SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,131
- 7,902
Baada ya kuangalia mahojiano ambayo Feisal Salum amefanya na Clouds Media, nimeshangazwa sana na kitendo chao cha kuachia mambo ya "off-air" yaruke hewani tena kwa muda mrefu.
Kuna video ambayo imekuwa inasambaa ambayo inasikika Feisal akizungumza na Wakili wake pamoja na watangazaji wa Clouds wakijadiliana nini aseme, nini asiseme na asemeje. Kwanza nikumbushe majadiliano kama hayo si kitu cha ajabu kwa mtu yoyote anayeenda kufanya mahojiano katika radio au television. Hadi viongozi wakubwa wa kitaifa, akiwemo Rais wa nchi lazima apangwe nini cha kusema na asemeje kwenye vyombo vya habari, hasa kama ni mahojiano yaliyo "sensitive" kisheria. Mara nyingine unayeenda kuhojiwa unaweza hata kutaka swali au maswali fulani usiulizwe na makubaliano haya huwa ni lazima yaheshimiwe.
Kinachonishangaza ni kwamba kituo kikubwa kama Clouds kurusha matangazo LIVE halafu kuachia kwa muda mrefu vile mambo ya "off-air" yaendelee kuruka. Kuna wakati camera zimemuonyesha Feisal muda mrefu huku kipindi kikiwa kimesimama. Hii inanifanya nianze kuhisi Clouds walikuwa wanataka kunasa kitu kutoka kwake ama cha picha au sauti kitakachomuharibia au tu kupata kitu cha kutrend.
Hivi unataka kuniambia Clouds katika urushaji wa matangazo yao hawana mtu maalumu anayemonita mambo ya sauti muda wote wa matangazo? Je huyu mtu aliyekuwa anamonita hakusikia mazungumzo hayo na hakuona umuhimu wa kukata sauti? Na pia kwa nini camera zenu zinaendelea kuruka LIVE zikimuonyesha Feisal kwa muda mrefu wakati kipindi kimesimama? Mnajua ethics za utangazaji kweli?
Mwisho nimalizie kwa kumwambia Feisal awe makini sana na kila anachokifanya sasa na hata siku zijazo maana si kila atakayemfuata atakuwa na nia nzuri na yeye. Kwa hiki anachokifanya kupigania haki zake amejijengea maadui wengi. Mambo haya ya Yanga na Simba ukiacha maslahi binafsi ya watu hayana tofauti sana na dini. Wengine watataka tu kumdhuru kisa anapingana na kiongozi wa timu yao.
Pia kutokana na uzito wa kile alichokuwa anaenda kujadili, nadhani angefanya mahojiano na mtu anayeweza kuwa serious kama Salama badala ya kwenda kwa hao wahuni ambao kwanza wanajivalia hovyo hovyo wakati mwingine bila kujali wanayemuhoji.