Clouds FM - Weekend Bonanza irekebishwe

Clouds FM - Weekend Bonanza irekebishwe

malipesa2014

Member
Joined
Jun 2, 2014
Posts
22
Reaction score
8
Kwa muda sasa nimekuwa mfuatiliaji wa kipindi cha weekend bonanza kinachoendeshwa na Kinyaiya na Suzy Baltazary. Kipindi hiki kimepita katika mabadiliko kadhaa lakini nadhani hayasaidii kukiboresha, bali kimezidi kuwa cha ovyo. Nadhani watangazaji (hawa wanaojiita wauza maneno wa mjini) warudishe maudhui yakinifu ya kipindi hiki. Enzi zile za weekend bonanza ilikuwa unapata vijihabari kadhaa vya kusisimua vinavyohusiana na bendi zetu. Ilikuwa unaweza kuwasikia wadau wa muziki wakijibu tuhuma au rumours zilioenea mtaani - iwe kuhama bendi, kujiunga ama uhasama baina ya wanamuziki na vijimambo kibao vinavyohusiana nao hawa wasanii wetu. Lakini siku hizi ni porojo na kusoma meseji za wasikilizaji na hata zisizokuwa na mvuto na uhusiano wowote na burudani ya muziki. Kama jana Suzy alirusha sound clips za club moja huko Arusha. The coverage's idea was ok, but sikutegemea aanze kuwauliza na walinzi changamoto wanazokabiliana nazo kwenye kazi yao! Wiki hii nzima kumekuwa na rumours kwamba Ally Choki amesaini kurudi Twanga Pepeta. Hiyo ingekuwa big story, lakini wauza maneno hawa sijui hata kama walifikiria kwamba ingesisimua kipindi na kuongeza hits za wasikilizaji. Wangemtafuta Choky, wangeongea pia na Asha Baraka hiyo interview ingekuwa hot mno! Lakini wanavyokifanya hiki kipindi wanajua wenyewe. Seriously, hii program inabidi ichongwe upya. Musa Hussein was the man for Weekend Bonanza. Haya mabadiliko yenu sometimes huwa hayasaidii, bali kupunguza ladha ya vipindi. Mnabadilisha badilisha watangazaji wa vipindi mpaka vinakuwa na rangi isiyoeleweka kama salads! Turudishieni Weekend Bonanza yenye ladha tuliyoizoea na sio hizi kelele zisizokuwa na substance ndani yake. I'm not against the presenters of this program, but i think they need to be guided on how they deliver the intended context.
 
Suzy Baltazary kipindi ni kikubwa kwake,ushamba haujamtoka bado huyu...maneno ambayo anaongea huko kwe kpndi unajiuliza huyu anafanya kipindi au anakitu zaidi anataka?? Nafikiri ndio maana hata kipindi chao kimekosa mvuto kama enzi za Musa,nadhan Ben atakua anapata tabu sana though hasemi
 
Back
Top Bottom