Clouds Media Group Jisafisheni; rudisheni fedha

ujanja umefanyika kati ya upande mmoja na upande mwengine, kisha dili likafanyika!!
hapo kuna upigaji, hiyo kazi ni danganya toto.
njia pekee kwa boss wa CMG ni kurudisha fedha ya watanzania.
kwa mujibu wa Ripoti ya CAG hiyo fedha haikulipwa kihalali kwa clouds ndio maana walikwepa taratibu zinazo stahili. ukifuatilia sana huo mzigo hata kodi haujatozwa.
Du watanzania kusoma tu tunashindwa ,pesa iliyolipwa clouds na TBC ni halali kabisa tatizo clouds na TBC hawakutoa fiscal receipts (risiti ya kieletroniki) kiufupi hizi kampuni zinatumia fiscal invoice (invoice za kieletroniki)hakuna kubwa hapo ni kutoekewa kwako tu ndio kunakusumbua.Pesa ambayo walilipwa wasanii wa wasafi ndio haikupaswa kulipwa soma vizuri haukimbizwi na yoyote
 
Kurudisha hawawez dawa ni kwamba hawa kima wasipewe tena tenda na serikali maana ni wahuni .
 
Shina la tatizo sio CMG kupokea pesa tatizo ni kwann nankwa malengo gan serikali ilikusudia kuandaa ilo tamasha lengo lake lilikuwa ni nini hasa ? Na output yake mbona hatukuambiwa

Aliyetoa ilo wazo la tamasha la uridhi afungwe . Una kaa ofisi una buni tamasha hovyo hovyo
 
yaani kuna baadhi ya kampuni zimeanzishwa kazi yake ni kupiga dili kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi walio kabidhiwa dhamana, ikitokea dili basi wanapigiwa pande.....ndicho kinacho onekana kwenye clouds.
tunarudia tena kusema clouds ni bora warudishe hiyo fedha ya watanzania vingineyo wasubirie kudhalalika zaidi.
Clouds rudisheni MZIGO
 
hata kama walifanya kazi, ile pesa haikuwa kwenye budget ya serikali hivo basi warudishe alafu wamnai kigwa kwa sababu hakuna mkataba baina ya serikali na clouds
Kwani wao serikali wajue ile pesa imetoka kwenye budget au la! Wao walipewa deal wakafanya yao mbona uwa wanarusha matangazo ya wizara ya afya. Wakuwajibishwa ni kigwa aliyewalipa hiyo pesa na kuandaa mambo ambayo hayakuwa kwenye budget
 
Uingozi wa Clouds Media Group wanajua vizuri kilicho tendeka, wanajua hiyo ilikuwa dili halali au haramu wanajua.

CAG ni ofisi nyeti na yenye wataalamu walio bobea kamwe wasingeweza kuituhumu clouds bila kuwa na ushahidi wa kutosha, inawezekana clouds walikula njama kukwapua mzigo kwa kutumia kivuli cha tamasha la urithi.
njia pekee ya kujisafisha ni kurudisha fedha zinazo daiwa kuwa walilipwa bila hata risiti...sasa sijui yalikuwa malipo ya nini ambayo hayakuwa na stakabadhi!!!
 
Njia pekee ya kujisafisha kutoka ktk uchafu huu ulio tolewa na ripoti ya CAG na kuhusisha clouds kupokea Tz sh. zaidi ya million 600 njia pekee ya kujisafisha ni kurudisha pesa ya serikali maaana utaratibu ulikiukwa na hivyo kubatilisha utaratibu wote, hakuna uhalali wa clouds kupokea fedha ambayo haikuzingatia utaratibu vinginevyo lazima kulikuwa na njama au nia ovu ya kuiibia serikali.

Kwa sasa baada ya ripoti njia pekee ni kurudisha fedha ya watanzania badala kuanza kujisafisha kupita media zenu hiyo haisaidii kwa sasa. kwa sasa ripoti ya CAG ndio inasimama kwa uzito.

Kwa sasa Clouds Media Group hamna uhalali wa kujadili ripoti ya CAG kwa sababu nyinyi ni wachafu, kwani mnatuhumiwa kukwapua fedha za umma kwa kushirikiana na watu wasio waadilifu.

Clouds njia pekee ya kujisafisha ni kurudisha pesa ya watanzania mlio ipokea kinyume na taratibu.
Siyo lkurudisha pesa wanatakiwa kulipa kodi ya serikali!!!
 
Siyo lkurudisha pesa wanatakiwa kulipa kodi ya serikali!!!
warudishe kwanza hiyo fedha maana haikufuata taratibu za malipo.

1. Hakuna risiti iliyotolewa hivyo haifahamiki walilipwa kwa kazi/huduma gani. hapo ndipo kwenye tatizo, hakuna invoice inayo onyesha huduma iliyo tolewa. ndio maana clouds wanahusishwa kwenye ukwapuaji wa fedha ya wananchi.
warudishe ili mchakato uanze upya.
 
Wamesema wana risiti na walilipa TRA.. ingekuwa wewe ungerudisha pesa ulizofanyia mtu kazi!!!!

Kama unataka wakuonyeshe waombe wafanye hivyo..
mataga hamueleweki! Kwahiyo saiz mko against CAG mnatetea wezi? Au ndo mko against bi mkubwa? Au niaje? Hamueleweki! Mmevurugwa
 
zaidi ya milioni 600, tnapata madrasa ya shule za msingi mengi na hivyo kuepusha baadhi ya wanafunzi wetu kukaa chini ya miti.
 
Clouds wanaonewa bure. Ushaambiwa walilipwa kiasi fulani cha fedha, thats means walifanya kazi ndo maana wakaripwa. Kosa lao ni kwamba hawakudai risiti au hawakua na mkataba na serikali kwa sababu ambazo wanazijua wao.

Sisi wa kulia nae ni kigwangala ambate ndo alikua na dhamana ya pesa yetu. Huyu ndo wa kumuandama maana ndo tulimuamin na kumpa wizara.

Ukiwa mfanya biadhara una focus, kwenye pesa kuingia na kazi ya mteja kufanyika. Over.

#Cloudspigenimziki.
#Risitimnawezakudaihataleo
#Tupambanenakigwangala

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
 
Kitendo Cha hayati Magufuli kukataa utawala bora wa sheria na uwazi uneligharimu Taifa kiasi kikubwa. Watu waliiba na serikali iliwakingia kifua na hivyo Mamlaka za uwajibikaji zilishindwa kufanya kazi wakisubiria maelekezo ya Rais.

Rest in peace Mwamba... makaburi yanaenda ea kufukuliwa
 
Back
Top Bottom