nadhan la msingi kujiuliza uyo pj yeye anataluma gani kuweza kutoa analysis ya faida na hasara tunazopata as a result na hao barrick kua apa nchini, wana jf tunaomba cv ya pj plz?
Pili wakati pj anaenda kutembelea barrick alikua amejiandaa kwa data za kutosha kabla hajafanya uo uchunguzi wa kutosha?
Tatu nani alimtuma kwenda kufanya iyo study? Wakati anatumwa alithaminishwa na nani kwamba yeye ni mtu sahihi?
Mi nadhan hawa pj angebaki kuchambua mambo ya bongo fleva at least uko is where they belong!
Biashara siyo kupotosha umma.Chombo cha habari ni pamoja na maakama, bunge na serikali ni mihimili mwingine ya dola.unapoongelea dola ni chombo cha umma.chukulia bunge au maakama waanze kupotosha umma tutawachukuliaje. Angalia sheria za kusadili vyombo vya habari hakuna kipengele hicho unachosema cha kupotosha umma ilimradi unapata faida.chunga sana unapochangia.Twende mbele turudi nyuma, Clouds FM kama chombo chochote cha habari kinaendeshwa kibiashara na biashara yao ni pamoja na matangazo ya biashara.
Sioni ubaya kwa wao kutumia chombo chao kujiingizia kipato kwa kuwafagilia wateja wao, Je unajua ni kiasi gani wamelipwa kwa kazi hii? Mbona hata kina Matunge na waganga wa kienyeji hujitangaza kwenye vyombo vya habari. Kwani mjumbe hauwawi na Clouds si chama cha siasa, tutenganishe siasa na biashara.
Ni dalili ya kwamba watu wanaelewa ukweli na kwamba hawataki kupotoshwa au kudanganywa.- Mkuu Hofstede, heshima mbele sana na saafi sana, sasa kumbe kuna watu wanaotaka kuingilia tena uhuru wa habari? Yaani turudi kule kule tulikotoka kwenye mikingamo na pwagu na pwaguzi!
- I mean huyu PJ ana utaalamu gani kuhusu madini mpaka m-thread mzima kumshambulia as if ni Rais wa Tanzania! Kulikoni wakuu? Huyu PJ ni waziri wa nini hasa mpaka kelele zote hizi? Tatizo la madini sio la PJ ni letu sote wananchi wa Tanzania, we have no clue kabisaa kuhusu madini, sasa tunategemea PJ ndiye aje kutuweka sawa kuhusu madini, what a joke!
- Hebu heshimuni vyombo vingine vya habari jamani, piganeni na hoja zake, lakini hizi sweeping statements za kufagilia ufisadi, bila facts wala evidence mtalimaliza hili taifa, maana itafika wakati wote tutakua mafisadi, jamani mnashuhsa hadhi ya hili neno fisadi!
Respect.
FMEs!
Bahati mbaya Barrick ki-historia hawajawahi kuwa wazuri. Jaribu ku-google kampuni ya Barrick na mazingira. Sehemu kubwa ni lawama za mabaya yake. Bahati mbaya zaidi kwetu TZ ni mazingira pamoja na corruption!
Mi nawahurumia ndugu zangu mnaopoteza muda wenu kusikiliza radio hii.
Kuna watu na akili zao timamu wakifanya mahojiano na mtu basi utakaa na kusikiliza.
Hebu kaa siku usikilize Radio deutsche welle usikie kina aboubakar lyongo, umil kher, mohamed abdulrahman, othman miraji, sekione kitojo na watangazaji na wachambuzi wenye elimu, ujuzi na uzoefu katika taaluma ya habari jinsi wanavyotangaza ama kufanya mahojiano na mtu.
Kisha uje usikie uharo wa hao clouds wanaotangaza huku wanajambisha, mara wapige kelele, mara waanze kutekenyana....
Ni uharo mtupu
Nadhani watu wanashutumu bila kuwa na data.....someni utafiti wa dr .semboja ndo mtajua nani ni nani kwenye madini..
