafanyika!!
hapo kuna upigaji, hiyo kazi ni danganya toto.
njia pekee kwa boss wa CMG ni kurudisha fedha ya watanzania.
kwa mujibu wa Ripoti ya CAG hiyo fedha haikulipwa kihalali kwa clouds ndio maana walikwepa taratibu zinazo stahili. ukifuatilia sana huo mzigo hata kodi haujatozwa.
 
Ripoti ya CAG ni useless. Hamna mtu hata mmoja atalipa au kuwajibishwa, in a month tutasahau atazungumziwa tena mwakani akija na ripoti nyingine.
Ndo maana mm sihangaiki na hiyo ripoti..ukipata chocho jilimbikizie mwenyewe hii nchi haiji kuwa bora hata siku 1
 
Wamesema wana risiti na walilipa TRA.. ingekuwa wewe ungerudisha pesa ulizofanyia mtu kazi!!!!

Kama unataka wakuonyeshe waombe wafanye hivyo..
Kama Clouds wanataka kushindana na Ripoti ya CAG basi ngoja tusubiri, ila pia TAKUKURU NA FIU wachunguze hizi pesa za watanzania ambazo zimekwapuliwa kijanja.

CMG hamna moral authority ya kujadili ripoti hii ya CAG kwani mmehusishwa ktk kashfa ya kula fedha za watanzania
 
Badala ya kusukumizana nani atoke hadharani anze kuisafisha clouds ni bora uongozi ukaamua kufanya kitendo cha kizalendo na cha kiungwana, kwa kuwa imebainika fedha hiyo haikuzingatia utaratibu ktk malipo basi ni vyema wakairudisha kwanza. hiyo ndio njia pekee ya kujisafisha kuliko kuhaha na kujiosha ktk vyombo.
 
Clouds wameshajisafisha wanasema wao wanadocument na walishaziwasilisha mahala sahihi kabisa kwa iyo wao wapo safe
hawa clouds wanazidi kujipalia makaa.
kwa maelezo hayo inamaana wanataka kuwaambia watanzania kuwa CAG hakufanya kazi yake vyema.

Ripoti ya CAG inasema hakuna RISITI au kiambatanisho chochote cha malipo, kwa ufupi taratibu za malipo hazikuzingatiwa kabisaa.
sasa tuamini RIPOTI YA CAG au MHASIBU WA clouds??!!

Kati ya ripoti ya CAG na maelezo ya Mhasibu wa clouds tuamini ya nani?
 
Back
Top Bottom