Katika kila wakia moja inayouzwa kutoka kwenye migodi, serikali inapata jumla ya kodi mbalimbali ya asilimia 15 , production cost ni asilimia 61, kulipa madeni ya benki asilimia 12, faida kwa mwenye mgodi asilimia 10, community services 2
sasa hapo wizi uko wapi? Tatizo lipo kwenye matumizi ya hizo asilimia 15 inazo pata serikali wanazitumia je? Mathalani watu wanataka mwekezaji awaendeleze jamii inayozunguka migodi, je serikali inafanya nini? Je kila mwenye biashara anafanya hivyo....
Mfano mzuri ni royal kingdom of mafikeng south africa, wao wanapata royalty asilimia 3 ya kila mgodi ulio kwenye aridhi yao, kwakuwa viongozi wao wanajali wananchi wao, wamewajengea nyumba wananchi wao wote, wanawasomeshea watoto na pia wanawekeza kwenye sekta nyingine ili mali ikiisha wasitaabike....wamejenga uwanja kwa ajili ya world cup 2010 pale rusternburg...
Tuangalie akili za watanzania, sasa
wilaya ya kahama walilipwa milioni 220 kama mgao wao kutoka bulyankulu, milioni 110 walilipana malimbikizo ya posho za vikao, milioni 50 walitumia kwenye vikao vya kamati mbalimbali
tarime wao walitumia fedha zao zote (milioni 220) kulipia wanafunzi wa sekondari.....kwa mfano huo tu utaona tatizo ni sisiem na viongozi wao hawana vipaumbele, wao ni chama chao, wao wenyewe wananchi baadaye
Kulogwa ninakozungumzia mimi hapo ni ''literary''. Nadhani umenielewa sasa!
Hizo $ 200,000 ni kodi inayolipwa kwa halmashauri za wilaya ambako migodi hii iko. Lakini maendeleo yaliyofanywa na migodi hii ni pamoja na ujenzi wa shule za kisasa za sekondari na msingi kwa wananchi, nyumba za kisasa kwa wafanyakazi wote wanaofanya migodini zikiwa na umeme na maji na kisha wakakopeshwa na kukatwa pesa kidogo kidogo. Pia barabara zote zinazoelekea migodini hukarabatiwa na migodi hii.
Isitoshe, Bulyanhulu Gold Mine wamejenga soko la kisasa katika kijiji cha Kakola ambalo sasa hivi lina karibu mwaka mzima tangu likabidhiwe kwa uongozi wa kijiji bado halitumiki. Ukiuliza utaambiwa vikao vya madiwani havijakaa kuamua uendeshaji wa soko, au pengine wanasubiri siku JK akitembelea huko aende akalifungue. Hao ndio Watanzania mnaowatetea!
Tatizo hapa sio wawekezaji, tatizo ni serikali yenu. Nyie mlioko nje ya nchi huwa mnadhani mambo yamebadilika sana hapa nchini, lakini hakika nawaambia siku mkirudi mtasikitika sana kuona kwamba ''mind set'' ya Watanzania bado iko kwenye zama za kale za mawe....Hii ni kuanzia viongozi wao mpaka wapiga kura wenyewe!
That argument is completely irrelevant here. Ulitaka Barrick waiambie serikali kwamba hapana jamani, 3% ni kidogo sana, tunataka kulipa 20%? Ungekuwa wewe ndiye mwanahisa mkuu wa Barrick ungefanya hivyo?
Ni nani atapiga risasi mtu asiye na hatia? Tanzainia haijafikia huko. Kwa taarifa yako kama kuna watu wanafuata sheria za nchi hapa Tanzania basi makampuni ya kutoka nje, hasa ya madini yanaongoza! Sio zile biashara za wahindi wenu wajanja wajanja waoiba fedha za umma za pale BoT halafu mnawachagua kuingia bungeni!
Amedhalilishwa, period. Hoja ingejengwa kwamba hana utaalamu wa kujua kiasi dhahabu inayochukuliwa, si kwamba eti alipewa chakula, malazi na kupandishwa ndege ya Barrick ili apotoshe ukweli. Huko ni kudhalilisha!
Tatizo leni mkishakaa sana nje ya nchi basi mnadhani kila mtu anajua misamiati ya USA.....House Negro(!?) Ndio nini?